Padre Anjelo Bargio, paroko wa kanisa Kathoriki, parokia ya Isimani Iringa, ambaye amelazwa katika Hospitalia ya mkoa bada ya kuvamiwa na majambazi na kupigwa Risasi ya kifua, upande wa kushoto .
Hapa Paroko Anjelo akiwa mwenye furaha siku ya mahafali ya kidato cha nne katika sekondari ya Isimani.
IKIWA imepita siku moja tangu watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi
kuvamia kanisa Kathoriki mkoani Iringa jimbo la Kihesa na kuiba baadhi ya mali,
tena kanisa hilo hilo katika jimbo la Isimani mkoani Iringa, limevamiwa huku
mapadre wakiumizwa vibaya.
Tukio hilo ambalo limetokea usiku wa kuamkia jana (Leo)
ambapo majambazi waliingia katika kanisa hilo kwa kuvunja milango na kuwapiga risasi
na panga padre Anjelo Bargio na Helmani Myala na kuiba fedha zaidi ya shilingi
milioni 3.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema majambazi hao baada ya
kuingia ndani walimkamata makamu wa Paroko na kumpiga wakitaka waonyeshwe kwa
paroko huku wakidai wapatiwe fedha, na tukio hilo limetokea majira ya sa tano
na nusu usiku.
Akizungumzia hali ya wagonjwa hao, kaimu mganga mkuu wa
Hospitalia ya mkoa wa Iringa Dr. Haustin Gwanchele amesema wamepokea majeruhi
watatu, mmoja akiwa ni mlinzi wa kanisa kathoriki Kihesa Bw. Bathromeo Nzigilwa
ambaye alipigwa nondo kichwani na kupoteza fahamu nab ado mgonjwa huyo hajitambui.
Dr Gwanchele amesema
Nzigilwa ameumia maeneo ya kisogoni na hali yake siyo nzuri, huku siku ya leo(jana)
wakiwamepokea wagonjwa wawili , kutoka kanisa katholiki parokia ya Isimani
katika Wilaya ya Iringa.
Amesema amempokea padre Helmani Myala (36) ambaye amepigwa
nondo na padre Anjelo Bargio (60) muitaliano ambaye naye alipigwa risasi
kifuani upande wa kushoto na kutokea kulia, huku nyingine zikiwa bado mwilini
na wanafanya mpango wa kuzitoa.
Mashuhuda hao wamesema majambazi walikuwa 7, huku wawili wakiwa
na bunduki na waliobaki wakiwa na nondo na panga n kuwa wameiba zaidi ya
shilingi milioni 3.
Hata hivyo wananchi wameiomba serikali kufungua macho na masikio yake, katika kulitatua tatizo hilo ambalo linaweza kuleta madhara makubwa kama halitatafutiwa
ufumbuzi mapema, kwani wanahisi kuwa ni mpango ulioratibiwa ili kulihujumu kanisa Kathoriki.
Kauli hiyo inakuja baada
ya kanisa hilo katika mkoa wa Iringa, kuvamiwa mara tatu, huku awali kanisa
katholiki Nyololo katika Wilaya ya Mufindi likivamiwa huku Padre akijeruhiwa
vibaya, na majambazi wakiondoka na mali mbalimbali za kanisani hapo.
Huku katika Kanisa la
jimbo kuu la Kihesa mkoani Iringa, majambazi hayo yamemjeruhi vibaya mlinzi na kutoroka na fedha, huku wakifanya uharibifu
mkubwa ikiwa pamoja na kuvunja baadhi ya mali kama Misalaba na kumwaga
Sakrament.
No comments:
Post a Comment