Wednesday, May 16, 2012

TBL YAKABIDHI ZAWADI YA GARI NA BAJAJI


Kampuni ya bia nchini (TBL) inayozalisha vinywaji kama Safari, Kilimanjaro, Castle Lager, Castle Milk, Castle Lite, Safari water, Ndovu, Redd's, Grand Malta nk. imekabidhi zawadi ya gari aina ya Mitsubish yenye No. T-604-BXU,  pamoja na  Bajaj No. T-910 BYR kwa mshindi Bw. Augustine Kisinga, wa mji wa Makambako katika mkoa wa Njombe 




Mshindi wa Gari na Babaj Bw. Augustine Kisinga akiendesha Bajaj baada ya kukabidhiwa funguo za usafiri huo, mjini Makambako.



Mkurugenzi wa mamlaka ya mji mdogo wa Makambako Bw. Godwin Beene, akimpongeza meneja wa TBL kanda ya kusini Bw.James Kavuma kwa zawadi  kwa mwananchi wa mji wake.


Mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya TBLBw. Frances akionyesha baadhi ya vinywaji vinavyozalishwa na kampuni hiyo.


Ofisa biashara wa kampuni ya Safari Bi. Asta Hiza na James Kavuma meneja wa kampuni ya TBL kanda ya kusini wakiangalia wafanyakazi wa kampuni hiyo wanaposhangilia gari na bajaj kama moja ya vifaa vyao vya kazi.


Gari na bajaj zikiwa katika ofisi ya Bw. Augustine Kisinga, zilizofika katika ofisi yake kama ni zawadi ya ushindi wake alioshindanishwa na mawakala kutoka mikoa ya Arusha, Mwanza na Dar es salaam.


Mshindi wa zawadi zilizotolewa na Kampuni ya TBL Bw, Augustine Kisinga, akiwa katika moja ya bidhaa zake


Meneja mauzo Iringa na Ruvuma, Bw. Reymond Degeka akiwa katika picha ya pamoja katika makabidhiano ya Gari na bajaj katika mji wa Makambako









No comments:

Post a Comment