Monday, April 8, 2013

HIVI NDIVYO MANGULA ALIVYOJICHUKULIA JIKO


Gari lililowapakiza maharusi- Bi Yoranda na Bw. Philip Mangula likiwasili katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kusini. 
 Maharusi wakiteremka katika usafiri wa kisasa, kuingia  kanisani kufunga pingu za maisha.


  
 Wakiwa katika picha ya pamoja Askofu na Mashekhe.
 Bw. Philip Mangula akiweka sahihi katika cheti cha ndoa, kama ni ushahidi wa yeye na mkewe kuingia katika mkataba wa kuishi pamoja.
 Bi. Yolanda akiweka sahihi katika cheti chao cha ndoa, kama ni ushahidi wa yeye na mumewe kuingia katika mkataba wa kuishi pamoja.
 Philip Mangula akiwa na mkewe katisani, baada ya kufunga pingu za maisha na hivyo kuwa mwili mmoja.
 Waziri mkuu - Mizengo kayanda Peter Pinda, akiteta jambo na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdurahaman Kinana (Kulia) ni Mkuu wa mkoa wa Njombe Assery Msangi. 
 Viongozi wa dini mbalimbali wakisikiliza somo katika misa hiyo ya harusi.
 Waziri mkuu Mizengo Pinda, akisalimiana na viongozi mbalimbali mkoani Iringa na Njombe, kabla ya kuingia kanisani katika sherehe ya ndoa.
  
"HAYAWI hayawi sasa yamekuwa", Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Philip Mangula (72 ) ameepuka fedheha na fitina za wanasiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 baada ya kufanikiwa kufunga pingu za maisha na mwalimu wa Shule ya Sekondari, Yolanda Kabelege ( 54).


Mangula amefunga ndoa hiyo  Aprili 06, majira ya saa 8: 12 mchana katika Usharika wa Njombe wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kusini.  


Yolanda ambaye ni mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Imalinyi iliyopo Wilaya ya Wanging’ombe mkoa mpya wa Njombe, amefunga ndoa hiyo na Mangula ikiwa ni miaka tisa (9) tangu kiongozi huyo wa CCM ampoteze mke wake wa kwanza, marehemu Lucy Mng’ong’o Septemba 3, mwaka 2004.


Katika ibada hiyo ya ndoa iliyoongozwa na Askofu wa KKKT, Dayosisi ya Kusini, Isaya Mengele akisaidiwa na Askofu mstaafu wa Kanisa hilo Solomon Swalo, Mangula na mkewe walikabidhiwa hati ya ndoa yenye namba B  0401290 kama ushahidi uliotolewa na kanisa hilo mbele ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya sheria ya ndoa ya mwaka 1971.


Akihubiri kabla ya kuwaunganisha wanandoa hao mbele ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdurahaman Kinana na viongozi wengine waandamizi wa serikali wakiwamo Mawaziri,Wakuu wa Mikoa, Wilaya na viongozi wa vyama vya siasa, Askofu Swalo, alisema kuanzia sasa, serikali inapaswa iache kukaa kimya na kukemea mauaji ya raia yanayoendelea nchini ambayo kwa namna moja ama nyingine yanaathiri zaidi maisha ya wanawake na watoto na kusababisha familia nyingi kusambaratika.


“Hebu serikali sasa ione haki ipo wapi, hivi kwa nini watu wanachinjana,wanauana na wengine kuua wake zao na watoto kwa sababu zisizo na msingi.Msikae kimya, chukueni hatua kwa hali ilivyo sasa maana mauaji hayo ni hatari kwa taifa…Mangula hihi sasa wewe ni Mheshimiwa,hebu mgawie na mkeo huo uheshimiwa,”Alisema Askofu Swalo.


"Lakini pia Mangula na mkeo Yolanda,tambueni kwamba vipihavitakiwi wala ubabe usifanyike katika kuamua mabo yenu kwa sababu jambo zuri kama mnatofauti zenu kaeni mezani na myamalize bila kuwapa watu faida,"Alionya Askofu Swalo.

Mangula awasili Kanisani  

Makamu Mwenyekiti huyo wa CCM Bara aliwasili kanisani hapo majira ya saa 6:20 mchana akiwa katika gari jeusi la kifahari lenye milango sita aina ya Toyota Lincolin lenye namba T 215 likisindikizwa na maofisa wa usalama wa taifa pamoja na viongozi kadhaa wa serikali akiwamo Naibu Waziri wa Ujenzi, Gerson Lwenge.

 Katika msafara huo,Mangula alikuwa akiungwa mkono pia na watoto wake wanne waliozaliwa na marehemu Lucy Mng’ong’o ambao ni Twide, Lukelo, Malumbo na Nemela ambao walishindwa kuzuia furaha yao kanisani hapo baada ya baba yao kuvisha pete mwalimu Yolanda Kabelege.

Tofauti na ilivyotarajiwa na wengi, Mangula alisindikizwa na Katibu Mkuu Abdurahaman Kinana bila wajumbe wengine wa sekretarieti ya chama hicho.

Waziri Mkuu Pinda

Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliwasili katika mji wa Njombe saa  6:55 akitokea mkoani Mbeya na kuungana na wanandoa hao katika kanisa kuu la KKKT Njombe mjini kabla ya kuelekea katika eneo maalumu la tafrija ambalo ni chuo cha ualimu Hagafilo.

Mawazo yangu binafsi
Ninampongeza sana kiongozi huyu, kwani kwa wadhfa alionao angeweza kubadirika na kuoa mwanamke mwenye muonekano tofauti ambao unalingana na cheo chake, nikiwa na maana angehitaji kuwa na mwanamke ambaye anauwezo kifedha, na sifa za kumpamba nje katika jamii.

Lakini Mangula amerudi nyumbani na kumuoa mwanamke ambaye kwanza niwa umri wake, yaani ambaye anawatoto, anayefahamu nini anahitaji kufanya katika ndoa, anayefahamu mjukumu yake, kwani Mama Yolanda ni mama mtu mzima mwenye watoto na hata wajukuu.

 Kiongozi huyu kwa mtazamo wangu, niwa mfano wa kuigwa, kwani hata harusi yake ni tofauti na vile ambavyo wengi walitegemea, kuwa ingekuwa niya kisasa sana, LA KHASHA!! ilikuwa niya kawaida sana.

Mungu aibariki na kuiongoza ndoa yake, iwe ni ile yenye furaha na amani ndani ya nyumba yao, na siyo ya muonekano wa nje, huku ndani "Wanaota joto ya jiwe"...Amen.



No comments:

Post a Comment