Wednesday, February 13, 2013

HAMAD RASHID - APONDA “KILIMO KWANZA” PASIPO ELIMU NA ZANA ZA KISASA




 Mh. Hamad Rashid mbunge wa jimbo la Wawi Zanzibara kikagua shamba la mradi mkubwa wa Kimataifa wa “Ethical Hubs Farm Ltd”  uliopo katika Kijiji cha Ikwavila Kata ya Kijombe, Wilaya ya Wanging’ombe katika mkoa mpya wa Njombe.
 Mh. Hamad Rashid akikagua shamba la mradi mkubwa wa Kimataifa wa “Ethical Hubs Farm Ltd”.
 Meneja wa mradi  wa “Ethical Hubs Farm Ltd”,  (Aliyeinama) Bw. Omary Costantino akimuelekeza jambo Mh. Hamad Rashid, baada ya kuzindua mradi huo.
 Mkurugenzi wa mradi wa “Ethical Hubs Farm Ltd”  Bw. Kaushik Amlani (Wa kwanza kushoto) raia wa India- akipokea shukrani kutoka kwa wananchi wa kijiji cha Ikwavila, katikati ni mbunge wa Wawi Mh. hamad Rashid akiwa na mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Ikwavila Bw. Godlove Nyunja.

 Mkurugenzi wa mradi wa “Ethical Hubs Farm Ltd”  Bw. Kaushik Amlani akiwa na mbunge wa Wawi Zanzibar Mh. Hamad Rashid.
MBUNGE wa Wawi (CUF), Bw. Hamad Rashid, akikabidhi msaada wa fedha taslimu shilingi laki tatu kwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ikwavila - Mwl/Justine Njenga.
 Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Ikwavila wakiwa katika mkutano huo wa uzinduzi wa mradi wa Ethical Hubs Farm Ltd.
 Wananchi wa kijiji cha Ikwavila wakifurahia jambo katika uzinduzi huo katika shamba la mradi wa Ethical Hubs Farm Ltd.

 "Tunasikiliza kwa makini sana!!
 Mkurugenzi wa mradi wa "Ethical Hubs Farm Ltd"  Tanzania  Bw. Sebu Panya akisikiliza maelezo kutoka kwa mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Ikwavila Bw. Godlove Nyunja (Hayupo pichani).
 Bw. Gerlady Mpanye (Mwananchi) akiwa katika shamba hilo.

MBUNGE wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Abdalah, ameitaka serikali kujikita kwanza kutoa elimu kwa wakulima juu ya kilimo bora cha kisasa, badala ya kukimbilia kuwapatia wananchi pembejeo ambazo hazina tija na manufaa kwa mustakabari mzima wa sekta hiyo.

Akitoa rai hiyo wakati wa uzunduzi wa mradi mkubwa wa Kimataifa wa “Ethical Hubs Farm Ltd”  uliopo katika Kijiji cha Ikwavila Kata ya Kijombe, Wilaya ya Wanging’ombe katika mkoa mpya wa Njombe, wakati akizungumza na wananchi wa kijiji hicho juu ya mradi huo wa kuendesha shughuli za kilimo cha Mihogo na Alizeti.

Aidha Hamad Rashid, amesema Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, inatakiwa pia kuufuta utaratibu wa ununuzi wa mazao ya wakulima kwa kutumia mfumo wa stakabadhi gharani na badala yake iruhusu utaratibu wa uwekezaji wa kimataifa wa kuingia ubia na wakulima kwa kuwekeza kwa asilimia 50 ili kuwawezesha wakulima nchini kunufaika na ardhi yao pasipo kuiuza.

“Sipendezwi na mfumo wa wawekezaji wanaoingia nchini na kununua ardhi, ardhi ni rasilimali ya watanzania, inatakiwa kukodishwa kama wanavyofanya hawa Ethical Hubs, unapoiuza ardhi mwananchi anapoteza haki yake ya umiliki katika ardhi yake, na hiyo ndiyo sababu za kuibuka kwa migogoro baina ya wananchi na hao wawekezaji, mpango huu wa Ethical Hubs siyo wa uwekezaji, bali niwa uwezeshaji kwani wananchi wanakuwa wananufaika kwa asilimia kubwa kupitia   ardhi inayotumika tena wakipata ajira,” Alisema Hamad Rashid.

Amesema shamba hilo litatumika katika uzalishaji wa mbegu bora za Mihogo na Alizeti baada ya kuingia ubia na wananchi kwa asilimia 50, huku mradi ukigharamaia mbolea, madawa mbalimbali ya kilimo, vibarua pamoja na   kuwafundisha wananchi hao juu ya elimu sahihi ya kilimo cha kisasa kupitia mashamba darasa.

Amesema mradi utarejesha asilimia 50 ya faida kwa wananchi baada ya mavuno, Alisema mbunge huyo, jambo litakalo wasaidia wakazi hao kujikwamua kiuchumi kupitia rasilimali yao ya ardhi.

Pia alisema  utaratibu wa sasa wa serikali kukopa mazao ya wananchi pasipo kutoa fedha tasilimu na kisha kuyahifadhi kwa mfumo wa stakabadhi gharani, hauwapi fursa wakulima kufurahia jasho lao baada ya kufanya kazi ngumu ya kupambana na shughulki hiyo, na hivyo kuendelea kudumaza sekta ya kilimo.

Akizungumzia hatua hiyo Hamd Rashid alisema Shirika la Kimataifa lisilo la Kiserikali la (EDF) linaloendesha utaratibu huo katika nchi za Afrika ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, limeamua kufika mikoa ya nyanda za juu kusini, kwa kuanza na mkoa wa Njombe kwa lengo la ja kutoa elimu hiyo kwa watanzania hasa waishio maeneo ya vijiji.

Naye Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo la EDF, Kaushik Amlani ambaye ni raia wa Uingereza mwenye asilia ya India, amesema wakulima wa Kijiji cha Ikwavila katika kipindi cha miaka miwili kuanzia sasa watapata hiyo ya kilimo cha kisasa, ikiwa pamoja na kujengewa  nyumba za kisasa kutokana na malipo yenye tija atakayowapatia.

Hivi sasa kila mwananchi anayefanya kazi katika mradi huu, kwa siku analipwa shilingi elfu 14, ikiwa pamoja na kumpatia chai asubuhi na chakula cha mchana  kama ujira baada ya kujifunza,na tutafanya hivi hadi kila mtu ajikomboe na umasikini, awe na makazi bora...katika eneo hili nimepata hekta 10,000, ambapo hekta elfu 9 kwa ajili ya mashamba darasa,”Alisema Kaushik.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho,Godlove Nyunja amesema ujio wa mwezeshaji huyo wa kimataifa umesaidia kuboresha maisha ya wananchi wake, kwani awali walikuwa na  maisha duni, baada ya kushindwa kuendesha shughuli za kilimo katika maeneo makubwa yaliyopo kwa kukosa  zana bora za kisasa kilimo na pembejeo.

Wananchi wamesema utaratibu wa mradi huo unapaswa kuigwa kote nchini, kwani mwezeshaji huo anakodi mashamba ambayo kijiji na wananchi wameshindwa kuyalima, na wao kunufaika na ajira endelevu ambazo zitasaidia kuinua hali ya uchumi ambayo ilitegemea kufanya vibarua katika mashamba madogo ya wananchi wenzao na kulipwa ujira mdogo.

"Tulikuwa na hali ngumu mno hapa, lakini siku chache hizi tunapata kila siku elfu 14, mabadiliko yameanza, tunataraji  kujenga nyumba  bora, kwani fedha hii ya siku tu, tunaweza kununua bati na kubadili nyasi katika majengo yetu haya unayoyaona," Alisema Bahati Mgombela. 

Mwezeshaji huyo kutoka nchini India pia anaendesha miradi ya aina hiyo katika nchi yaKongo, na ameanza kuingia ubia na wananchi kwa kukodi kila ekari moja kwa dola 50 za kimarekani kwa mwaka.

Hata hivyo Mh. Hmad rashid alikabidhi fedha shilingi laki tatu kwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ikwavila, Mwalimu Justine Njenga, kwa ajili ya kusaidia ukarabati wa vyumba vya madarasa katika shule ambayo ilianza tangu mwaka 1977.

MWISHO.

No comments:

Post a Comment