Tuesday, November 26, 2013

MUME AMVUNJA MKEWE MIGUU YOTE KWA LISASI HUKU WATU 106 WABAKWA

WAKATI maadhimisho ya kutokomeza ukatili wa kijinsia yakiendelea kote nchini, mwanamke Frolida Lalika (24) mkazi wa kijiji cha Ilasa katika Wilaya ya Mufindi mkoni Iringa, amelazwa katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa iringa baada ya kupigwa lisasi ya miguu na mume wake.

Akizungumzia mkasa huo, Frolida ambaye ni mwathirika wa matukio ya ukatili, akiwa amelazwa katika word namba 7 kwa zaidi ya miezi sita amesema tukio hilo limempata tarehe 18 mwezi wa sita mwaka 2013, ambapo mume wake huyo alimtaka warudiane baada ya kutengana kwa muda.

“Mume wangu alifikia hatua ya kunitelekeza baada ya kupata mwanamke mwingine, alihama katika nyumba ya shule tuliyokuwa tunaishi, akaondoka na kuniacha mimi na watoto wangu wawili ambao nilikuwa nimezaa naye, na nilipoona maisha magumu niliamua kuondoka katika nyumba hiyo na kurudi kwa wazazi wangu, lakini baada ya kuona wanashindana na mwanamke wake alianza kunifuata mimi nyumbani kwa wazazi akitaka turudiane, mimi nilikuwa ninamkatalia na siku hiyo ya tarehe 18 alikuja nyumbani na kuniita nje huku akisisiotiza jambo hilo la kurudi nyumbani nilipomuonyesha msimamo wangu wa kutotaka kurudiana nae ndipo aliponipiga risasi ya mguu, grory za bunduki ili zilinifunja miguu yangu yote miwili, mpaka sasa nipo hapa ni zaidi ya miezi sita,” Alisema Frolida.

Frolida licha ya kukaa kwa muda wote huo wordin akiwa amelala na hivyo shughuli zake nyingi za kiuchumi kusimama, ameanza kufanya mazoezi ya kutembea kwa kutumia vifaa maalumu vya usaidizi, huku mguu mmoja ukiwa umeathirika zaidi na hivyo kushindwa kutembea, jambo ambalo huwenda likamsababishia mwanamke huyo ulemavu wa kudumu.

Akizungumzia uwepo wa matukio ya ukatili mkoani Iringa,
Monica Lyelu- ambaye ni afisa huduma ya mama na motto katika Hospitali ya rufaa mkoa wa Iringa amesema tatizo la ukatili wa kijinsia ni kubwa kutokana na kuwepo kwa matukio ya ubakaji 106.

Lyelu amesema jumla ya matukio hayo nikwa kipindi cha miaka mitano ambapo mwaka 2009 watu 17 walifanyiwa vitendo hivyo watu.

Aidha Lyelu amesema mwaka 2010 walibakwa watu 22, 2011 walibakwa watu 16, mwaka 2012 waliofanyiwa ukatili huo walikuwa 27 na mwaka huu 2013 walibakwa 24.

Pia amesema waathirika wa matukio hayo ya ubakaji wengi ni wale walio na umri wa miaka 6 hadi 15, ambapo baada ya kufika hupatiwa huduma ya haraka ili kuwakinga na magonjwa ya kuambukizwa yatokanayo ngono ukiwemo ugonjwa wa ukimwi.

Nuru Mhagama ambaye ni afisa muuguzi kitengo cha ukatili wa kijinsia katika Hospitalia ya Rufaa mkoa wa Iringa amesema Hospitali imepokea jumla ya wagonjwa 139 wa matukio yatokanayo na ukatili wa kupigwa huku wengi wao wakiwa wanaume.

Nuru amesema takwimu kubwa ya vipigo kwa upande wa wanaume vinatokana na kuvamiwa na majambazi, au ugomvi sehemu za vileo, huku matukio ya wanawake yakihusisha masuala ya mahusiano.

“Tunapokea wagonjwa wengi sana wa matukio ya ukatili yatokanayo na vipigo, lakini hapo awali tulikuwa hatuyaweki katika kumbukumbu, ila wanaume ndiyo wengi zaidi, na wengi katika maelezo yao wamekumbwa na tatizo hilo kwa kupigwa na vibaka njiani, au katika sehemu za pombe, lakini wanawake wengi tunaowapokea wamepigwa na wapenzi wao au waume zao,” alisema.

No comments:

Post a Comment