Thursday, March 31, 2011

Madiwani watakiwa kuhamasisha upandaji wa miti


Pichani: Ni Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Bi. Gulza Sabir ambaye pia ni diwani wa kata ya Rujewa Mbarali.

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wametakiwa kuwahamasisha wananchi juu ya upandaji wa miti.

Wito huo umetolewa na mkuu wa Wilaya ya Mbarali kanari mstaafu Cosmas Kayombo wakati wa kikao cha baraza la madiwani wa wilaya hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa maji katika mji mdogo wa Rujewa.

Kayombo amesema hali hiyo ya upandaji miti ikifanikiwa wilaya itaepukana na uhaba wa mvua zinazonyesha kwa kiwango kidogo na kutishia ukame na janga la njaa.

No comments:

Post a Comment