Mkamu mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Iringa, Bw. Henry Mangenya akifuatilia jambo katika moja ya mafunzo ya wafanyabiashara katika Kata ya Matamba wilaya ya Makete, mkoa mpya wa Njombe (Iringa)
Mshauri mwezeshaji wa TCCIA mkoa wa Iringa Bw. Dustun Mpangala akitoa mafunzo kwa wafanyabiashara, hiyo ikiwa ni moja ya kufikisha elimu juu ya madhara ya Lumbesa.
Bw. Dustun Mpangala akitoa mafunzo kwa wafanyabiashara,
Mkufunzi Bw. Dustun Mpangala akitoa mafunzo kwa wafanyabiashara,
Mmoja wa wanufaika wa elimu ya vipimo vya mizani kutoka mkoa wa Iringa Bw. Mwalubandu akifuatilia jambo kwa ukaribu zaidi.
Mwenyekiti wa TCCIA Wilaya ya Ludewa Bw. Charles Mwasanga akifuatilia mafunzo ya elimu ya matumizi ya vipimo vya mizani Wilayani humo
Diwani wa Kata ya Ludewa Bi. Monica Mchilo akichangia madhara ya vipimo vya mabede, Plastiki na Ndoo.
Picha ya pamoja ya wafanyabiashara wa MATAMBA wilaya ya Makete, wakiwa na wawezeshaji wa TCCIA na wanahabari.
Picha ya pamoja ya wafanyabiashara wa Wilaya ya Ludewa, wakiwa na wawezeshaji wa TCCIA na wanahabari.
Picha ya pamoja ya wafanyabiashara wa UWEMBA Wilayani Njombe wakiwa na wawezeshaji wa TCCIA na wanahabari.
Picha ya pamoja ya wafanyabiashara wa BULONGWA wilaya ya Makete, wakiwa na wawezeshaji wa TCCIA na wanahabari.
Baadhi ya wafanyabiashara wakifuatilia somo la madhara ya kutotumia vipimo vya mizani katika uununuzi na uuzaji wa mazao.
CHAMA cha wenye viwanda na wafanyabiashara Tanzania mkoa wa Iringa TCCI , kimewataka wafanyabiashara wote wa mazao kuacha mara moja mazoea ya kutumia vipimo visivyo vya kitaalamu katika ununuzi wa mazao kwa wakulima, kwa kuwa hatua hiyo ni uvunjaji wa sheria ya mizani ya mwaka 1982., na badala yake watumia vipimo vya mizani.
Hatua hiyo imekuja hivi karibuni baada ya TCCIA mkoa wa Iringa kuwakutanisha wafanyabiashara na wanunuzi wa mazao ili kuwapa elimu itokanayo na madhara ya kununua na kuuza mazao kwa kutumia vipimo visivyo rasmi kama NDOO, PLASTIKI na MADEBE jambo ambalo linchangia kudumaza uchumi wa wakulim na Taifa kwa ujumla.
Mafunzo hayo ambayo yamewafikia wafanyabiashara wa wilaya ya Ludewa, Makete na Njombe ymeonyesha dhahili namna wananchi wasivyo na ufhamu juu ya vipimo vya mizani, ambapo lawama kubwa zilielekezwa katika idara ya vipimo, kwa kushindwa kufika vijijini kukagua mizani hata inayotumika katika maduni na hivyo wananchi kupoteza imani na mizani hiyo.
Tanzania chamber of Commerce (TCCIA)
mkoa wa Iringa kupitia uongozi wake umewataka wafanyabiashara kuacha kuwaonea wakulima kwa kununua mazao yao kwa njia ya ujazo na hatimaye sasa watumie vipimo vya mizani.
Wananchi hao walisema hawana mazoea
ya kutumia vipimo vya mizani kutokana na kutopatikana kwa vipimo hivyo, ikiwa
pamoja na kupoteza imani kwa baadhi ya mizani ya wafanyabiashara, kutokana na
wakaguzi kutofika katika Wilaya zao kufanya ukaguzi na hivyo kujikuta
wakipunjwa katika manunuzi ya bidhaa yanyotumia mizani.
Fikiria Nyambo mkulima wa Matamba Wilyani
Makete alisema wamekuwa na mazoea ya kununua na kuuza mazao ya chakula kwa
kutumia bede au plastiki jambo ambalo halina utaalamu.
“Unakuta hta katika soko la
Chimala, tukifika na mazao pale wanatutaka tuanze kupima upya kwa mujibu wa
mnunuzi, wengine wanataka gunia liwe na ujazo wa debe 8, wengine 9 hadi 10,
sasa tukisema sisi tusiweke Lumbesa tunajisumbua, kwani huko tunakokwenda kuuza
wanakataa,” Alisema
Greyson Buha alisema endapo
serikali itahimiza kila mununuzi kuwa na mzani tatizo hilo litakwisha na
kuwainua wakulima katika kilimo chao ambacho wamekuwa wakitumia gharamaa kubwa
na kujikuta wakipata hasara wakati wa mauzo.
Witness Mwinuka alisema wamekuwa
wakipata hasara pindi wafikapo na mazao katika masoko makubwa, kwani
wafanyabiashara huwalazimisha kujaza upya katika magunia, na hivyo gunia moja
kujaza debe zaidi ya 9 hadi kumi.
Juditha Mpoma mnunuzi wa mazao wa
kijiji cha Bulongwa Wilayani makete alisema tatizo kubwa ni kukosekana kwa
elimu juu ya matumizi ya mizani ni moja ya sababu kubwa ya matumizi ya madebe
na ndoo katika upimaji wa mazao.
Naye Charles Mwasanga, mwenyekiti
wa wafanyabiashara Wilaya ya Ludewa alisema tatizo kubwa linalowakabili
wakulima wilayani humo ni ubovu wa miundombinu ya barabara, ambapo huwafanya
wakulima wauze mazao yao kwa gharama ndogo pindi wanunuzi wanapofika Wilayani
humo.
Wananchi hao walisema hujikuta
wakilazimishwa kujaza mazao katika mifuko (Maroba) yenye kilo 200 kwa malipo ya
ujazo wa kilo 100 hatua ambayo inarudisha nyumba uchumi wao.
“Gunia moja linalotakiwa kuwa na
kilo 100, tunaliuza kwa ujazo wa kg 150 hadi 200, kilo 100 nzima tunadhurumiwa,
sasa unadhani kama mfanyabiashara anahitaji gunia 100 amedhurumu kiasi gani, ni
zaidi ya gunia 100 anajipatia bure, sasa kwa Wilaya nzima kuna hasara kiasi
gani tunaipata,”? Alisema Mwasanga.
Mshauri mwezeshaji wa TCCIA mkoa wa
Iringa Dustun Mpangala alisema endapo serikali haitaingilia kati katika
kudhibiti ujazo huo wa lumbesa, kilimo kitashindwa kuwa mkombozi wa mkulima,
kwani hatua hiyo inadumaza nguvu kazi ya
mkulima, na kuwa ni ukiukwaji wa sheria ya vipimo ya mwaka 1982.
“Ndugu zangu, kutumia vipimo vya
madebe na ndoo ni ukiukwaji wa sheria ya vipimo ya mwaka 1982, na hakuna kitu
kizuri kama kufuata sheria, kwani adhabu ya uvunjaji wa sheria, adhabu yake ni
kubwa, fuateni sheria jamani,” Alisema Mpangala.
Hata hivyo makamu mwenyekiti wa
TCCIA mkoa wa Iringa, Henry Mangenya alizishauri Halmashauri zote kuweka vipimo
vya mizani katika masoko, ili kuwawezesha wakulima kutumia vipimo sahihi katika
uuzaji wa mazao yao, na kuachana na mazoea ya kutumia ujazo wa vifaa visivyo
rasmi, lengo likiwa ni kuwaepusha
wakulima kupata hasara inayochangia hata uchumi wa Taifa kudumaa.
MWISHO
No comments:
Post a Comment