Mwenyekiti wa kamati ya bunge, ardhi, maliasili na mazingira Mh. Jemsy Lembeli (wa kwanza kulia) akiwa na mkuu wa Wilaya ya Mufindi Bi. Evarister Kalalu, na mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, Mh. Peter Tweve katika kikao baina ya kamati, viongozi wa Halmashauri na wadau wa msitu wa Taifa wa Saohill, kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi mkoni Iringa.
Bw. Juma Mgoo mtendaji mkuu wa wakala wa huduma za misitu Tanzania, akiwa katika kikao cha kamati ya bunge ardhi, maliasili na mazingira, katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, wakati wadau wa msitu wa Saohill wakitoa malalamiko yao juu ya kupandishwa kwa gharama za uvunaji, ushuru, huku qubicmita zikipunguzwa kutoka mita 500 hadi kufikia Qubic mita 250.Baadhi ya wadau wa Msitu wa Taifa wa Saohill uliopo Wilayani Mufindi, wakimsikiliza mwenyekiti wa kamati ya bunge, ardhi, maliasili na mazingira mh. Jemsy Lembeli (Hayupo pichani) wakati wakifikisha malalamiko yao juu ya utaratibu wa ugawaji wa maeneo ya uvunaji katika shamba hilo la Saohill.
Mwenyekiti wa wavunaji Bw. Christian Ahia akisisitiza jambo kwa kamati ya ardhi, maliasili na mazingira, iliyo chini ya mwenyekiti wake mh. Jemsy Lembeli Mbunge.
Mh. Jemsy Lembeli mwenyekiti wa kamati ya bunge ya ardhi, maliasili na mazingira, akiwa na mmoja wa mjumbe wa kamati hiyo katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, wakijadili suala la ugawaji wa vibari vya kuvuna miti katika Msitu wa Taifa wa Saohill.
"Mh. Mwenyekiti!! Kwa kweli utaratibu uliotumika mwaka huu siyo mzuri kabisa," Ni maneno ya mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mh. Peter Tweve akifafanua juu ya ubovu wa utaratibu mpya wa ugawaji wa vibari, kutoka Qubic mita 500 hadi kufikia Qubic mita 250.
"Tunateta kidogo" Ni mkuu wa Wilaya ya Mufindi Bi. Evarister Kalalu akiteta jambo na mwenyekiti wa kamati ya bunge, ardhi, maliasili na mazingira Mh. Jemsy Lembeli, katika kikao baina ya kamati, uongozi wa halmashauri ya Wilaya ya Mufindi na wavunaji wa shamba la miti la taifa la Saohill.
Mwenyekiti wa wavunaji Bw. Christian Ahia (aliyesimama) akichangia hoja katika kikao hicho cha kamati ya Mh. Lembeli na baadhi ya wavunaji wa msitu wa Taifa wa Saohill, uliopo Mufindi mkoani Iringa, wengine katika meza kuu ni viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi , mbunge Mendrady Kigola (mwenye suti nyeusi) na viongozi wa kamati hiyo, wakiwa katika kikao.
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, Bi. Evarister Kalalu akiiomba kamati hiyo ya ardhi, maliasili na mazingira kulifanyia kazi lalamiko la wavunaji, kwa madai kuwa anapata taabu wananchi wake wanapokuwa na tatizo hilo.
Meneja wa msitu wa Sao hill Bw. Salekh Bereko akiwa na kiongozi mwenzie (aliyesuka) itu wa SaoHill wakimsikiliza mtendaji mkuu wa wakala wa huduma za misitu Tanzania Bw. Juma Mgoo (mwenye shati la kitenge)
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kusini Mh. Mendrad Kigola akiwa nje ya Ukumbi wa Halmashauri baada ya kutoka katika kikao cha kamati ya kudumu ya bunge,ardhi, maliasili na mazingira.
HABARI>>>>>>
WAVUNAJI wa miti katika Msitu wa Taifa wa Sao hill uliopo Mufindi mkoani Iringa, wamelalamikia utaratibu wa utoaji wa vibari vya uvunaji wa miti katika msitu huo, kwa madai kuwa umelenga kuwadidimiza wananchi na siyo kuwakomboa kama malengo ya uanzishwaji wa shamba hilo yalivyokuwa hapo awali.
Wakilalamikia mgao huo katika kikao baina yao na kamati ya bunge ardhi, maliasili na mazingira, iliyotembelea wilaya hiyo ya Mufindi kwa lengo la kupata taarifa mbalimbali za maeneo ya kazi ya kamati hiyo, nao viongozi wa Wilaya ya Mufindi wanapaza sauti, wakiiomba kamati hiyo kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo mapema.
Dickson Luteleve mwakirishi wa wavunaji amesema gharama za usajili wa kibali zimepandishwa mara tatu zaidi, kutoka tozo la shilingi Laki mbili hadi kufikia laki 7 na elfu 82, wakati mgao wa vibari ukipunguzwa kutoka Qubic mita 500 hadi kufikia Qubic mita 250 pekee.
Mwenyekiti wa wavunaji Christian Ahia ameiomba kamati hiyo kusaidia kutatua changamoto hiyo ambayo alidai kuwa isipoangaliwa kwa jicho la tatu mpango huo unaweza kuchangia uchumi wa wananchi wa Wilaya ya Mufindi kudumaa
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Bi. Evalister Kalalu amesema amekuwa akipata taabu kwani kimbilio kubwa la wananchi ni katika ofisi yake, na kuiomba kamati hiyo kulitafutia ufumbuzi wa haraka suala hilo kabla halijaleta madhara kwa wananchi.
Naye Mh. Peter Tweve- Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mufindi alisema utaratibu wa kugawa vibari kwa "Qubic mita" sawa kwa waombaji wote pasipo kuangalia uhitaji wa muombaji ni kikwazo kikubwa cha hali ya maendeleo ya wananchi wa wilaya ya Mufindi.
"Ndugu mwenyekiti jambo hili ni shida sasa, kwa ni ugawaji huu haujazingatia hitaji la muombaji, unajua hata hivyi vidole vimetofautiana, kuna vilefu, vinene, vifupi na hata katika utendaji wa kazi vidole hivi vinatofautiana sana, kwa hiyo huu mpango mpya wa kutoa Qubic mita sawa kwa waombaji wote sioni kama hapo mnawatendea haki wananchi wa Mufindi," Alisema Tweve.
Akitoa majibu ya malalamiko hayo, mwenyekiti wa kamati hiyo ya ardhi, maliasili na mazingira mh. Jemsy Lembeli amesema ameyaona mapungufu mbalimbali baada ya kutembelea wilaya hiyo katika sekta ya kamati yake, likiwemo la kutowafikishia wananchi na wadau wa msitu wa saohill utaratibu huo, na kuwa wahusika wamekurupuka kufanya hivyo.
"Niseme hoja zote zilizomo kwenye lisara hii na zile mlizozisema nanyi humu ndani, zote tunazichukua na tutazifanyia kazi immediatilly tukifika tu bungeni, na mrejesho mtauona, lakini niseme jambo hili tumelikisikiahapa ndani kwa mara ya kwanza, Wizara ilishaleta taarifa kwenye kamati, na sisi kama kamati tulishauri wananchi waandaliwe kwanza, waelewe nikwa nini lakini pia wasikilizwe, lakini tunayoyapata hapa ni kuwa wananchi hawajashirikishwa wala hawajaandaliwa vya kutosha juu ya hatua hii, na hatua zote zinazostahili ushirikishwaji hazijafuatwa, mimi ninachomba tuelewane kitu kimoja, haya mtuachieni tutayafanyia kazi, kwani hatuwezi kuwa na majibu hapa ya moja kwa moja,"Alisema Lembeli.
MWISHO
No comments:
Post a Comment