Daladala yenye usajili Namba T .717 AWK mali ya Bw. Ayub Said mkazi wa Manispaa ya Iringa, ikiteketea kwa moto maeneo ya Mshindo katika mji wa Iringa.
Wafanyakazi wa kikosi cha zimamoto wakiwajibika kuokoa gari hilo.
Daladala ikiteketea kwa moto
Eneo la tukio.
Gari la zimamoto likiwa limewasili katika eneo la tukio.
Bw. Ayob Said, akiangalia gari yake kwa huzuni
Mmiliki wa daladala Bw. Ayub Said akiangalia gari yake kwa masikitiko makubwa, baada ya kuikuta imeungua kwa moto.
WATU waliokuwa
wakisafiri katika bus dogo la abiria, wamenusurika kuteketea kwa moto, baada ya gari
walilokuwa wakisafiria, kuteketea kwa moto mjini Iringa.
Tukio hilo limetokea katika eneo la Mshindo Manispaa ya
Iringa, baada ya daladala inayofanya kazi ya
kusafirisha abiria kutoka mjini
Iringa kwenda Mkwawa na Kihesa kilolo maeneo ya pembezoni mwa Manispaa ya
Iringa kuwaka moto.
Daladala hiyo yenye
usajili Namba T .717 AWK mali ya Bw. Ayub Said mkazi wa Manispaa ya Iringa, imekutwa
na mkasa huo, huku mashuhuda kwa mara ya kwanza wakipongeza kikosi cha zimamoto, kwa kufika kwa wakati katika tukio, japo wamekuta tayari gari hilo likiwa limeteketea kwa moto.
Bw. Julius Mdope amesema zimamoto katika tukio ilo hawapaswi kulaumiwa kwani asilimia kubwa ya wananchi wakati wa tukio walikuwa awana hata namba za kikosi hicho, jambo lililowafanya kumtuma mtu mwenye pikipiki ili akatoe taarifa ya moto huo.
"Kuna muda tunatakiwa kuwapongeza kikosi cha zimamoto, leo hii wamewahi sana, kibaya zaidi wananchi hatuna namba za zimamoto, hapa tumejaribu kuhangaika kila mmoja hana, hata wale walionayo wanalalamikiwa kwa matumizi mabaya," Alisema Julius Mdope.
Naye Bw. Kasimu Nyalusi mfanyakazi wa kituo ca mafuta cha GAPCO mshindo amesema kikosi hicho kimefika katika tukio kwa wakati, huku wakiwa na maji jambo ambalo katika matukio mengine uwa wanakwama.
Naye mmiliki wa gari hiyo Bw. Ayub Said amesema anawashukuru wananchi kwa ushirikiano waliouonyesha katika kutaka kuliokoa gari lake, kwani ata yeye alipigiwa simu akiwa kazini kuwa gari yake inaungua na gari hiyo ilikuwa na dereva wake.
Hata hivyo kaimu mkuu wa kikosi cha zimamoto mkoani Iringa, Sajenti meja John Zacharia-alisema kuna changamoto zinazosababisha wao kuchelewa katika matukio mbalimbali
ya majanga ya moto, ikiwemo la madereva wawapo barabarani kutokubali kuachia njia ili gari la zimamoto lipite, ikiwa pamoja na uwepo wa kikwazo cha nyaya nyingi za Tanesco kuwa chini na hivyo gari hilo kushindwa kupita na kuwahi matukio, na hivyo kulazimika kutafuta njia mbadala ya kufika katika tukio.
MWISHO
No comments:
Post a Comment