Wednesday, October 23, 2013

AJARI YAJERUHI 38 IRINGA

Daladala aina ya Coster yenye namba za usajiri T.960 AQY  inayofanya safari zake za Kibwabwa mjini Iringa mara baada ya kugongana na gari aina ya Isuzu Tipa, lenye namba SM 3363 katika  Mlima wa Ipogolo eneo la Kisima cha Bibi.    
 Taxi ambayo nayo ilisababishiwa ajari ikiwa katika eneo la tukio, huku askari polisi wakilinda usalama wa mali za abiria na baadhi ya vitu katika eneo la tukio.
 Wananchi wa mji wa Iringa wakitazama ajari hiyo katika mlima wa Ipogolo (Kisima cha Bibi).


 Basi aina ya Coster linalofanya ruti zake Kibwabwa Manispaa ya Iringa likiwa eneo la tukio, baada ya kugongana na Roli Tipper na kusababisha ajali iliyojeruhi zaidi ya watu 30. 

 Bi. Mutbay Ally mmoja wa majeruhi wa ajari hiyo akiwa katika Word namba saba. 
 Mmoja wa majeruhi akipelekwa katika Word kulazwa na wauguzi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Iringa.
 Majeruhi wa ajari iliyohusisha magari manne akisubiri kupata huduma nyingine katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Iringa.

ZAIDI ya abiria 30 wamejeruhiwa katika ajari iliyohusisha magari manne mjini Iringa, baada ya Bus dogo la abiria aina ya Coster kufeli breki na kuyagonga magari matatu, ajali ambayo imetokea majira ya saa saba mchana wa siku ya leo.

Tukio hilo limetokea  katika mlima wa Ipogolo, eneo maarufu mjini Iringa kama "Kisima cha bibi", ambapo ajali hiyo imesababisha majeruhi 38 ambao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani Iringa, huku chanzo cha ajali hiyo kikisemekana kuwa na kuferi breki kwa Bus hilo la abiria,lenye namba T. 960 AQY na kuyavaa magari matatu, gari kubwa aina ya Tipper Isuzu SM784 BNA la manispaa ya Iringa,  Tax pamoja na Hiace.

Akizungumzia hali ya majeruhi wa tukio hilo , Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Iringa Dr. Deogratius Manyama amesema wamepokea majeruhi 38, na waliolazwa ni 8 huku majeruhi watatu wakiwa na hali mbaya, na kuwa majeruhi wengi wameumia zaidi  kichwani na kifuani, huku majeruhi 27 wakiruhusiwa kurudi nyumba kwao kutokana na kutokuwa na majeraha makubwa.

                                                    MWISHO

No comments:

Post a Comment