Sunday, July 22, 2012

MWANAVALA WAUNG'OA UONGOZI WA SERIKALI


WANANCHI wa kijiji cha Mwanavala kilichopo katika Halmashauri ya Wilya ya Mbarali mkoani Mbeya wameuondoa uongozi wa serikali ya kijiji hicho kwa madai ya kuhujumu mali za serikali ikiwemo ardhi ya kilimo.



Wananchi hao wamefikia hatua hiyo baada ya siku chache kuandamana hadi katika shamba la MNAZI lililopo ndani ya kijiji hicho ili kugawana mashamba ambayo yameuzwa pasipo kushirikishwa na hivyo wao kukosa ardhi ya kilimo.



Hatua ya wananchi hao kuuondoa uongozi wao madarakani imetokana na uongozi huo kushindwa kutimiza ahadi  katika mkutano ambao uliitishwa na viongozi hao kwa lengo la kumaliza mgogolo huo, baada ya kuwasitisha wananchi hao kutochukua uamuzi huo wa kugawana mashamba.


Hata hivyo mkuu wa Wilaya ya Mbarali Bw. Guramhussein Kifu amesema hatua ya wananchi kuvunja uongozi wa serikali ya kijiji hicho haitambui kwa kuwa haujafuta sheria na taratibu  zinazotakiwa kufuatwa, na kuwa atafika katika kijiji cha Mwanavala ili kusikiliza kero za wananchi hao.


Uamuzi  wa wananchi hao unatokana na wao kukosa ardhi ya kilimo, na hivyo kuwa mashuhuda wa kuona magari yanayopita na mazao yanayotoka katika ardhi yao, yakichukuliwa na wananchi wasio wakazi wa kijiji hicho.


No comments:

Post a Comment