Wanakikundi cha VICOBA LUMULI, tarafa ya Kiponzelo katika Wilaya ya Iringa, wakisherehekea uzinduzi wa kikundi chao cha akiba na mikopo, nje ya ofisi yao ya kijiji.
MC wa uzinduzi wa Kikundi cha VICOBA LUMULI Mwalimu Elizabeth Sikawa, akiandika dondoo za maelezo ya shughuli hiyo.
Mratibu wa VICOB Wilaya ya Kilolo, Bi. Christina Kawaganise (wa kwanza kulia) akisikiliza mkutano huo wa uzinduzi wa VICOBA LUMULI.
Bi. Rehema Mitimingi, (mwenye suti nyeusi) ambaye ni mratibu wa VICOBA wilaya ya Mufindi akisikiliza maelezo ya mchumi wa mkoa Bw. Adam Swai (hayupo pichani) baada ya kupatiwa taarifa ya utaperi uluiofanywa.
Mwenyekiti wa VICOB LUMULI Bi. Annah Mkute akisoma risala mbe;le ya mgeni rasmi Bw. Adamu Swai katika uzinduzi huo.
Wanachama wakisikiliza maelezo katika sherehe ya uzinduzi huo.
"Tunashukuru baba" Wakifurahia jambo kutoka kwa mchumi wa mkoa Bw. Adam Swai, baada ya kutoa tamko la kusakwa kwa udi na uvumba taperi huyo wa fedha za wanavicoba.
Bi. Anjelika Kihakwi katibu wa VICOBA TWIYENDAGE cha Kataa ya Ifunda, katika tarafa ya Kiponzelo Wilaya ya Iringa, naye alishiriki sherehe hizo za uzinduzi wa kikundi jirani cha VICOBA LUMULI.
(Kushoto) ni diwani wa Kata ya Lumuli Bw. Charles Lutego na ofisa mtendaji wa Kata ya Lumuli Bw. Benedict Kibiki (mwenye suti nyeusi) wakiwa katika uzinduzi wa VICOBA LUMULI.
Mzee maarufu wa Kata ya Lumuli Bw. Rashid Chonya akiwa na ofisa mtendaji wa Kta ya Lumuli Bw. Benedict Kibiki.
Mratibu wa VICOBA mkoa wa Iringa Bi. Tisiana Kikoti (aliyekaa) akisubiri kupatiwa zawadi kutoka kwa wanakikundi wa VICOBA LUMULI, zawadi ambayo ilitolewa kwa lengo la kumpongeza kwa kazi nzuri ya uhamasishaji aliyoifanya na kuleta mafanikio kwa wanakikundi hao.
"Zawadi hii ni shukrani kwetu wanakikundi cha Lumuli" Ni maneno ya diwani Lutego, akikabidhi kikapu kwa mgeni rasmi Bw. Swai ambaye ni mchumi wa mkoa wa Iringa.
"Asanteni kwa zawadi hii ya Jogoo ambalo litanisadia kuniamsha asubuhi niwahi kazini" Ni maneno yake Bw. Adam Swai.
Diwani wa Kata ya Lumuli Bw. Lutego akimshukuru mgeni rasmi Bw. Swai kwa kazi aliyoifanya katika sherehe za uzinduzi.
BENKI ya wananchi waishio Vijijini, Village Community Bank
(VICOBA) ya mkoani Iringa, imetaperiwa zaidi ya shilingi Milioni 30 na mwanamke
aliyejitambulisha kuwa ni mratibu wa Vicoba ambapo aliwachangisha
wananchi fedha kwa madai ya kuwapatia mikopo.
Akitoa tarifa hizo mbele ya mchumi wa Mkoa Adam Swai, katika
uzinduzi wa Vicoba Lumuli katika Wilaya ya Iringa, mratibu wa Vicoba mkoa wa
Iringa Tisiana Kikoti alisema fedha hizo zilikusanywa na mwanamke (Rehema
Mbwanji) aliyejitambulisha kuwa yeye ni mratibu wa Vicoba, ambapo alikusanya
zaidi ya shilingi Miliobi 30 katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.
Tisiana alisema “Tumepata hasara kubwa kwani mtu huyo
amechukua fedha kwa kutumia cheo changu cha uratibu, na taarifa za awali
nilizipata kutoka katika kijiji cha Kitumbuka, Kata ya Ilole ambako alichukua
zaidi ya shilingi Milioni 12 na point,” Alisema.
Tisiana alisema katika Kata ya Ibumu Wilaya hiyo ya Kilolo mtu
huyo pia alikusanya fedha kwa vikundi mbalimbali, kwa kutumia udanganyifu huo
huo na wananchi baada ya kutoa fedha hizo ambazo alidai atawapatia mikopo
alitokomea na kuingia katika maeneo mengine.
Alisema baadhi ya wananchi bado wamekuwa wakifika katika ofisi
yake ya Vicoba mkoa wakilalamikia utapeli huo, na kuwa mtu anayefanya
matukio hayo si muhusika wa ofisi yake, huku akiwaasa wananchi kuacha kutoa
fedha kwa watu kwani hao ni waraghai.
Aliwataka wananchi kutotoa fedha kwa watu wasio na vielelezo na
uhakika kutoka katika ofisi wanazodai kufanyia kazi, kwa kuraghaiwa kupatiwa
mikopo, kwani banki ya Vicoba haichukui fedha bali inatoa elimu tu kwa
wanachama.
“Wananchi niwambie kuwa wawe makini na mataperi hao, kwani sisi
Vicoba hatuchukui hela ya mtu yoyote, tunachofanya ni kutoa elimu tu ya
kuendesha vikundi vyao vya akiba na mikopo, na waratibu wangu wote wa wilaya
huwa wanabarua zinazowatambulisha,” Alisema Tisiana.
Aidha alisema kutokana na tatizo hilo wananchi wamepoteza imani
juu ya vicoba na kuiomba serikali iingilie kati juu ya udanganyifu huo ikiwa
pamoja na kumkamata mwanamke huyo anazunguka amaeneo mbalimbali
kunachangisha fedha na hivyo kurudisha nyuma maendeleo yao.
Mratibu wa Vicoba Wilaya ya Kilolo Christina Kawaganise alisema
mwanamke huyo alianza kwa kuhamasisha uundwaji wa vikundi na kufanikiwa kupata
wanachama wengi na badaye kuwaambia wanavikundi wampe hela ambazo zitakuwa ni
dhamana ya kuchukua fedha benki ili awapatie mikopo.
“Wengine walitoa laki tano, laki sita hadi laki 8, na katika
kikundi cha MUWAKI alichukua laki moja na nusu, ninawataka wananchi wawe makini
na viongozi waanzirishi wa vikundi, wengine wanalengo la kujinufaisha wenyewe
na sio kuleta maendeleo kwa wananchi, Alisema Christina.
Hata hivyo mchumi wa mkoa wa Iringa Adam Swai alisema ameuagiza
uongozi wa Wilaya ya Kilolo kufuatilia suala hilo, na kuna haja ya kuingilia
kati ofisi ya mkoa ili kuwachukulia hatua matapeli hao kwa lengo la kumfikisha
mtu huyo katika vyombo vya dola, ikiwa pamoja na kurudisha fedha za
wananchi hao.
“Uongozi wa wilaya uwafahamu hao watu, ikishindikana mkoa
utaingilia kati ili tuwachukulie hatua, lakini maofisa ushirika, maofisa
maendelkeo ya jamii na mkurugenzi washirikiane kumbaini mwanamke huyo taperi,”
Alisema Swai.
MWISHO
No comments:
Post a Comment