Naibu waziri wa nishati na madini Mh. George Simbachawene (aliyesimama) akizungumza na baadhi ya viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, (wa kwanza kulia) ni mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bi. Pudensiana Kisaka, akiwa na mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw. Steven Mhapa.
Naibu waziri wa nishati na madini Simbachawene akizungumza na kaimu meneja wa Tanesco Iringa.
Naibu waziri (wa kwanza kulia) akitembelea kiwanda cha uzarishaji wa nguzo, cha Green Resources ya mjini Mafinga katika Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Mh. Simbachawene akionyeshwa shehena ya nguzo zilizokosa soko na meneja wa Green Resources Bw. Sangito Sumari (nguzo hazipo pichani).
Mh. Simbachawene akiwa ameketi na mkuu wa wilaya ya Mufindi, Bi. Evarister Kalalu, akisikiliza malalamiko ya wazarishaji wa nguzo wilayani humo.
mkurugenzi wa kiwanda cha SHEDA, Bw. Awadhi Shedaffa akitoa taarifa kwa naibu waziri Simbachawene juu ugumu wa upatikanaji wa soko wa nguzo, na nyingine zikikosa soko wakati Tanesco inaagiza bidhaa hiyo nje ya nchi.
meneja wa Green Resources Bw. Sangito Sumari
Bw. John Mwaula meneja wa kitengo cha nguzo katika kiwanda cha Green Resources,(Katikati) akifafanua jambo kwa Mh. Simbachawene.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bi. Pudensiana Kisaka, na mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw. Steven Mhapa, wakimsikiliza kwa makini naibu waziri wa nishati na madini, mh. George Simbachawene, (hayupo pichani).
NAIBU
waziri wa nishati na madini George Simbachawene amelitaka shirika la umeme
Tanzani kuacha kuagiza nguzo za umeme kutoka nje ya nchi na badala yake itumike
bidha ya hapa nchini.
Hatu
hiyo imekuja baada ya Mh. Simbachawene kutembelea baadhi ya kampuni
zinazojihusisha na uuzaji wa nguzo na mbao katika Wilaya ya Mufindi mkoani
Iringa, na kushuhudia hali halisi ya nguzo zikikosa soko.
Aidha Mh. Simbachawene amesema wakati sasa
umefika kwa Tanesco wa kutumia bidhaa hiyo iliyopo nchini ili kuleta tija kwa
viwanda vya hapa nchini, na kupunguza mzigo wa manunuzi ya gharama kubwa kwa
wananchi wanaohitaji nishati hiyo nyumbani mwao.
Amesema
hawezi kuruhusu nguzo ziendelee kuletwa nchini, kwani hali hiyo inachangia kuua
viwanda vidogo, inaua uchumi na ajira, na inaleta madhara makubwa kwa Taifa, na
kuwa hali hiyo isingekuwepo, kwa sababu jambo hilo la upatikanaji wa nguzo
limekuwa halisemwi vizuri.
Muuzaji
wa nguzo katika mji wa Mafinga Awadhi Shedaffa amesema hatua ya Tanesco kuagiza
nguzo nje ya nchi inawanyima fulsa wazawa kuuza bidhaa zao, kwani kampuni yake
inao uwezo wa kuzalisha nguzo elfu 12 kwa mwaka, na amekuwa akiuza nguzo 700
pekee kwa mwaka jambo linalodumaza uchumi wake nawa taifa.
Naye
Sangito Sumari meneja wa Kiwanda cha Green Resources cha Mufindi Mafinga mjini
Iringa alisema kampuni hiyo inayo uwezo wa kuihudumia Tanesco kwa nguzo, kwani
bidhaa hiyo inapatikana kwa kiwango kikubwa na kushindwa hata soko la kupeleka
licha ya kuwa shirika hilo linanunua bidhaa hiyo nje ya nchi.
John
Mwaula meneja wa kitengo cha nguzo Green Resources alisema kiwango hicho cha
nguzo kinazalishwa na mtambo mmoja, na endapo Tanesco wangetumia nguzo zao
wangeweza kutumia mitambo miwili na kupata nguzo idadi kubwa zaidi.
MWISHO
No comments:
Post a Comment