Monday, April 18, 2011

Mbunge Kilufi awafunda wanafunzi


Mbunge wa jimbo la Mbarali mkoni Mbeya Bw. Dickson Kilufi amewatembelea wanafunzi wa shule ya sekondari ya Malenga, na kuwataka wajikite katika masomo ya Sayansi ili kuwa wataalamu bora wa siku za usoni.

Kilufi aliwataka pia wanafunzi wa kike kuacha kujikita katika masula ya ngono ambayo huwasababishia kuacha masomo na kushindwa kufikia malengo yao ikiwa pamoja na wanafunzi wa kiume kuacha tabia ya kuwahadaa dada zao, kuwataka wawaone ni ndugu zao, washauriane na kufundishana masomo ili kufaulu kwa pamoja.

No comments:

Post a Comment