Friday, May 18, 2012

R.I.P (REST IN PEACE) PATRICK MUTESA MAFISANGO

Ni jeneza la aliyekuwea mchezaji machachari , wa timu ya Simba Sports Club ( Wekundu wa Msimbazi) marehemu Patrick Mutesa Mafisango, aliyefariki kwa ajali mnamo tarehe 16


Mchezaji wa timu ya Simba Tanzania na timu ya Rwanda Patric Mutesa Mafisango aliyefariki dunia kwa ajali ya gari maeneo ya Tazara akielekea nyumbanikwake wakati akijaribu kumkwepa mwendesha pikipiki ambapo gari  lilipinduka na kumsababishia maumivu makali na kufariki dunia wakati akikimbizwa Hospital.
 
Watu aliokuwa nao kwenye gari hilo ni pamoja na  dada yake, na mdogo wake.
 Wadau, mashabiki na wapenzi wa soka, wakiwa wamebeba bango linaloandikwa R.I.P. MAFISANGO, Ikiwa ni moja ya njia ya kuonyesha majonzi yao kwa mchezaji mahiri wa timu ya Simba, aliyefariki siku ya tarehe 16 usiku kwa ajali, masaa machache baada ya kupokelewa nchini yeye na timu nzima ya Simba.
MWENYEZI MUNGU AILAZE MAHALA PEMA ROHO YA MAREHEMU ..PATRICK MAFISANGO




No comments:

Post a Comment