MBUNGE KIGOLA WA MUFINDI APATA AJALI
Taarifa za awali ambazo mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com umezipata kutoka mkoani Iringa zinadai kuwa mbunge wa jimbo la Mufindi kusini Mendrady Kigolla amepata ajali mbaya na kulazwa katika Hospitali ya mkoa wa Iringa.Kwa mujibu wa mmoja kati ya madaktari wa Hospitali ya mkoa wa Iringa wamedai kuwa mbunge huyo amefikishwa Hospitalini hapo leo majira ya jioni na kuwa hadi sasa bado amelazwa katika Hospitali hiyo ya mkoa akiendelea kupatiwa matibabu zaidi.
No comments:
Post a Comment