Wednesday, December 26, 2012

MCHUNGAJI ATOA ONYO KWA WAZAZI


Bi. Frola Kabogo mkazi wa Mwangata, akimpa mtoto mchungaji Rhoden Mang'ulisa, baada ya kichanga hicho kuzaliwa tena upya Kiroho (Kubatizwa kwa maji) katika kanisa la Kilutheri la kiinjili usharika wa Mlandege mjini Iringa.

Mtoto mchanga Raitness Mhapa ambaye amebatizwa na kuzaliwa upya kiroho, "katika siku ya familia takatifu", siku moja baada ya kuzaliwa Yesu Kristu Masiya (Christimas).
Watoto Sarafina Mhapa (wa kushoto) na Christina Mhapa (Mwenye blauzi ya zambarau) , wa familia ya Bw. J. Mhapa wa Mwangata mjini Iringa, wakipongezana baada ya kubatizwa katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri usarika wa  Mlandege mjini Iringa.
 Wanafamilia wakiwa nje ya kanisa, baada ya watoto wao kupata sakramenti ya Ubatizo.
 Mtoto Doreen Mhapa, akipokea Sakramenti ya Ubatizo, kutoka kwa mcungaji Petro Majere, kama ni ishara ya kuzaliwa upya kiroho, na kuwa muumini safi anayemjua na kumkiri Kristo.
 Mchungaji Petro Majere akitoa sakramenti ya Ubatizo.


 Muinjiristi Joel Mkemwa akitoa neno kwa waumini wa kanisa la Kilutheri Mlandege, katika misa ya Ubatizo wa watoto.


  
 Familia zikiwa katika picha ya pamoja ndani ya kanisa, baada ya kupokea sakramenti ya ubtizo.
 "Hongereni sana wanangu," Nimaneno ya Bi. Frola Kabogo akiwavisha taji watoto wake, baada ya kubatizwa. 
 "Waaooooooo!!," Tumezaliwa upya mdogo wangu, ni kama anasema Mtoto Doreen Mhapa, baada ya kupokea sakramenti ya ubatizo, katika kanisa la Kilutheri la kiinjiri la Mlandege, mjini Iringa. 
 "Niwakubwa kwa umri, lakini leo tumezaliwa upya pamoja, sisi ni watoto wa kristo, tunaamini na kumkiri Kristo kwa maneno na matendo yetu," Ni kama wanajisemeza ndani ya nafsi zao, baada ya kubatizwa.

WAZAZI kote nchini wametakiwa kuwalea watoto kwa kufuata  maadili mema ili miongoni mwa jamii hiyo wapatikane viongozi walio bora na wenye hofu na Mungu.

Wito huo umetolewa na Mchungaji wa kanisa la kiinjili la Kilutheri usharika wa Mlandege, mchungaji Rhoden Mang’ulisa wa mkoani Iringa, wakati akitoa sakramenti ya Ubatizo kwa watoto zaidi ya 50.


Aidha mchungaji Rhoden Mang’ulisa amewataka wazazi na walezi wa watoto hao kuacha kusisha vinywaji vyenye kileo katika sherehe za watoto.

Mchungaji Mang'ulisa amesema wazazi wakitoa malezi bora kwa watoto, jamii itakuwa na busara, na atimaye kuwapata viongozi walio bora, na wenye nguvu yaMungu katika kuongoza.

"Hivi mfano mama yake wa Rose Migiro, au rais wetu Kikwete angejua kuwa anayemnyonyesha ni rais au katibu wa nchi za Afrika ingekuwaje, wangetoa malezi ya hali ya juu, sasa kwa sababu hawakufahamu kitu chochote na nivigumu hilo kulielewa, sasa ninawaombeni wazazi wangu ninyi, toeni malezi bora nayenye kumpendeza Mwenyezi Mungu kwa hao watoto wenu, hamuwezi kujua kesho hao watakuwa ni akinanani??" alisema Mchungaji Mang'ulisa.


Kwa niaba ya waumini Bi. Frola Kabogo mmoja kati ya wazazi, wa  watoto waliobatizwa katika kanisa hilo, amesema   endapo wazazi watazingatia malezi bora na maadili mema kwa watoto wao, wataifanya jamii itoe zao bora la viongozi wa baadaye, ambao watakuwa msaada na tegemeo kwa Taifa.


MWISHO

No comments:

Post a Comment