Wakiwa katika makaburini ya ukoo ya akina Msumule
Kushoto ni Juma Msumule akiwa na baba yake mzazi mzee Salum Msumule na kulia ni Richard Msumule wakibadilishana mawazo katika sherehe hiyo.
Mzee Salum Msumule baba wa famili na ukoo wa akina Msumule
Elia Msumule akiwa na mama yake mzazi.
Juma Msumule akiwa na baba yake mzazi.
Richard Msumule (Kulia) akiwa na baba yake mzazi mzee Msumule.
Ni km Kikapu, lakini hiki ni chombo maalumu cha kabila la Wahehe, nikwa ajili ya kunywea Pombe (komoni) kinafahamika kama KINYAMKONYI.
Wakisherekea kwa KIDUO, ngoma maalumu kwa kabila la WAHEHE.
Pombe aina ya Komoni ikipata mashambulizi kutoka kwa waalikwa wa sherehe hiyo.
wakiwa katika Picha ya pamoja baadhi ya wanafamilia wa ukoo wa Msumule.
Baraka Msumule (katikati) akiwa na babu zake.
Vinywaji vya asili navyo havikuachwa nyuma.
Wanakwaya wakisherehesha katika siku hiyo.
Elia Msumule (wa kwanza kulia0 akiwa na shemeji yake (katikati pamoja na dada yake (kushoto).
UKOO wa Msumule wenye makazi yao Mazombe katika Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, wamefanya kumbukumbu za kuwakumbuka ndugu zao wote waliofariki dunia.
Akizungumzia hatua hiyo kaka mkubwa wa familia ya Msumule Bw. Richard Msumule amesema mpoango huo ni katika kuwaunganisha familia na ukoo wote, kwa lengo la kufahamiana na kujadili masuala mbalimbali yahusuyo ya ukoo.
Aidha Msumule amesema mpango huo utawawezesha kujadili pia changamoto na matatizo yanayowakabiri katika ukoo huo na kwa umoja wa pamoja kuyatatua ili kumfanya muhusika kuendelea na shughuli nyingine za ujenzi wa Taifa baada ya kumalizika kwa tataizo lake.
Mzee salum Msumule ambaye ni baba na kiongozi wa ukoo huo amesema muungano huo utarahisisha utatuzi wa matatizo pindi mwanafamilia anapopata tatizo.
Mzee Msumule ni kati ya wazee maalufu mkoani Iringa ambapo katika tetesi imefahamika alikuwa na wake zaidi ya watano, watoto zaidi ya 35 na wajukuu zaidi ya 50 na hivyo kuufanya ukoo huo kuwa mkubwa, na umoja huo utawafanya wafahamine na kujaliana kama ndugu wamoja.
No comments:
Post a Comment