Mkuu wa chuo cha mafunzo ya ufundi stadi cha Donbosco Manispaa ya Iringa padre akitoa rai kwa wanafunzi wake chuoni Donbosco.
ZAIDI ya wanafunzi elfu 18 wamekosa nafasi ya kujiunga na masomo ya
elimu ya mafunzo ya ufundi stadi VETA, kutokana na uchache wa fulsa hiyo ndani ya vyuo 26 vilivyopo katika mikoa yote hapa nchini.
Hayo yamezungumzwa na meneja wa VETA kanda ya nyanda za kusini Aleus Tubike katika mahafali ya 17 ya wanafunzi wa chuo cha VETA Iringa, kilichopo katika manispaa ya Mjini wa Iringa, ambapo amesema katika kipindi cha miezi 3 mwaka huu jumla ya vijana elfu 20 pekee ndiyo waliobahatika kupata nafasi za kujiunga na masomo hayo ya ufundi kati ya maombi elfu 20 waliyopokea nchini, na hivyo wanafunzi elfu 18 kukosa fulsa hiyo ya masomo.
Tubike alisema idadi hiyo ya wanafunzi waliokosa fulsa ya kujiunga na vyuo hivyo ni kubwa na hivyo kuwataka wanafunzi walioipata fulsa hiyo kuitumia vyema kwa kujituma kusoma kwa bidii ili kuyafikia malengo yao .
Na kuwa katika kuiepusha jamii na dhana tegemezi ya ajira, VETA imeanzisha mpango wa kutoa elimu ya masomo Ujasiriamali kwa wanafunzi wa vyuo vyote vya ufundi nchini, ili kuwaongezea uwezo na ujuzi wa kubuni shughuli mbalimbali za kiuchumi.
Hata hivyo Tubike amesema VETA nyanda za juu imepokea jumla ya vijana elfu moja pekee ambao watajiunga na vyuo hivyo vya ufundi katika mikoa mitatu ya Njombe, Ruvuma na Iringa, huku idadi ya wanaohitaji kujiunga na mafunzo hayo ikiwa ni kubwa zaidi.
Mkuu wa chuo hicho cha VETA Iringa - Hamenya Ntabaye alisema tatizo kubwa linalokikabili chuo ni pamoja na ukosefu wa sehemu kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo, kutokana na vikwazo vya baadhi ya wadau kuwakataa wanafunzi kufanya mafunzo kwa vitendo katika maeneo yao ya kazi, huku baadhi yao wakidai fedha za utoaji wa mafunzo hayo ya vitendo, na pia kukosekana kwa vifaa na mashine za kisasa kunachangia kushindwa kwenda na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.
Wakisoma risala ya wanafunzi, wahitimu Deus Vapefya na Oliver Adriano walisema changamoto kubwa inayowakabiri ni upungufu wa vifaa vya kufundishia katika karakana, ukosefu wa vifaa, mitambo na mitambo kuwa ile iliyopitwa na wakati, na kusababisha baadhi ya mafunzo yanayotolewa kuwa ni yale yasiyoendana na wakati uliopo, kutokana na mitambo mingi kuwa niya kizamani.
Vapefya alisema pia wanakabiliwa na changamoto ya vitabu vya rejea kwa baadhi ya fani, huku tatizo kubwa linalodumaza taaluma hiyo ni ucheleweshaji katika kupata vyeti vyao vya kuhitimu elimu hiyo, pamoja na utoaji wa vyeti ngazi ya cheti wakati elimu waliyoipata niya miaka mitatu na hivyo kuonekana elimu hiyo duni wakati wa kutafuta ajira.
"Mitambo na mashine nyingi zilizopo hapa chuoni ni zile zilizopitwa na wakati, na hivyo inatuwia vigumu kuendana na ulimwengu huu mpya wa sayansi na teknolojia kwa hiyo inakuwa ni vigumu katika kuleta ufanisi wa kiteknolojia,"
Wahitimu hao walisema kukosekana kwa walimu wa baadhi ya masomo mtambuka, kama somo la ujuzi wa mawasilino na biashara, ni changamoto inayowasumbua kwa kiwango kikubwa katika upatikanaji wa elimu hiyo.
Hata hivyo walisema baadhi ya makampuni na mashirika mengi nchini bado yanatambua mfumo wa zamani wa mafunzo uliokuwa ikiendeshwa na VETA, kwani mafunzo hayo mapya ya "Basic assesment" bado hayajatambulika, huku wakiomba chuo kiwe na jukumu la kuwatafutia wanafunzi sehemu za kufanyia mafunzo kwa vitendo ili kupata ujuzi thabiti.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment