Wakulima wakiendesha shughuli ya kilimo kwa kutumia zana duni za jembe la mkono, ambazo hazina tija kwao.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri mkuu - Sera na Uratibu wa Bunge, Mh. Willium Lukuvi, ambaye pia ni mbunge wa jimbo hilo la Isimani, akisaini kitabu cha wageni katika jijiji cha Izazi, kabla ya kupata taarifa za janga la njaa kutoka kwa wananchi.
Baadhi ya viongozi wa Kata ya Izazi na Migori katika Wilaya ya Iringa, Wakiwa katika kikao chao na Mbunge wao Mh. Willium Lukuvi, ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri mkuu - Sera na Uratibu wa Bunge.
WANANCHI
wa Tarafa ya Isimani katika Wilaya ya Iringa, wamekumbwa na baa la njaa, na
kusababisha baadhi yao kukimbia familia, .
Wakizungumzia
hali hiyo katika kikao chao na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri mkuu - Sera na Uratibu wa Bunge, Willium
Lukuvi, ambaye pia ni mbunge wa jimbo hilo la Isimani, Wananchi wa Kata ya Izazi walisema hali
ya njaa imewaathiri zaidi, kwani baadhi ya wazazi na walezi wamekimbia familia
zao.
Jasmini
Muhalu mkazi wa kijiji cha Mnadani, alisema licha ya uwepo wa tatizo hilo, pia
hata chakula kimekuwa hakipatikani kwa uraisi na hivyo kununu kwa gharama
kubwa, huku bdhi ya wanaume wakikimbia familia zao na asilimia kubwa ya wakazi
kijijini hapo kubaki wanawake na watoto.
“Yaani
kungekuwa na njaa halafu chakula madukani kinapatikana haingekuwa tatizo kubwa
sana, lakini sasa hata upatikanaji wa chakula umekuwa ni mgumu, mfano unga kilo
moja unauzwa shilingi elfu moja na miambili, na debe moja shilingi elfu kumi na
mbili, na hapa hakuna shughuli zozote za kiuchumi zaidi ya uvuvi ambao
umeseimama kutokana na Bwawa la Mtera kukauka maji,” Alisema Jasmin
Eudia
Masi mkazi kijiji cha Mnadani alisema hali ya njaa ni kubwa, kwani imesababisha
baadhi ya wanaume kuhama makazi yao wakifuata maji katika Bwawa la Mtera kwa
ajili ya kuendesha shughuli za uvuvi
ambazo nazo zimekuwa ni ngumu kutokana na kupungua kwa kiasi kikubwa katika
bwawa hilo.
Petro
Ng’ala alisema watu wamehama makazi yao ili kutafuta chakula katika maeneo
mengine, na hivyo familia zilizoachwa kuishi maisha magumu, huku wanafunzi
wakishindwa kuhudhuria masomo.
“Tumekuwa
na idadi kubwa ya wanawake wanaoishi bila wanaume, kutokana na waume zao
kukimbia kijijini hapa kwenda kutafuta ridhiki, lakini hali halisi ni mbaya
zaidi,” Alisema Ng’ala.
Costantino Makala mwenyekiti kijiji cha
Mnadani alisema debe moja la mahindi katika kijiji hicho linauzwa shilingi elfu
kumi n mbili, na hivyo familia nyingi kushindwa kumudu gharama hizo.
“Hali
halisi ya chakula katika kijiji change ni shida sana, ni muda mfrefu sasa, na
hili linatokana na mvua kushindwa kunyesha na hivyo kusababisha kukosa mavuno,
kwa siku wanapata mlo mmoja, na hivyo wengi wameshindwa kuvulimia hali hii na
kukimbia,” Alisema Makala.
Alisema
hali hiyo imesababisha hata shughuli za maendeleo kukwama, kutokana na nguvu
kazi ambayo ni wanaume walio wengi kuhama makazi katika kijiji hicho na kubaki
wanawake na watoto.
Makamu
mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Mnadani katika Kata ya Izazi Joyce Mgongolwa
alisema hali hiyo imeathiri pia mahudhurio ya wanafunzi, kwani wengi hawafiki
shuleni kutokana na asilimia kubwa ya wazazi kuwafanya ni wakuu wa kaya, kwa
kuwaachia nyumba.
“Mahudhulio kwa keli hasa kwa wale wasio na
mitihani ilikuwa ni hali mbaya, wanafunzi hawafiki shule labda kwa yale
madarasa yenye mitihani, nao utawaonea huruma, hasa ukifika muda wa mchana,”
Alisema Mwalimu Mgongolwa.
Ofisa
kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Lucy Nyalu, alisema tathmini
imefanyika na kuonyesha uwepo wa tatizo hilo, na tayari wameomba chakula
cha msaada katika ofisi ya waziri mkuu kitengo cha maafa.
Nyalu
alisema tathimini ilionyesha upungufu wa chakula utakuwa mkubwa hasa mwezi wa
kumi na mbili, na tayari Halmashauri wameomba tani miatano ili kuwasaidia
wakulima hao chakula na hata kwa ajili ya kilimo.
Alisema
Halmashauri inahimiza kitengo cha maafa ili kuwawezesha chakula wananchi hao,
kwani asilimia kubwa ya wakazi hao hawana chakula na awali walikuwa wanategemea
Bwawa la Mtera ambalo limekauka, huku zao la Mtama walilohimiza kulima
limeshindwa kutoa mavuno kutokana na mvua kushindwa kunyesha kwa kiwango
kinachotakiwa.
Hata
hivyo Nyalu alisema tatizo la njaa limeongezeka zaidi baada ya mvua
zilizoambatana na upepo mkali kufanya uharibifu katika maeneo hayo, huku
vyakula vya wananchi hao vilivyohifadhiwa nyumbani mwao vikiharibiwa na mvua na
hivyo tatizo la njaa kubwa zaidi.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment