Thursday, May 31, 2012

MAMBA WAWAMALIZA WANANCHI RUAHAMBUYUNI



WANANCHI wa Kata ya Ruaha Mbuyuni katika Wilaya ya kilolo mkoani Iringa, wameiomba serikali kuwakwamua na adha ya maji inayosababisha kuuawa na Mamba pindi wanapokwenda mtoni kuchota maji.

Sijawa Mgoe, Rahel Mgoe, Rehema Ngwelele, Zamda muhanga na Aisha Chambo watoto waliokutwa katika mto huo wakichota maji wamesema wanapata taabu kuipata kwa ajili ya tishio ya kuwepo kwa mdudu huyo hatari, lakini pia kitendo cha kuingia ndani yam to huo pindi wanapotaka kuchota maji ni hatari zaidi kwao.

Sijawa amesema watoto wenzake wamepotelea katika mto huo, jambo linalomfanya awe na woga wa kuchota maji, lakini analazimika kuingia katika hatari hiyo.

Ofisa mtendaji wa Kata ya Ruaha Mbuyuni Manyota Magiga amekiri kuwepo kwa shida hiyo ya maji, na kuwa hatari ya Mamba ni tishio kubwa kwa wananchi wake, kwani hata uchumi wa eneo hilo unadidimia kutokana na kukosekana kwa huduma hiyo muhimu.

Maginga amesema kwa wastani wananchi ambao huuawa na Mamba ni wanne kila mwaka jambo linalopunguza nguvu kazi ya RuahaMbuyuni, huku baadhi yao wakiogopa hata kufanya shughuli za kilimo kutokana na tatizo hilo.

Amesema wananchi wanakwama kufanya shughuli za kilimo cha umwagiliaji ambacho ndiyo kinategemewa na wananchi wa eneo hilo kwa kuwa maji hutoa katiuka Mito hiyo yenye tishio la mamba na viboko.

Anafafanua kuwa mazao yanayolimwa katika Kata ya Ruaha Mbuyuni ni Vitunguu, Nyanya, Karanga, Mahindi na maharage, na kilimo cha mazao hayo ni kile cha umwagiliaji, na kuwa endapo hakutapatikana muafaka wa tatizo hilo, kilimo hicho kinaweza kikapotea kwa hofu ya mdudu huyo.


No comments:

Post a Comment