Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake (UWT) mkoa wa Iringa Bi. Zainabu Mwamwindi (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa umoja wa Vijana mkoa wa Iringa (UVCCM) Bi. Tumaini Msowoya (mwenye sweta la njano) pamoja na Bi. Natalia Magohagasenga ambaye ni mwenyekiti CCM Kata ya Mlandege mjini Iringa- wakiwa katika sherehe ya kumpongeza Mwenyekiti wa UWT. Bi. Mwamwindi.
Bi. Zainabu Mwamwindi-Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Iringa akitoa nasaha kwa wanachama wa CCM Iringa pamoja na wanachama wa umoja huo, katika sherehe ya kupongezwa kwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti tena wa jumuiya hiyo, sherehe zilizofanyika katika ukumbi wa chuo cha mafunzo na maendeleo ya ufundi Stadi (VETA) mkoani Iringa.
Bi. Tumaini Msowoya- Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Iringa, akisikiliza jambo kwa umakini mkubwa.
Baadhi ya Wanachama wa jumuiya ya umoja wa wanawake mkoa wa Iringa wakiwa katika sherehe hizo.
Baadhi ya wanachama wakisikiliza jambo, kutoka kwa mwenyekiti wao Bi. Zainabu Mwamwindi.
Bi. Natalia Magohagasenga (w kwanza kuli) akiwa na mwenyekiti wake wa jumuiya ya umoja wa wanawake CCM mkoa wa Iringa Bi. Zainabu Mwamwindi.
Bi. Ndendya mkazi wa Kata ya Kitwiru, akijumuika na wajumbe wenzie katika sherehe hizo za kumpongeza mwenyekiti wao wa UWT mkoa wa Iringa.
ILI kufanikisha mipango
mbalimbali ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) wanawake wametakiwa kuacha mara moja majungu na tabia
ya manemo yanayojenga chuki miongoni mwa wanachama na wananchi kwa ujumla.
Hayo yamezungumzwa na mwenyekiti
wa Umoja wa wanawake UWT mkoa wa Iringa Bi. Zainabu Mwamwindi, wakati wa
sherehe za kumpongeza zilizoandaliwa na wanawake wa umoja huo Manispaa ya
Iringa, na kufanyika katika ukumbi wa VETA.
Bi. Mwamwindi amesema ili
kulikomboa jimbo la Iringa mikononi mwa wapinzani, wanawake ambao ni nguzo kubwa ya chama wanatakiwa
kuwa wamoja na watu wenye upendo na mshikamano.
Aidha amesema kuachana na tabia
hizo zisizo na mafanikio kutasaidia kulipa deni la kulikomboa jimbo hilo kutoka
mikononi mwa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) likiongozwa na mbunge Peter Msigwa.
Amesema ili kufanikisha lengo
hilo atahakikisha anafika katika maeneo mbalimbali ili kuleta umoja kwa
wanawake mkoani Iringa, huku akiwahimiza viongozi kufanya kazi kwa ushirikiano
na wanachama ambao ndiyo shina la chama.
“Ndugu zangu!! Uongozi ni shughuli ya
kujitolea, ambayo wakati ukifika nafasi hiyo huchukuliwa na mtu mwingine, kwa
kufuata taratibu, ni vizuri basi tukawa na utaratibu wa kuwaandaa viongozi wa
kushika nafasi zetu pindi tumalizapo muda wetu, na nidhahiri kuwa viongozi
wazuri ni wale wanaowatumikia wenzao kwa ushirikiano ili kutambuana, lakini pia tuwapende hata wale walio nje ya chama, ili tujue matatizo yao ya wao kushindwa kuungana na sisi wanawake wenzao, na tukipata kero zao tuzitatue kirafiki na kwa upendo mkubwa,” Alisema
Bi. Mwamwindi.
Naye mwenyekiti wa Umoja wa
vijana CCM mkoa wa Iringa Bi. Tumaini Msowoya amesema ili kuleta nguvu ya
pamoja kwa vijana umeandaliwa mpango wa kuliinua kundi hilo kiuchumi, ili
kuwaepusha na tabia ya kuhamahama vyama kwa kutafuta maisha.
No comments:
Post a Comment