Tuesday, July 24, 2012

RUJEWA HOUSE OF TALENTs - RHT OFISA MICHEZO WA WILAYA HAWAONEI HURUMA??


Hili ni jengo la RHT- Rujewa House Of Talents, lililopo katika mji wa Rujewa, Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, jengo hili ndilo linategemewa kuibua vipaji vya vijana, Wizara ya habari na michezo kuna haja ya kuhoji fedha za kitengo cha michezo katika Wilaya hiyo.

Hali hii inavunja mioyo ya vijna  kupenda michezo mbayo kwa sasa ni moja ya ajira kubwa hapa nchini, kutokana na idadi kubwa ya wasanii marusu kutokea katika makundi hayo ya vipaji.


Kwa kuwa lengo ni kuinua vipaji, kuna kila sababu ya kuwatazama vijana wenzenu hawa wa RHT- Rujewa House of Talents, kwa ni kma unavyoliona jengo hilo hapo juu ndiyo ofisi yao na eneo l kufanyia mazoezi.THT- TANZANIA HOUSE OF TALENTS ni nyota  ing'aayo katika sana.  "THT" si jina geni masikioni mwa watu wengi hapa nchini na hata nje ya nchi yetu ya Tanzania , ni vijana wanao unda kundi la sanaa mbali mbali ikiwemo music na dance , kundi linafanya vizuri sana kwa sasa , vichwa vikali kama Barnaba , Linah ,Pipi, Mwasiti , Dogo Dito, Sam , Mataluma na wengine wengi ni baadhi ya zao la THT , kundi hili la THT lipo chini ya Redio ya Clouds FM.





Hali hiyo inashiria ni kiasi gani baadhi ya maofisa michezo wasivyojua wajibu wao, kwani kuna ubaya gani vijana hao wanaohangaika katik PAGARE hili wakapangiwa japo ofisi yenye chumba kimoja na Halmashauri kupitia ofisi ya michezo ikawa inalipa kodi, kwa lengo la kukuza sekta hiyo ya michezo kwa kuboresha vipaji vya vijana na wanajamii husika.

  

No comments:

Post a Comment