Monday, April 1, 2013

MAGUFULI AOMBWA KUSAIDIA BARABARA MAKETE

WAZIRI wa Ujenzi, Dk John Pombe Magufuli.

  Gari zikiwa zimekwama katika barabara ya Makete, na hivyo kusababisha barabara kufungwa.



WAZIRI wa Ujenzi, Dk John Magufuli, ametakiwa kuzisaidia barabara za Makete mkoani Njombe ili kuepusha usumbufu na  gharama kubwa za usafiri kwa wananchi, kutokana na miundombinu hiyo kuwa duni, na hivyo magari mengi kushindwa kufika.


Hayo yamezungumzwa na wananchi na wamiliki wa magari yanayofanya safari zake katika Wilaya hiyo ya Makete, ambapo sasa ni zaidi ya siku nne, barabara ya Ivalalila kuharibika vibaya na hivyo magari kukwama na kufunga barabara hiyo.

 

Bw. Junich Daniel alimarufu Mwarabu, mmiliki wa mabasi ya Japanise amesema kwa hali iliyopo katika barabara hiyo inayoelekea Makete na Mbeya usafiri hautakuwepo kutokana na kuingia wao kutumia gharama kubwa katika kufanya marekebisho kwani licha ya tope pia barabara hiyo imekuwa na mashimo makubwa hali inayopelekea magari yao kuharibika.


Bw. Mwarabu amesema kuna haja kwa viongozi husika pamoja na waziri mwenye dhamana kusaidia ujenzi wa barabara za wilaya hiyo ya Makete kwani sasa hali ni tete hususani  katika msimu huu wa masika.

Aidha mkuu wa wilaya ya Makete Bi. Josephine Matiro amewataka wananchi  wa Makete  kushiriki katika  ukarabati wa miundombinu ya barabara pindi tatizo linapotokea hasa maeneo korofi.

Bi. Matiro amesema wananchi wanatakiwa kuwa na ushirikiano pindi barabara zinapokuwa zimeharibika ili kurahisisha usafiri, huku kifafanua kuwa tayari viongozi wa Tanrods mkoa wa Njombe wamepewa taarifa kuhusiana na tatizo hilo lililopo katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo hasa katika kijiji cha Ivalalila.

Mtandao huu umefika eneo la tukio nakujionea hali halisi  ya barabara ambapo mpaka sasa hakuna mawasiliano kutoka Makete kwenda jijini Mbeya kupitia barabara ya kijiji cha Ivalalila kutokana na mashimo yaliyopo katika eneo hilo.


Na Edwin Moshi - Makete


No comments:

Post a Comment