Gari la wagonjwa aina ya Land Cruiser Hard Top SM, lenye No. za usajiri 9108 likikabidhiwa katika kituo cha Lupembe na mbunge Deo Sanga.
Mbunge wa jimbo la Njombe kaskazini bw. Deo Sanga "Jah People" amekabidhi gari la wagonjwa kwa wananchi wa Kata ya Lupembe Njombe ili liwasaidie kuwapeleka wagonjwa Hospitali.
Gari hilo la pili kukabidhiwa kwa vituo vya afya vya jimbo hilo, ambapo siku ya kwanza Bw. Sanga ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa alikaidhi gari la wagonjwa (Ambulance ) katika kituo cha afya cha Makambako na hivyo magari hayo yote kugharimu zaidi ya shilingi milioni 400.
No comments:
Post a Comment