Monday, March 28, 2011

WANAHABARI WA KIKE NA NGUVU YA PAMOJA




Picha: Juu ni Mwanahabari Oliver Richard Motto wa Iringa na picha ya chini ni Esther Macha wa Mbeya wakiwa katika Kata ya Kapunga Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya ambako huko walipata kero mbalimbali kutoka kwa wananchi, kero ambazo zinawakabiri katika Kata hiyo na kusababisha kudumaza maendeleo.

Waandishi hao wa habari Esther Macha wa gazeti la Majira na Mmiliki wa Blog hii Oliver Motto ambaye pia ni mwandishi wa gazeti la Mtanzania na radio Ebony fm, wameanzisha mpango kazi wa kutafuta habari za wananchi wa vijjini ili kutoa fulsa kwa jamii hiyo sauti zao kusikika.

Mpango huo ambao umelenga kufika vijiji mbalimbali hususani vya pembezoni ambavyo habari za wananchi husika hazisikiki na hivyo kuonekana ni wanyonge kwa kushindwa kusikilizwa kwa kukosa sehemu ya kutolea malalamiko yao.
Bi. Motto na Macha wameazimia kuwaleta wananchi hao katika mstari wa mbele kwa kuzitangaza habari za wananchi hao katika vyombo vyao ili kuibua changamoto zinazoikabili jamii hiyo ya vijijini.

Lengo kuu la mpango huo ni kuwafanya wahusika (Viongozi) kuona kuna umuhimu wa kuwasaidia wananchi hao baada ya kusikia kero na changamoto zinazowakabiri, tofauti na awali ambapo wabanchi hao walikosa fulsa ya kupaza sauti zao kwa viongozi waliopo madarakani kwa kukosa wawakirishi wa kuwapazia sauti zao(Vyombo vya habari).

Usikose kutembelea Blog hii ili kujipatia chakula cha Ubongo kwa kujua mambo mbalimbali yanayoikumba jamii, hususani wale wa vijijini, katika changamoto zinazowakabiri pamoja na mafanikio yao.
Mwisho

No comments:

Post a Comment