Monday, November 12, 2012

DON BOSCO IRINGA NA MAONESHO YA UFUNDI

 Mkurungeni wa VETA Nyanda za juu kusini Bi. Monica Mbelle (Aliyeshika Kitabu)akionyeshwa moja ya kazi zinazofanywa na wanachuo wa Don Bosco Kata ya Mkwawa manispaa ya Iringa.
 Bi. Minica Mbelle akielezwa nama wanavyodhibiti matairi ya gari yenye pancha

 Akionyesha moja ya kifa cha gari kinavyofanyiwa matengenezo




 Akifafanuliwa namna wanavyotambua nozel chafu na safu



 Mwanafunzi Florida Mgedzi akifafanua upimaji wa Nozel safi na chafu
 wanafunzi chuo cha Don Bosco wanaendelea na kazi za ufundi

 Padre Abel Njeru ambaye ni mkuu wa chuo cha ufundi Don Bosco akiangalia kwa umakini mmoja wa wanafunzi wake akitoa maelezo kwa ugeni wa maonesho ya VETA

 Ni kama wanasema  "Tunaendelea na kazi"


 Kochi ambalo juu yake lina kitanda likiwa limetengenezwa kwa umakini mkubwa kwa kutumia vyumba na wanafunzi wa DON BOSCO YOURTH CENTRE.
Mwanafunzi Fredy Msamba akiwa amekaa katka kochi na kitanda vilivyounganishwa kwa ustadi mkubwa na yeye mwenyewe kama ni moja ya matunda ya chuo hicho cha ufundi DON BOSCO.


CHUO cha Don Bosco youth Training Centre, kilichopo chini ya Kanisa Kathoriki shirika la Wasalesiani Mtakatifu Yohane Bosco mjini Iringa kimefanya maonesho mbalimbali ya shughuli zinazofanywa na wanafunzi wa chuo hicho.

Akisoma risala mbele ya mkurugenzi mkuu wa vyuo vya maendeleo ya ufundi stadi VETA nyanda za juu kusini Bi. Monica Mbelle, mkuu wa chuo cha Don Bosco Padre Abel Njeru amesema lengo la kushiriki maonesho hayo ni kuunga mkono jitihada za serikali kupitia mamlaka ya VETA ili kuboresha uwezo na viwango vya nguvu-kazi ya vijana kwa maendeleo ya nchi.

Padre Njeru amesema hatua hiyo inatoa nafasi kwa wanafunzi kujipima kwa vitendo kazi zao wanazofundishwa chuoni hapo ili kutoa fulsa ya kujitathimini.

Aidha Padre Njeru amesema mafanikio ya chuo hicho, ni kwamb awanafunzi wameweza kupata nafasi ya kutumia ujuzi wao mbalimbali ambao wamejifunza katika kazi ya Useremala, Uungaji wa vyuma, Ufundi magari, Ufundi Umeme wa nyumbani, Uashi, Uchapishaji na Ushonaji.

Amesema changamoto inayowakabili katika chuo ni pamoja na idadi ndogo ya walimu ili kukidhi mahitaji ya mitaala mipya iliyoongezwa, kama somo la ujasiliamali, Kiingereza, Private Maintenance, atawapa auwezo wanafunzi wa kutambua matatizo, namna ya kushughulikia usalama mahala pa kazi.

Pia amesema masomo mengine yaliyoongezwa ni Kompyuta (Computer Application), Ujuzi wa mawasiliano (Communication Skillls), Uwezo wa kujihami na mgonjwa ynayoepukika, km ukimwi (Life Skills) kwa lengo la kuilinda rasilimali watu ambayo ndiyo nguvu kazi ya Taifa yaani Vijana.

Hata hivyo mkurugenzi wa VETA nyanda za juu kusini Bi. Monica Mbelle amesema ongezeko la masomo litasaidia vijana kupambana ana soko la ajira, hasa kwa somo la Ujasiliamali.   

Chuo cha Don Bosco Iringa ni mkombozi wa vijana katika kupambana na soko la ajira kwani kimekuwa kikitoa elimu ya mafunzo ya ufundi stadi kwa vitendo ili kumuwezesha kijana kujiajiri yeye mwenyewe na hivyo kumuepusha na tatizo la ukosefu wa ajira ambalo linawakumba vijana wengi hapa nchini.

No comments:

Post a Comment