Gari la Polisi likiwasiri katika Chumba cha kuhifadhia maiti mkoani Iringa, likiwa limebeba miili ya watu waliokufa katika ajari ya busi la Msanya, ambalo hufanya safari zake za Iringa kuelekea Usokami.
Wananchi wa manispaa ya Iringa, wakipita kutambua miili ya marehemu waliokufa katika ajali iliyotokea katika kijiji cha Ihemi/ Kichakani mkoani Iringa
Mmoja wa maiti akiingizwa katika chumba cha kuhifadhia maiti mkoani Iringa, baada ndugu zake kumtambua.
Mmoja wa ndugu za marehemu akiwa amemtambua ndugu yake.
IKIWA imepita wiki moja
tangu ajali mbaya ipoteza maisha ya watu 6 wa familia moja katika kijiji cha
Tanangozi, ajali nyingine imeua watu zaidi ya 10 katika kijiji cha Kichakani
katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
Tukio hilo limetokea
majira ya saa saba katika eneo la Ihemi kichakani, na kupoteza uhai wa watu 9
papo hapo huku majeruhi mmoja akifia Hospitalini.
Gari hilo aina ya Nisan
lenye usajili namba T. 803 AJV mali ya kampuni ya Msanya lililokuwa
likiendeshwa na dereva ambaye bado hajafahamika jina lake na amelazwa katika
word namba 7.
Gari hilo limekuwa
likifanya safari zake za Iringa kuelekea vijiji vya Mgama na Usokami, ambapo
lilikuwa likitokea Iringa mjini kwenda Usokami.
Akizungumzia tukio
hilo, kaimu mganga mfawidhi dr. Faustine Gwanchele alisema amepokea majeruhi 61,
waliotibiwa na kuondoka ni 33 na waliolazwa ni 28.kati yao wanaume 11 na wanawake 17.
Hata hivyo maiti watatu
bado hawajatambuliwa, huku maiti saba zikitambuliwa na ndugu zao na kuhifadhiwa
katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya mkoa wa Iringa.
Kwa mujibu wa mashuhuda
ajali hiyo ilitokea katika gati la mwisho katika barabara ambayo inaendelea
kutengenezwa ambapo dereva alisimama katika gati hilo lilipinduka na kuingia
kwenye korongoni.
No comments:
Post a Comment