Mvuvi Lion Semfukwe akiwa kazini katika Bwawa la Mtera Iringa, miti hiyo awali ilifunikwa na maji ambayo yaliipa jina la "Mtera" sasa maji hayo yamekauka na kubaki mto pekee, huku eneo hubwa la Bwawa hilo likiwa kavu.
Meneja mkuu wa shirika la umeme TANESCO Mtera, Injinia Nazir Yazid Kachwamba akiwaeleza wadau wa mazingira kupitia bonde la Rufiji (hawapo pichani) namna maji yalivyoshuka kina katika Bwawa la Mtera.
Bwawa la Mtera ambapo maji yake yanaingia katika ufuaji wa umeme.
Mtera eneo la mapokeo ya maji ya kufulia nishati ya umeme.
Baadhi ya Wadau wa mazingira kupitia bonde la Rufiji wakiwa ndani ya mgodi wa Mtera, wakipata maelezo kwa injinia Nazir Yazid.
Bw. Onesmo zakaria Sigalla (Mwenye shati jeupe), kiongozi wa timu ya miradi ya maji WWF Tanzania, akisikiliza maelezo kutoka kwa staf wa Mgodi wa Tanesco Mtera.
SHIRIKA la Umeme Tanzania- TANESCO limepoteza mapato ya shilingi Bilioni 740 kutokana na maji katika Bwawa la Mtera kukauka, huku likiingia hasara ya zaidi ya shilingi Bilioni 403 kwa kutumia nishati ya mafuta ili kuendesha mitambo yake.
Hayo yalizungumzwa na meneja mkuu wa Tanesco Mtera, Injinia Nazir Kachwamba, wakati wadau wa mikoa na Wilaya zinazopitiwa na bonde la Rufiji walipotembelea mgodi huo wa uzalishaji wa nishati ya umeme, kwa lengo la kutambua changamoto zinazolikabiri Bwawa la Mtera, kutokana na vyanzo vya maji kuharibiwa, na hivyo mto mkuu ruaha kushindwa kutiririsha maji na kusababisha Bwawa hilo kukauka.
Nazir alisema kupungua kwa maji kwa kiwango kikubwa katika Bwawa hilo, kunasababisha grid hiyo kutumia nishati nyingine za kuendeshea mitambo, na hivyo kuingia gharama kubwa tofauti na kiwango halisi cha uzalishaji na hivyo kupata hasara.
“Vile vile kutokuwepo kwa Hydro ya kutosha kunaathiri uzarishaji wa grid, kwani mitambo ya maji inafua umeme kwa haraka bila kuathiri uzalishaji, tofauti na nishati nyingine za mafuta, huku upatikanaji wa maji kwa ajili ya matumizi ya kawaida hapa ukiwa chini,” Alisema Injinia Nazir.
Aidha alisema kutokuwepo kwa maji katika Bwawa hilo la Mtera kumesababisha uzalishaji wa umeme kutokuwa wa kutosha na hivyo kuyumbayumba juu ya uendeshaji wa mitambo, licha ya kuwa .
Alisema hali hiyo inatokana na wananchi kufanya uchepushaji wa maji mengi pasipo kuwa na vibali, kwa shughuli mbalimbali za kibinadamu kama kilimo na hivyo kusababisha hasara kubwa kwa mgodi huo.
Alisema kwa kawaida mitambo hiyo inaweza kuvumilia kutembea hadi mita 687.00 mita mbili kwenda chini na sasa wapo mita 688.84, kiwango cha juu cha matumizi, ambapo walilazimika kuomba kibari wizara ya maji ili kuendelea kutumia maji hayo na kupata ruhusa ya kutumia mita mbili na nusu nyingine kwenda chini.
Alisema kupungua kwa maji kwenye Bwawa athari zake ni nyingi ikiwemo la kutumia gharama kubwa za fedha, katika kusafisha maji hayo ambayo sasa ni machafu kutokana na kutumia maji yaliyochini ya kina sahii kinachotakiwa.
Pia alisema umeme nafuu ni ule unaozalishwa kwa gasi tofauti na umeme wa mafuta na maji, kwani unit moja kuzalisha umeme wa maji ni senti 3 za kimarekani sawa na shilingi 195, huku umeme wa gesi ukiwa na gharama ndogo mara tatu ya umeme huo wa maji.
Huku unit moja ya umeme wa mafuta ukizalishwa kwa gharama ya senti 41 za kimarekani, kiwango ambacho ni kikubwa mno cha fedha, na hivyo Kidatu na Mtera kutumia fedha nyingi licha ya kushindwa kuzima mitambo hiyo inayotumia maji, kunatokana na kutokuwa na vyanzo vingine mbadala vya kufua umeme.
Akifafanua sababu za kuyumba kwa uzalishaji wa umeme, injinia Nazir alisema ni kutofahamu kiwango sahihi cha maji kinachohitajika kwa uzalishaji kwa mwaka ili kutafuta njia mbadala ya kupata nishati hiyo.
Aidha Injinia Nazir amesema athari za kupungua kwa maji katika Bwawa hilo, zinasababisha matumizi makubwa ya fedha, na hivyo uendeshaji wa grid hiyo kuwa mgumu zaidi, kwa kuwa mitambo ya maji inazalisha umeme kwa haraka tofauti na nishati nyingine kama gasi na mafuta, inagharimu fedha nyingi, na hivyo tatizo hilo la maji katika Bwala la Mtera kuyumbisha uzalishaji wa umeme.
Hata hivyo injinia Nazir alisema kukauka kwa maji katika Bwawa la Mtera siyo sababu ya umeme kutozalishwa katika mgodi huo, au kuwepo kwa mgao wa umeme, kwani kuna vyanzo mbalimbali vya kufua umeme kama gesi.
“Mitambo iliyopo ikisimama kwa kukosa maji, itatengwa mingine mipya inayotumia vyanzo vingine, wananchi nawaomba waomnndokane na dhana ya kuwa maji yakikauka kutakuwa na umeme wa mgao, hapa,” Alisisitiza injinia Nazir.
Petro Mbwela na Manka Richard wakazi wa kijiji cha Mtera na Migoli wanaotegemea shughuli za kiuchumi kutoka katika Bwawa hilo, walisema Uvuvi katika Bwa hilo umekwama kutokana na kukauka kwa maji katika Bwawa hilo na hivyo hali yao ya uchumi kuyumba.
“Bwawa hili limetuathiri vibaya, hebu ona hapa tulikuwa tunapata Samaki wakubwa, tunauza na kuwasomesha watoto wetu, lakini leo hii kuna baadhi yetu wamekimbia familia zao kwa sababu ya kukauka kwa Bwa hili, “ walisema.
Nicholaus Kalinga mwenyekiti wa Upatikanaji Matumizi ya Usimamizi wa Rasilimali Maji endelevu (UMURAME) alisema kukauka kwa Bwawa la Mtera kunatokana na baadhi ya viongozi kuvihujumu vyanzo vya maji, kwa kupanda miti isiyo rafiki na maji.
"Tunaumizana vichwa hapa bure juu ya kuharibu vyanzo vya maji, nyinyi wenyewe viongozi mnakwenda huko vijijini nmapanda miti hadi kwenye vyanzo vya maji, wananchi wanashindwa kuelewa wafuate lipi, lakini hapa tunapiga kelele ya kilimo cha umwagiliaji kinachopoteza maji mengi, viongozi ndiyo wenye mashamba makubwa ya kilimo hicho, tunapozungumzia mashamba siyo ya wakulima wadogo, kuna mashamba makubwa yapo chini ya viongozi sasa mnadhani wananchi wanelewa nini, miaka 20 tunaweka mipango na mikakati ya kunusuru mto Ruaha mkuu uweze kuriririsha maji lakini hakuna mafanikio," Alisema kalinga.
Bwawa la Mtera kwa hali iliyonayo sasa, huwenda likapoteza jina na sifa yake, endapo wadau hao hawatafanya kazi ya ziada katika kuvinusuru vyanzo vya maji, vinavyotirirish a maji yake katika mto Ruaha Mkuu.
Bwawa la Mtera kwa hali iliyonayo sasa, huwenda likapoteza jina na sifa yake, endapo wadau hao hawatafanya kazi ya ziada katika kuvinusuru vyanzo vya maji, vinavyotirirish a maji yake katika mto Ruaha Mkuu.
MWISHO
No comments:
Post a Comment