Thursday, February 14, 2013

"EBONY FM" - YAIBADIRI SIKU YA WAPENDANAO – YAFANYA KUFURU

 Hivi ndivyo siku ya Wapendanao kwa wananchi wa mikoa ya Nyanda za juu kusini ilivyokuwa na muonekano wa tofauti. Kweli  "Ebony Fm Feel The Deference"  Mwanaume huyu akiwa  amevalia nguo zake nyekundu kama ishara ya siku ya Wapendanao, na mgongoni akiwa amembeba mtoto wake, katika kituo cha "Sisi ni kesho" Kilichopo Nyololo Wilayani Mufindi katika mkoa wa Iringa.

Mmiliki wa mtandao huu, na mwakirishi wa Star Tv na Rfa, Bi. Oliver Motto- akiwa katika Bango la kituo cha kulelea watoto yatima na wale waishio katika mazingira hatarishi, mara baada ya kufika Nyololo.
Akina baba na watoto wao!!, Hii ni tofauti sana na ilivyozoeleka katika siku za nyuma, ambapo majukumu kama haya yalionekana kuwa niya mwanamke (mama) pekee.-  Kweli kuna haja ya siku ya wapendanao ikasherekewa katika mtazamo wenye mlengo bora kwa jamii na familia zetu.

Muhudumu wa kituo cha "SISI NI KESHO" akiwa amewashika watoto anaowalea, ambao ni yatima.
Mzee David Butinini akiwagawia Biscuti na Pipi watoto wa kituo cha "Sisi ni Kesho" Kma ni moja ya kusherekea siku ya wapendanao duniani.
Baadhi tu ya misada iliyokabidhiwa katika kituo cha "Sisi ni Kesho", Michngo kutoka kwa wananchi walioguswa na watoto yatima na waishio katika mazingira hatarishi.
Bw. Reymond Fransis mratibu wa harambee ya kuwachangia watoto yatima na waishio katika mazingira hatarishi, akiwa na Bi. Maria Waitara, ofisa tawala Wilaya ya Mufindi, wakifuatilia jambo.

Mbunge wa jimbo la Mufindi Kusini- Mh. Mendrady Kigola (Mwenye suti) akiwa na Bw. Reymond Fransis.
Baadhi ya watoto yatima na waishio katika mazingira hatarishi na magumu, wa kituo cha "Sisi ni Kesho".
Bi. Grace Mwambulesi, akionyesha fedha taslimu shilingi Milioni 3.na laki moja ambazo zimechangwa na wananchi, kwa ajili ya kusaidia watoto wa kituo cha "Sisi ni Kesho" 

 Bi. Teddy Ankungwe (wa kwanza kulia) akiwa na Bw. Imma (IMO) wote wafanyakazi wa kituo cha radio Ebony fm, wakiwa katika hafla hiyo ya kukabidhi fedha na bidhaa mbalimbali katika kituo cha "Sisi ni Kesho".
  Bw. Raymond Francis mratibu wa zoezi hilo, na mtangazaji wa kituo cha Radio Ebony fm akitoa nasaha juu ya harambee na siku ya Wapendanao- VALENTINE DAY, katika hafla ya kukabidhi misaada kwa watoto yatima.
 Baadhi ya watoto yatima wa kituo cha "Sisi ni Kesho"
 Vyombo mbalimbali vya habari, vikinukuu maelezo ya Bw. Raymond, mratibu wa harambee ya "Valentine day 2013, upendo kwa watoto".
 Bi. Suzana Mfugale, mmoja wa wahudumu wa kituo cha "Sisi ni kesho" akisoma lisara ya kituo hicho.
 Bi. Judith Mzulikwao (Mtangazaji wa Ebony fm) akiwa na mtoto yatima wa kituo cha "Sisi ni Kesho".

 Bi. Hatya Omary (mama Sinyoritha- aliyempakata mtoto) akiwa Bi. Khadija Kulanga katika hafla hiyo.

 
 Bi. Aggy Andason (aliyejishika sikio) akiwa na Bi. Neema Msafiri (aliyeshika mtoto) katika hafla hiyo.
 "Mtoto wa mwenzio ni wako" Usemi huu unatimizwa na Bi. Neema Msafiri - aliyekipakata kitoto kichanga cha mwezi mmoja, mtoto anayelelewa na kituo cha "Sisi ni Kesho".


  
 Katibu tawala wa Wilay aya Mufindi, Bi. Maria waitara na mbunge wa jimbo la kusini Mh. Mendrady Kigola- wakishukuru baada ya kuonyeshwa bidhaa zilizochangwa na wananchi kupitia hamasa kutoka katika kituo cha Radio Ebony fm, ya mjini Iringa.
 Bw. Raymond Fransis- (aliyenyanyua Radio) ambaye ni Mratibu wa harambee, akionyesha Radio ambayo nayo ilikabidhiwa katika kituo hicho, kwa lengo la watoto na wahudumu wa kituo kusikiliza matangazo na burudani mbalimbali za kituo hicho cha Ebony fm.
 Baadhi ya misaada 
 Misaada mbalimbali iliyotolewa na wananchi.



 Magodoro zaidi ya 15 yaliyonunuliwa kwa fedha za michango ya wananchi, yakiingizwa katika moja ya chumba cha kituo vcha "Sisi ni kesho", ambayo yalikabidhiwa kwa kituo hicho.
 Wafanyakazi wa Radio Ebony fm wakipanga Magodoro hayo.

 Waandishi wa habari, Bw. Godfrey Mushi  wa gazeti la Nipashe (aliyeshik kitabu) na Bw. Clement Sanga wa Chanel Ten, wakiteta jambo nje ya kituo cha "Sisi ni kesho"
Staff wa Ebony fm, wakibadilishana mawazo, nje ya kituo cha "Sisi ni Kesho".

 Mmiliki wa mtandao huu, Bi. Oliver Motto wa Star Tv na RFA - akiwa na Godfrey Mushi wa Nipashe.
Mzee David Butinini (wa kwanza kushoto) akiwa na Mbunge wa Mufindi Kusini Mh. Mendrady Kigola pamoja na mratibu wa "Valentine Day 2013, Upendo kwa watoto" Bw. Raymond Fransis, wakifuatilia jambo.
 Dj- Kwasa, wa Ebony fm, akipata kumbukumbu ya picha ya Bi. Hatya Omary na mtoto yatima.
 Bi. Grory Pelle- akiwa na Bi. Grace Mwambulesi (aliyempakata mtoto)
 Tswaga nazo zilikuwepo, ni baada ya kumaliza shughuli za makabidhiano ya misaada mbalimbali ya watoto. 
 Dj Kwasa mtoto amekupendeza balaa.
Clement Sanga na Godfrey Mushi, 
 Akinamama wa kikundi cha "GRAD WOMAN GROUP" cha Mafinga wakitekereza majukumu yao katika hafla hiyo.
GRAD WOMEN GROUP- Ni kikundi cha akinamama 15, kinachojishughulisha na mapishi katika sherehe na hafla mbalimbali, ambacho kilijitolea kupika chakula bure na kukigawa katika shughuli hiyo.
 Mzee David Butinini akipata huduma ya chakula kutoka kwa kikundi cha "GRAD WOMAN GROUP".
 
Mbunge Kigola akihudumiwa chakula na "GRAD WOMAN GROUP".

WAKATI akili, Mioyo na fikra za wananchi walio wengi duniani kote zikielekezwa katika siku ya wapendanao almaarufu kama “VALENTINE DAY” kama ni siku ya kimahaba na kimapenzi,  mambo hayo yamekuwa tofauti kwa wakazi wa mikoa ya nyanda za juu kusini- Iringa, Mbeya..

Hatua hiyo imekuja baada ya radio Ebony fm iliyopo katika mkoa wa Iringa kubadili mfumo na utaratibu huo, na hivyo kuwahamasisha wananchi kuchangia ili kuwatembelea kundi la watu wenye mahitaji muhimu.

Akizungumzia mpango huo, mratibu wa zoezi  la hilo lenye kaulimbinu ya “VALENTINE DAY 2013, UPENDO KWA WATOTO” kupitia kampuni ya Ebony fm, Bw. Reymond Fransis Chali - amesema lengo la kuendesha harambee hiyo ni kuwakumbuka watu wenye mahitaji muhimu ambao wamesahaulika katika jamii, hasa katika siku hiyo ya wapendanao.

“Imezoeleka kama siku hii ya VALENTINE ni malumu kwa wapenzi, katika kununuliana kadi, Maua mekundu, na zawadi mbalimbali, fikra hizi kupitia kituo chetu cha Ebony nikaamua kubadili mawazo hayo na hivyo kuwaelekeza wananchi kuwakumbuka watoto yatima na wale wanaoishi katika maisha magumu na hatarishi,” Amesema Reymond.

Aidha Reymond amesema anawashukuru wananchi wote waliopokea kwa mikono miwili zoezi hilo na kwa kuitikia harambee hiyo ya uchangiaji wa fedha na mahitaji mbalimbali kwa watoto wa kituo cha “SISI NI KESHO” kilichopo kijiji cha Nyololo katika Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa.

Amesema jumla ya fedha zilizochangwa na wananchi kupitia M-PESA ni zaidi ya shilingi Milioni 9.5, huku baadhi ya wananchi wakijitolea kwa hali na mali vifa mbalimbali kama Magodoro zaidi ya 15, nguo, mashuka, Mablanketi, Viatu, Vinywaji baridi (Visivyo na kileo), Katoni za Sabuni, Sukari, Unga wa ugali na Ngano, madishi ya kufulia na kuogea na hata mabero ya nguo mbalimbali.

Ofisa tawala wa Wilya ya Mufindi Bi. Maria Waitara ameitaka jamii kuiga mfano huo, kwa kuyakumbuka makundi hayo, hasa hilo la watoto yatima ambao kwa kiwango kikubwa wamepoteza wazazi wao kwa tatizo la ugonjwa wa ukimwi.

“Kwa kweli Radio Ebony imetupa somo, kubadili sura ya siku ya VALENTINE kwa kuwakumbuka watoto hawa, tunatakiwa kuendeleza zoezi hili ambalo katika wilaya yetu limetusaidia, kwani watoto hawa ni wetu wote, kuna watu watu wanafanya maasi mengi katika siku kama hii, lakini hawa ndugu zetu wameamua kuleta misaada hii ambayo itawasaidia kwa muda mrefu watoto wetu,” Alisema Waitara.

Hata hivyo Bi. Suzana Mfugale mmoja wa wahudumu wa kituo hicho cha “SISI NI KESHO” akisoma lisara  katika hafla hiyo amesema changamoto inayokikabiri kituo hicho ni pamoja na jamii kutojihusisha katika kuhudumia watoto hao, na hivyo kuwepo kwa mapungufu mengi.



No comments:

Post a Comment