Wednesday, October 10, 2012

MTUHUMIWA ASHINDWA KUFIKISHWA MAHAKAMANI


Marehemu Daud Mwangosi akivishwa Skafu na mmiliki wa mtandao huu, Bi. Oliver Motto, ambaye ni mwanahabari aliyekuwepo katika tukio hilo la kuuawa Daud Mwangosi, Marehemu alivishwa skafu hiyo Siku ya maandamano ya UHURU WA VYOMBO VYA HABARI. 



Marehemu Mwangosi, nayeonekana mguu wenye suruali ya Kaki, akiwa ameelekezewa mtutu ambao alifyatuliwa sekunde chache na kupoteza maisha yake, ktika kijiji cha Nyololo mkoani Iringa. 

Marehemu Mwangosi, Kulia aliyenyanyua Kamera, akiwa katika kituo cha Kwanza cha ufunguzi wa Matawi ya CHADEMA dakika chache kabla ya kumfika umauti katika ofisi ya CHADEMA Nyololo, baada ya kutoka katika  tawi hili la Kwanza lililofunguliwa.

Marehemu Mwangosi wa pili kulia, ambaye alikuwa mwenyekiti wa clab ya wanahabari mkoa wa Iringa (IPC) akiwa na wanahabari wenzie katika  ziara ya kikazi katika Hifadhi ya Ruaha mkoani Iringa, mwenye Tshirt ya Orange ni katibu wa clab ya wanahabari mkoa wa Iringa (IPC) Bw. Frenk Leonard, akieleza jambo.


Marehemu Mwangosi akiwa ameshika bango siku ya UHURU WA VYOMBO VYA HABARI, akiwa na diwani wa  Miyomboni/Kitanzini, Mh. Jesca Msambatavangu, katika mndamano ya siku hiyo.



WAKATI kamati ya Waziri wa mambo ya Ndani Mh, Emanuel Nchimbi, ikiwa imetoa ripot  yake juu ya mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa Chanel Ten, mkoa wa Iringa, Marehemu Daud Mwangosi, aliyeuawa Septemba 2 katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa, wakati akitimiza wajibu wa kazi yake ya uandishi,  nae mtuhumiwa wa kesi hiyo ameshindwa kufikishwa mahakamani.

 Mtuhumiwa huyo wa kesi ya mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha Luninga cha Channel Ten, Marehemu Daud Mwangosi, amelifanya shauri la kesi hiyo kukwama  kuendeshwa baada ya kushindwa kufika mahakamani hapo. Akisoma maelezo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, mh. Dyness Lyimo, Mwendesha mashataka wa serikali mkoa wa Iringa, Mh. Michael Luwena ameiambia mahakama kuwa  mtuhumiwa huyo hajafikishwa mahakamani hapo kutokana na taarifa ya ugonjwa. Mh. Luena amesema mtuhumiwa Pasificus Cleophace Simon (23) mwenye namba G 25 73,anayekabiliwa na tuhuma ya  kumuua kwa makusudi mwandishi wa habari Daud Mwangosi, Septemba 2 ameshindwa kufika mahakamani hapo kutokana na kuugua. Mtuhumiwa huyo alitakiwa kufikishwa mahakamani hapo ikiwa ni mara ya tatu tangu tukio hilo la mauaji litokee, huku wanahabari wakikwama kupiga picha za mtuhumiwa kila anapofikishwa Mahakamani, kutokana na ulinzi mkali aliowekewa. Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka wa kesi hiyo, upelelezi haujakamilika na kuwa  shauri la kesi hiyo limeahirishwa hadi mwezi Oktoba 24 mwaka huu, litakapotajwa tena.


MWISHO
 


No comments:

Post a Comment