Monday, April 4, 2011

Shule ya Magwalisi na ukosefu wa vyoo vya walimu


Picha : Ni ofisa elimu wa mamlaka ya mji wa Rujewa Bw. Gerlad Chavala( Wa pili kushoto) , mwalimu mkuu wa shule ya msingi Magwalisi Jonathan Chengula (Wa pili kulia), na baadhi ya walimu wakikagua baadhi ya madarasa ya shule ya msingi Magwalisi ambayo haina vyoo vya walimu.

Wakizungumza na Blog hii walimu wa shule hiyo wamesema hulazimika kurudi nyumbani kujisaidia pindi wanapojisika haja, na kupoteza muda wa vipindi darasani kutokana na ukosefu wa vyoo vya walimu.
Shule hiyo ina zaidi ya wanafunzi ambao wote wanakaa katika darasa moja, huku wanafunzi wa madarasa tofauti wakisomea chumba kimoja kwa kugeukiana migongo na kila mwalimu kwa upande wake akiendelea kufundisha wanafunzi wake.

No comments:

Post a Comment