Walimu na baadhi ya maafisa wa FAWE na
TUSEME wakisikiliza jambo kutoka kwa wanafunzi waliopo katika kambi ya
siku tatu, Wilayani Mufindi Iringa.
Baadhi ya wanafunzi
washiriki wa Clab ya TUSEME kutoka katika Wilaya mbalimbali nchini
wakiwa katika Kambi ya siku tatu katika ukumbi wa shule ya sekondari JJ
Mungai, iliyopo Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa. Mratibu wa FAWE Taifa Bi. Neema Kitundu (wakwanza kulia) akiwa na baadhi ya walimu wawakirishi wa mradi wa TUSEME wakishangilia jambo kutoka kwa wanafunzi waliofika katika Kambi hiyo ya siku tatu, wakijadili changamoto mbalimbali zinazowakabili watoto wa kike katika sekta ya elimu.
"Baadhi ya walimu wakisikiliza ujumbe kutoka kwa wanafunzi wao wa club ya TUSEME, wanafunzi wanaopatiwa elimu ya namna ya kupinga ukatili na unyanyasaji wa kijinsia kwa mtoto wa kike, kwa kusema pasipo kusubiri kusemewa.
Wanafunzi wa club ya TUSEME wakiwa katika maandamano ya kupinga unyanyasaji na ukatili wa kijinsia kwa mtoto wa kike katika sekta ya elimu, mradi unaoendeshwa kwa ufadhili wa UNICEF chini ya shirika la FAWE.
Wanafunzi wa club ya TUSEME wakiingia kwa maandamano katika viwanja vya shule ya sekondari JJ Mungai, kujadili masuala mbalimbali yanayowakwamisha watoto wa kike kunyimwa haki zao za msingi ikiwemo haki ya elimu.
Profesa Penina Mlama- Mwakirishi wa TUSEME Tanzania, akifafanua jambo nje ya kambi ya club ya wanafunzi wanaotete haki za watoto wa kike "TUSEME", katika shule ya sekondari JJ Mungai Wilayani Mufindi- Iringa.
<<<<<HABARI>.>>>>
SHIRIKA la Forum For Africa Women Educationalists (FAWE) linalojihusisha
na elimu kwa motto wa kike, chini ya mradi wa TUSEME ambao unatoa
malezi ya elimu ya kujitambua, kujiamini, kujithamini na kutete haki zao
kwa wanafunzi wa elimu ya msingi na sekondari, imewakutanisha wanafunzi
wa Wilaya tisa nchini, ili kutambua changamoto zinazowakabiri.
Akizungumza katika sherehe za
uzinduzi wa kambi ya wanafunzi hao, kambi iliyopo katika shule ya
sekondari JJ Mungai katika Wilaya ya Mufindi mkoni Iringa, mratibu wa
FAWE Tanzania Bi. Neema Kitundu amesema Wilaya zilizoshiriki katika
kambi hiyo ni Temeke, Njombe, Mtwara na Mbeya Vijijini.
Bi. Kitundu amesema Wilaya
nyingine ni Mufindi, Iringa vijijini pamoja na Makete, huku Wilaya mbili
ya Magu na Mbarali ya mkoni Mbeya, zimeshindwa kuhudhuria shughuli
hiyo.
Aidha Bi. Kitundu amesema
shirika la FAWE lilianzishwa Afrika mnamo mwaka 1992, huku nchini
Tanzania likianza mwaka 1996 ambapo lengo lake kuu lilikuwa ni kujenga
uelewa kwa jamii juu ya haki ya elimu kwa motto wa kike.
Amesema pia shirika huhamasisha
watoto wa kike kuwa na uthubutu wa kuchukua masomo ya Sayansi ili waweze
kuingia katika taaluma mbalimbali kwa usawa baina ya motto wa kike nawa
kiume.
Amesema shirika la FAWE limekuwa
likiboresha vituo vyake kwa kujenga majengo yanawewezesha upatikanaji
wa elimu bora, kwa kuyaweka mazingira rafiki kwa elimu katika jinsia
zote.
“FAWE tunajihusisha pia na uboreshaji wa mazingira rafiki ya elimu, kwa kujenga majengo yanayoisapoti elimu, mfano kama
hapa tulipo JJ Mungai, FAWE tumeweza kujenga Maktaba bora naya kisasa,
na pia tumejenga hili jengo la kulia Chakula (Dinning Hall),” Alisema
Kitundu.
Mwanzirishi wa TUSEME nchini
Profesa Penina Mlama amesema tangu kuanzishwa kwa mradi huo mwaka 1996
kumekuwa na mafanikio makubwa, kwa kuzifikia nchi 25 barani Afrika,
ikiwa pamoja na mtoto wa kike nawa kiume kutambua haki stahiki dhidi
yao.
Proffesa Mlama amesema akiwa
chuo kikuu cha Dar es salaam yeye na mwenzie Amandina Lihamba
walianzisha mpango huo kwa lengo la kuondoa mfumo dume katika jamii,
ambao umekuwa ukimkandamiza zaidi mtoto wa kike, kwa kumbana katika haki
ya elimu.
Amesema licha ya TUSEME kumpa
uwezo mtoto wa kike ili aweze kutambua changamoto zinazomkabili na
kuzitete mwenyewe, pia wanawajengea uelewa watoto wa kiume kuacha tabia
ya wao kujiona ni bora zaidi kuliko kike, na lengo likiwa ni kuleta
usawa kuanzia ngazi ya familia, jamiii na Taifa kwa ujumla.
Kaimu afisa elimu mkoa wa Iringa Mwalimu Ezekiel Kiagho ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi wa hafla hiyo, amesema shirika hilo
ni chachu katika sekta ya elimu, kutokana na ukweli kuwa baadhi ya
wazazi na walezi wamekuwa wakiwabagua watoto wa kike katika afua ya
elimu.
Kiagho amesema kutokana na elimu
inayotolewa na FAWE kupitia mradi wa TUSEME jamii imepata uelewa dhidi
ya haki sawa baina ya motto wa kike nawa kiume kwa kuona umuhimu wa
kuwapeleka watoto wote shule.
Hata hivyo watoto washiriki
waliopo katika kambi hiyo, Erick Kisima, Irene Nyavanga wanafunzi kutoka
Wilaya ya Mufindi na Jennifer Steven Luvanda kutoka Wilaya ya Makete
wamesema bado baadhi ya wazazi na walezi wanaendeleza ubaguzi kwa watoto
wa kike katika suala zima la elimu, na majukumu ya kazi za nyumbani,
huku baadhi ya familia zenye uwezo wa fedha nazo zikishindwa
kumuendeleza mtoto wa kike kwa dhana potofu na iliyopitwa na wakati kuwa
“Mtoto wa kike niwa kuolewa”.
“Wazazi tukifika nyumbani, sisi
watoto wa kike ndiyo tumekuwa tukifanyishwa kazi nyingi, tofauti na
wenzetu watopto wa kiume, hii inachangia kukosa muda wa kutosha
kujisomea, tunawaomba wazazi na walezi wetu watugawie majukumu ya kazi
za nyumbani kwa usawa ili kutupunguzia mzigo wa kazi,” Alisema Jennifer
na Irene Nyavanga.
No comments:
Post a Comment