Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo- Mkoni Iringa
Wataalamu wa masauala ya afya katika
Halmashauri ya wilaya ya Kilolo, wa kwanza kulia ni Bi. Faraja Chaula,
mratibu wa Ukimwi Wilaya ya Kilolo, akiwa na kaimu mganga mkuu wa Wilaya
ya Kilolo Bw. Nimroad Chengula.
Bi. Faraja Chaula akisikiliza kwa
makini jambo, katika moja ya vikao vya baraza la madiwani wa Halmashauri
ya Wilaya hiyo, akiwa na kaimu mganga mkuu wa Wilaya ya Kilolo Bw.
Nimroad Chengula.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya
kilolo Mh. Joseph Muumba (mwenye joho jekundu) akiwa na makamu
mwenyekiti wake, katika moja ya vikao vya baraza la madiwani.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya
kilolo Bi. Rukia Muwango akiwa ndani ya ukumbi wa mikutano katika
Halmashauri yake, wakati wa kikao cha baraza la madiwani.
Bw. Benson Kilangi mmoja wa maafisa
wilayani Kilolo akisikiliza jambo na mkurugenzi Bi. Rukia Kiwango katika
ukumbi wa mikutano wa Wilaya hiyo.
Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo wakiwa katika majukumu yao ndani ya kikao cha baraza la madiwani.
Jengo la halmashauri ya Wilaya ya kilolo.
<<<<<HABARI>>>>>
HALMASHAURI
ya Wilaya ya Kilolo imetoa msaada wa Mbuzi 18 kwa waathirika wa ugonjwa
wa ukimwi wa kikundi cha Matumaini kilichopo kijiji cha Kitumbuka,
msaada wenye lengo la kuwaongezea mtaji katika kukuza uchumi wao na
kuwaepusha na hali duni.
Akikabidhi Mbuzi hao wenye thamani zaidi
ya shilingi Milioni 1 na nusu, katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi
duniani, iliyofanyika katika Kijiji cha Kitumbuka, mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Mh.Joseph Muhumba amesema msaada huo
utawawezesha waathirika hao kuendelea kuzihudumia familia zao.
Aidha Muumba amesema jamii inatapaswa
kufahamu kuwa waathirika wa ugonjwa wa ukimwi wanauwezo wa kuchangia
shughuli za maendeleo kwa kufanya kazi, huku akiwataka wananchi kutambua
kuwa kupata maambukizi sio mwisho wa maisha.
Amesema mapambano dhidi ya Virusi vya
Ukimwi ni jukumu la kila mmojawapo na hivyo jamii iache kuona kuwa
wajibu huo niwa Taasisi, Mashirika yasiyo ya kiserikali pamoja na
serikali, kwani fikra hizo ni potofu.
Amewataka wananchi kuona ugonjwa huo ni
sawa na magonjwa mengine kwa kuupa kipaumbele katika kupima, na kuacha
tabia ya unyanyapaa kwa wathirika, kwa kuwa nao wanao mchango mkubwa wa
maendeleo na uchumi katika Taifa.
“Ndugu zangu, ugonjwa huu mnapaswa
kuuona kama yalivyo magonjwa mengine, muwe na utayari wa kupima ili mjue
afya zenu kama mnavyofanya kwa maradhi mengine, lakini hata
ukigundulika unamaambukizi siyo mwisho wa maisha yako, unatakiwa
kuzingatia tu ushauri wa wataalamu na kasha kuendeleza majukumu ya
maendeleo kama kawaida, siyo mtu unatambulika umeathirika sasa hata kazi
hufanyi, au wananchi wanaona kuwa wewe ndiyo huna mchango, hapana,
tunatakiwa kubadili sana fikra hizo potofu kwa ukimwi ni ugonjwa kama
maradhi mengine kama Malaria, na yatupasa sote tuwajali na kuwapa faraja
wenzetu walioathirika ili waweze kuishi,” Alisema Muumba.
Pia Muumba amewasihi wale wote wanaoishi
na VVU na kutumia dawa za kupunguza makali ya Virusi vya Ukimwi (ARV’s)
kuacha tabia ya kutofuata masharti ya matibabu yao, kwa madai kuwa kupuuzia dawa hizo kunawasababishia wao wapoteze maisha.
Semeni Monge mmoja kati ya wanufaika wa
msaada huo wa Mbuzi amesema, msaada huo utawaboresha maisha yao, kwani
madai kuwa mifugo hiyo wataitumia kama mtaji wa kukuza uchumi katika
kuzihudumia familia zao.
Mwenyekiti wa kikundi cha Mshikamano,
cha wanaoishi na Virusi vya ukimwi Bw. Leonard Chusi amesema msaada huo
unaongeza imani kwao ya kuwa jamii inawajali, tofauti na awali jamii
ilivyokuwa na tabia ya kunyanyapaa, jambo lililochangia baadhi yao kupoteza maisha kwa hofu.
Hata hivyo mratibu
wa Ukimwi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Bi. Faraja Chaula
amesema Wilaya hiyo ina asilimia 9.1 cha watu wanaoishi na Virus vya
Ukimwi, na kuwa sababu kubwa ya tatizo hilo ni pamoja na jamii kuendekeza mila na destuli potofu zilizopitwa na wakati.
Bi. Chaula amesema pia tatizo la ulevi
wa kupindukia na jamii kutotumia Kondomu kwa usahihi wakati wa
kujamiiana ni sababu zinazochangia maambukizi mpya ya VVU na hivyo
kuwepo na idadi kubwa ya waathirika wa ugonjwa huo wa Ukimwi.
“Zipo sababu nyingi zinazochangia
ongezeko la watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi katika Wilaya yetu ya
Kilolo, sababu hizo ni Ulevu uliokithiri, jamii kuendeleza mila na
destuli zilizopitwa na wakati kama vile imani za kulogwa, kurithi
wajane/ wagane bila kupima afya zao, kuhudumia wagonjwa pasipo kuchukua
tahadhari ya kujikinga, lakini pia kuna tatizo la jamii kutotumia
Kondomu kwa usahihi na muda wote wakati wa kujamiiana, huku mwingiliano
mkubwa wa watu unaosabishwa na uwepo wa barabara kuu itokayo Dar es
salaam kuelekea Mbeya, ni suala linalochangia Wilaya yetu kuwa na idadi kubwa ya wafanyabiashara wa mali mbichi na mali kavu,” Alisema Chaula.
No comments:
Post a Comment