Tuesday, December 3, 2013

SAO HILL YAFUTA TATIZO LA MADAWATI MUFINDI

 Madawati yakiwa yamewasiri  katika viwanja ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi mkono Iringa, yakiwa yametolewa na uongozi wa Shamba la miti la taifa la sao hill lililopo Wilayani Mufindi mkono Iringa.
 Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Evarista kalalu (Tshirt ya Bluu) akiwa na maofisa wa sekta ya elimu wilayani Mufindi, pamoja na walimu wakuu wa shule zinazopatiwa msaada huo wa madawati.
 Madawati zaidi ya 100 ambayo yamekabidhiwa na uongozi wa Shamba la Sao hill katika kata ya Igowole Wilayani Mufindi. 
 Afisa elimu vifaa na takwimu shule za msingi Mufindi Bw. Faustine Mhapa akiwa katika moja ya mgao wa madawati.
 Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Bi. Evarista Kalalu (mwenye Tshirt ya Bluu) akitoa ujumbe wakati wa mgao huo kwa wakuu wa shule za msingi.
 Afisa elimu Vifaa na takwimu shule Msingi Bw. Faustine Mhapa akisikiliza jambo katika hafla ya mgao wa madawati kwa shule za Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Moja ya migao ya madawati inayotolewa na uongozi wa Shamba la miti la taifa Sao hill, mkakati ambao umelenga kutokomeza tatizo la madawati katika shule Wilayani Mufindi.

SHAMBA la miti la Taifa Saohill, lililopo katika Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa limetoa msaada wa madawati 2469, yenye thamani zaidi ya shilingi Milioni 111, katika shule zenye changamoto hiyo ya madawati.

Akikabidhi msaada wa madawati hayo, meneja msaidizi wa shamba la miti la Taifa Saohill Bw. Shadrack Bijura amesema lengo la mkakati huo ni kuwaepusha wanafunzi na adha ya kukaa sakafuni kwa kukosa miundombinu hiyo ya Madawati.

Afisa elimu Wilaya ya Mufindi Bw. Faustin Mhapa amesema Wilaya hiyo inauhaba wa madawati elfu 11, 341, kutokana na kuwa na madawati 17, 403 katika shule za serikali 173 zenye jumla ya wanafunzi elfu 63, 089.

Aidha Mhapa amesema msaada huo wa madawati kutoka Shamba la Taifa la Saohill utazisaidia shule 30, madawati yanayotokana na vibali vya kupasua mbao katika Msitu huo na kuweza kutoa jumla ya madawati elfu 2,469.


Amesema kukosekana kwa madawati kumekukifanya tendo la ujifunzaji na ufundishaji kuwa mgumu, na kuwa msaada huo utasaidia wanafunzi kushiriki vyema katika masomo kinadharia na vitendo.

“Katika tendo la ujifunzaji na ufundishaji, unawezeshwa pia na uwepo wa madawati, hiyo ni nyenzo muhimu sana ya kuweza kumsaidia mwanafunzi kushiriki katika kujifunza na mwalimu kuweza kumshirikisha vyema mwanafunzi katika vitendo na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi anatoa mchango katika nadharia na vitendo,” Alisema Mhapa.

Aidha amesema anatambua uwepo wa changamoto kubwa ya uhaba wa madawati katika Wilaya hiyo, na ipo haja ya kushirikiana kwa pamoja katika kuboresha mazingira ya elimu ya wanafunzi.

Naye kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo ya Wilaya ya Mufindi Bw. Isaya Mbenje amewataka walimu na wanafunzi kuyatunza madawati hayo, ili yaweze  kutumika kwa muda mrefu, katika kupunguza tatizo hilo.

Mbenje amesema tatizo la uhaba wa madawati uliopelekea baadhi ya wanafunzi kukaa chini na wengine kukalia madawati ya udongo ni jambo la aibu na linapaswa kuwa  historia pekee, kwa kuendeleza kampeni hiyo ya kuboresha sekta ya elimu.

“Wanafunzi katika Wilaya yetu ya Mufindi kukaa chini au kubanana sasa itabaki Historia,  kwani sisi tunazalisha miti na mbao nyingi, lakini jambo la muhimu hapa ni utunzaji wa madawati haya ambayo tumesaidiwa na hawa wadau wetu, mimi nitahakikisha ninapita katika shule zote ambazo mmepatiwa msaada huu, kuangalia kama mnayatunza, pindi yanapoharibika muhakikishe mnayafanyia ukarabati, madawati haya yanatengenezwa kwa gharama kubwa sana,” Alisema Mbenje.

Amewataka walimu kutumia fedha za uendelezaji wa shule “Capitation” pia kuzitumia katika ukarabati wa madawati yote yanayoharibika, huku akiahidi kulifuatilia suala hilo kwa madai kuwa haiwezekani kila mwaka wilaya hiyo ikawa ombaomba wa madawati.

Wakipokea msaada huo walimu wakuu Hilda Balama wa shule ya msingi Itulavanu na  Paspol Shodan Haule mwalimu mkuu wa shule ya msingi Bumilayinga wamesema msaada huo umesaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza tatizo la upungufu wa madawati shuleni kwao.

Mkuu wa Wilaya hiyo ya Mufindi Bi. Evarista Kalalu amesema kila kijiji ambacho shule zake zimepatiwa mgao huo wa madawati havitakuwa na tatizo hilo, na kuwa sasa kila Kata itapatiwa madawati 129 ambayo yatasaidia shule za Kata husika.

Kalalu amesema atahakikisha upungufu wa madawati unakwisha katika Wilaya yake, kwani kwa sasa  kuna uchongaji wa madawati 1,218 kwa kila Kata,  kwa jumla ya Kata 28 huku Kata ya Saohill peke yake ikichonga madawati 129 yatakayosaidia shule tatu.

Amesema katika awamu nyingine shule 30 pia zitapewa madawati, na kuondokana na tatizo hilo la upungufu wa madawati, huku vijiji 26 vikiwa vimepatiwa mgao huo huku vijiji vyote vikisisitizwa kipaumbele cha uchongaji wa madawati.

Amesema ipo haja kwa jamii kuona umuhimu wa kuwatengenezea wanafunzi mazingira mazuri ya kujisomea, huku akiwaomba wadau wote kuona umuhimu wa kuchangia madawati kwa shule za msingi, ili changamoto ya upungufu wa madawati kubaki historia katika Wilaya hiyo.

Hata hivyo mwezi wa nane mwaka huu uongozi wa shamba hilo la Taifa la Sao hill lilitoa msaada wa madawati 100 kwa shule zilizopo katika Kata ya Mtwango Wilayani Mufindi, jambo ambalo linaashiria nia thabiti ya uongozi wa Shamba katika kutokomeza kabisa tatizo hilo la ukosefu/ upungufu wa madawati katika Wilaya hiyo ya Mufindi.

Meneja msaidizi wa shamba hilo la Sao hill Shadrack Bijuro wakati huo alisema shamba limekuwa likitoa vibali vya bure vya ukataji wa miti kwa vijiji 58 vinavyolizunguka huku shamba pia likitoa shilingi milioni 25 kwa miaka minne mfululizo lengo likiwa ni vijiji  kumaliza matatizo yao wanayoyapa kipaumbele.

Ambapo Mandalo Abeid Salum afisa misitu idara ya mipango na matumizi ya rasilimali za miti alisema kuna utaratibu wa kutoa migao ya miti kwenye vijiji 58 vinavyozunguka shamba, huku asilimia kubwa ya shule wilayani humo zikikabiliwa na tatizo la madawati.

Mandalo alisema rasilimali ya shamba hilo ni kubwa na kuwa kuna umuhimu kwa wananchi husika kutoa taarifa za vipaumbele katika vijiji vyao ili kumaliza changamoto zinazowakabiri kupitia migao ya meta za vibari vya bure vinavyotolewa na shamba hilo.

Afisa elimu ufundi Faustine Mhapa kwa kipindi hicho alisema kupitia vibali vya bure kutoka Shamba hilo la Saohilo, wamefanikiwa kupata jumla ya madawati 2469 ambayo yamechongwa na kupunguza tatizo la uhaba wa madawati kwa shule za msingi 32.

Mhapa alisema wilaya ina jumla ya shule za msingi za serikali 173 zenye jumla ya wanafunzi 67, 089 huku madawati yakiwa 11,341 kati ya madawati 17, 403 yaliyopo na hivyo shule 141 zikiwa na upungufu wa madawati.
 

"Mufindi tuna jumla ya shule za msingi 173 za serikali ambazo zina jumla ya wanafunzi 67, 089 na madawati tuliyonayo ni 11,341, kati ya 17, 403 kwa hiyo shule 141 zina upungufu wa madawati," Alisema Mhapa.

Na kuwa katika kipindi cha mwaka 2012/ 2013 jumla ya madawati 2469 yalitengenezwa kupitia utaratibu wa vibali vya kupasua mbao huku jumla ya shule 32 zilizopo katika kijiji cha Kiyowela, Lugema, Lugolofu, Kilolo, Rungemba, Itulavanu, Igowole, Mkalala na Ikwega vikinufaika na mgao huo.

Vijiji vingine ni Itona, Kibao, Ifupira, Ifwagi, Igomtwa, Udumuka, Ibatu, Ihanu, Kilosa, Bumilayinga, Mapnada na Kisada,  kijiji cha Ihomasa, Mkonge, Igoda, Ludilo, Igeleke, Kibengu, Iyegeya, Ugesa na Chogo.

MWISHO









No comments:

Post a Comment