Sunday, December 30, 2012

SERIKALI KUVUNJA MIKATABA NA WAKANDARASI FEKI


  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bi. Pudensiana Kisaka, akitoa taarifa ya mpango wa ujenzi na ukarabati wa miradi ya barabara katika Halmashauri yake, (wa tatu kushoto) ni  mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bw. Steven Mhapa, katika kikao hicho na wakandarasi walioshinda Zabuni za ujenzi wa miradi 9 itakayogharimu zaidi ya shilingi Bilioni 3.

 Mkurugenzi wa kampuni ya GNMS Bw. Geofrey Mungai akitia saini ya makubaliano ya ujenzi wa mradi wa barabara.
 Mkurugenzi wa kampuni ya HJ. General Enterprises, Bw. Herman Madafu akitia saini ya makubariano ya ujenzi wa mradi huo alioushindia zabuni.
 Bw. Herman Madafu na shahidi wake wakiwajibika.
 Bw. Madafu akiwa na shahidi wake, wakati wa makubariano baina yake na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa juu ya mradi wa ujenzi alioushindia zabuni.

 Bw. Herson Mbwilo mkurugenzi wa SANTONA General Enterprises akiweka saini mbele ya shahidi wake.
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bi. Pudensiana Kisaka, akiteta jambo na mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bw. Steven Mhapa, katika kikao cha kusaini mkataba wa miradi 9 ya ujenzi na ukarabati wa barabara, inayogharimu zaidi ya shilingi Bilioni 3. 
 Bw. Omary Nurdin na shahidi wake, wakiingia makubariano na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, juu ya ujenzi wa mradi alioushindia zabuni.

 Mdau wa habari, (Ofisa habari wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa) Bw. Evaristo Myovela mmoja wa washiriki wa hafla hiyo.
 Ofisa mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Bw. Abel Mgimwa akiwa na ofisa ardhi Bi. Senje katika hafla hiyo.
Bw. Geofrey Mungai akifanya mahojiano na wanahabari nje, baada ya kushinda zabuni kati ya miradi 9, katika Hamashauri ya Wilaya ya Iringa.


 SERIKALI imekusudia kuvunja mikataba ya miradi ya ujenzi wa barabara dhidi ya makampuni yatakayobainika kufanya kazi chini ya kiwango kwa kuwa hali hiyo inachangia kudhorotesha hali ya uchumi wa wananchi huku Taifa likipata hasara kwa kushindwa kufikia malengo yake.


Hayo yamezungumzwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa (Vijijini) Steven Mhapa wakati Halmashauri hiyo ikisaini mkataba na wakandarasi wa miradi 9 ya ujenzi wa barabara ambayo itagharimu zaidi ya shilingi Bilioni 3.

Mhapa alisema hatawavulimia wakandarasi na makampuni yatakayofanya kazi chini ya kiwango sahihi kinachotakiwa, kwani kufanya hivyo ni kuwapa hasara wananchi juu ya kodi zao.


Hatua ya ujenzi wa barabara za vijijini katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, itanza punde baada ya Halmashauri hiyo ya Wilaya ya Iringa kuingia mkataba na wakandarasi, na kupunguza kero kubwa kwa wananchi wa wilaya hiyo, ambao baadhi yao wamekuwa wakishindwa hata kuuza mazao yao, kutokana na miundombinu ya barabnara kuwa duni.


Akizungumzia mafanikio hayo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Pudensiana Kisaka alisema Halmashauri kwa kuzingatia tratibu za kisheria na kiserikali, inakusudia kuanza utekerezaji wa miradi hiyo 9 ya maendeleo katika kipindi cha nusu ya pili ya mwaka 2012/2013.

Kisaka alisema Halmashauri kupitia vikao vya bodi ya zabuni vilifanya uteuzi wa wakandarasi ambapo jumla ya shilingi Bilioni 3, 78 Milioni, 055, 075 zimetengwa ili kukamilisha miradi hiyo ya barabara.

Akitaja barabara zitakazopitiwa na mradi huo, Kisaka alisema ni barabara aya Kitayawa-Ng’enza- Lupembelwasenga, barabara ya Ndiwili-Magulilwa- Ng’enza,   Mlowa-Kimande, barabara aya Isele- Kinyika pamoja na barabara aya Kimande na Izazi Mnadani.

Matengenezo mengine ni Mgama-Ilandutwa, Mgama – Itwaga- Lupembelwasenga, ukarabati wa barabara aya Wenda- Mgama, huku matengenezo yakifanyika katika barabara za Ilambalasi- Ng’enza, Kalenga- Kiponzelo- Wasa, Iguluba- Makadupa-Nyakavangala.

Huku barabara ya Pawaga sekondari- Mboliboli pamoja na kuendeleza ujenzi wa mradi wa kilimo cha umwagiliaji katika kijiji cha Mlenge ambazo kwa ujumla zaidi ya shilingi bilioni 3 zitatumika katika miradi hiyo.

Kisaka alisema ujenzi wa miradi ya barabara hizo utainua hali ya uchumi wa wananchi wa maeneo husika,  kwani wataweza kusafirisha bidhaa zao kwa uraisi, kama mazao na  wengi wao wakipata huduma kwa wakati.

Naye mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa  Steven Mhapa, aliwataka wakandarasi hao kuwa waaminifu, kwa kufanya kazi kwa  kiwango kinachotakiwa, ili kujenga imani kwa jamii juu ya kazi zao.

Mhapa alisema Halmashauri yake itawachukulia hatua wakandarasi wote watakaokiuka makubaliano hayo, kwa kufanya kazi isiyoendana na thamani ya fedha halisi walizopewa, kwani kuharibu kazi ni moja ya kudumaza maendeleo ya wananchi na Halmashauri.

“Mradi huu niwa fedha nyingi, ninawatakeni mzingatie dhamana mliyopewa, mtu yoyote atayefanya kazi chini ya kiwango, Halmashauri yangu haitasita kumchukulia hatua za kisheria mkandarasi wa aina hiyo, hizi ni kodi za wananchi, nitataka itumike kwa ubora wa kazi na kadri inavyopaswa kama ilivyo kwenye mkataba, kuomba ni suala linguine, na utekerezaji ni jambo lingine, malizeni kwa wakati kazi zenu,”. Alisema.

Herman Mbwilo mkurugenzi wa kampuni ya Santona aliwataka wakandarasi wenzie kutumia vipimo halisi katika upimaji wa barabara ili kuendana na hali halisi ya vipimo, kwa kuwa makini katika kufuata mikataba iliyosainiwa pamoja na kufanya kazi kwa muda uliopangwa.

Hata hivyo Geofrey Mungai mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi ya GNMS mmoja kati ya wakandarasi waliopata kazi ya ujenzi wa barabara hizo, alisema watafanya kazi kwa uhakika na kiwango kinachokubalika, ili kupunguza adha wanayoipata wananchi kwa kutokuwa na barabara nzuri.

Aidha naye diwani wa Kata ya Mgama Denis Lupala, alisema Kata yake imekuwa na changamoto kubwa ya miundombinu ya barabara, na hivyo mradi huo umefanikisha kupata barabara 3 na kupunguza vifo vya akinamama wajawazitio, vitokanavyo na ubovu wa barabara, ambapo baadhi ya wajawazito hushindwa kufika katika vituo vya afya na kupata huduma ya uzazi kwa wakati.

MWISHO

No comments:

Post a Comment