Barnaba Haran, ofisa mradi wa Tanzania Capacity and Communication Program (Care - TCCP) akiandika maazimio ya wanasemina wa mradi wa "Sheria ya kudhibiti Ukimwi ya mwaka 2008" - yaliyotolewa chini ya ufadhili wa THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY, semina iliyofanyika katika Kata ya Nyalumbu Ilula, katika Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.
Maazimio ya nini kifanyike kwa wanaoeneza Ukimwi kwa makusudi na wale wanaowanyanyapaa wanaoishi na VVU.
Dr. Wilson Mwakibete akitoa mada juu ya madhara ya Unyanyapaa kwa wanaoishi na VVU, katika semina ya siku mbili mjini Ilula.
Maoni ya sheria gani zichukuliwe kwa wanaoeneza kwa makusudi Ukimwi na wanaowanyanyapaa wagonjwa wa Ukimwi.
Kushoto ni Nathan Magova kaimu mratibu wa mradi wa sheria ya kudhibiti Ukimwi ya mwaka 2008 chini ya ufadhili wa THE FOUNDATION FOR CIVIL , akiwa na kaimu mkurugenzi wa Wilaya ya Kilolo (katikati) Venance Mwaikambo na kulia ni ofisa mtendaji wa kata ya Nyalumbu Jailos Kikoti wakiwa katika semina hiyo.
"TUPO WANGAPI?????" TULIZANA......Ni moja ya mafunzo waliyopatiwa wanasemina hao wa Kata ya Nyalumbu Ilulla, Wilayani Kilolo, huku wakihimizwa "WATULIZANE"
Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo (katikati) Venance Mwaikambo akisisitiza jambo katika semina hiyo.
Nathan Magova kaimu mratibu wa mradi wa "sheria ya kudhibiti Ukimwi ya mwaka 2008" Akisikiliza malalamiko ya wanasemina dhidi ya unyanyapaa wanaofanyiwa watu waishi o na Virus Vya Ukimwi (VVU).
Nathan Magova kaimu mratibu wa mradi wa "sheria ya kudhibiti Ukimwi ya mwaka 2008" akitoa elimu ya sheria ya Unyanyapaa na uenezaji wa VVU kwa makusudi, katika semina hiyo.
Ofisa mtendaji wa kata ya Nyalumbu Ilula Jailos Kikoti akiwa katika semina hiyo.
Wanasemina wakisikiliza kwa makini.
Kulia ni meneja wa mradi wa FHI 360 Isihaka Banzi, akiwa katika mafunzo hayo.
Isihaka Banzi na mwenzie Said Mbosa, wakiwasikiliza wanasemina.
Wanasemina wakiwa katika ukumbi wakipatiwa elimu dhidi ya sheria za kudhibiti Unyanyapaa na uenezaji Ukimwi kwa makusudi.
Lusiana Kisumbe (Mwakirishi wa walemavu) ambaye yeye ni Mlemavu wa macho akisaidiwa jambo na Fidelis Kawovela mwenyekiti wa kijiji cha Matalawe Ilula katika semina hiyo ya siku mbili.
WANANCHI wa Ilula katika Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa
wamelalamikia tabia ya baadhi ya watu kuendeleza tabia ya unyanyapaa kwa
wagonjwa wa Ukimwi, huku baadhi yao wakigomea hata kununua bidhaa zinazouzwa na
waathirika hao.
Wakizungumza katika mafunzo ya siku mbili yaliyotolewa na mradi
wa sheria ya kudhibiti Ukimwi ya mwaka 2008 chini ya ufadhili wa THE FOUNDATION
FOR CIVIL na kufanyika Ilula Kata ya Nyalumbu katika Wilaya ya Kilolo
mkoani Iringa, wananchi hao tabia hiyo inadumaza uchumi wa waathirika, kwani
baadhi ya wananchi wanaamini kuwa wakinunua bidhaa kwa mwenye VVU wataambukizwa
ugonjwa wa Ukimwi.
Lusiana Kisumbe amesema kuna aina mbaya ya unyanyapaa kwa
wagonjwa wa ukimwi, kutokana na baadhi ya wananchi kushindwa hata kununua
biashara zinazouzwa na waathirika hao, hususani chakula na vinywaji.
“Unapopata Ukimwi jamii inakutenga, au hata unapopita tu njiani
unasikia wanasema hilo lina ukimwi, yaani watu wanawazungumzia watu wenye
Ukimwi vibaya, wanadhani hata ukila nao chakula unaweza kjuwaambukiza, yaani
wenye ukimwi hawana raha kutokana na kuzungumziwa kila mara,” Alisema Lusiana.
Lusiana amesema kuna haja ya kupatiwa elimu ili kuwakomboa na
dhana hiyo ya unyanyapaa ambayo inawafanya wananchi waogope kupima kwa kuhoifia
kutegwa na jamii.
Mwajuma Mgeveke amesema unyanyapaa upo hata kwa wanandoa, ambapo
wanaume wamekuwa wakiwatenga na hata kuwafukuza wake zao pindi wanapogundulika kuwa
na ugonjwa wa Ukimwi, licha ya kuwa wanaume hao wao hawataki kupima ili kujua
afya zao.
Ofisa mtendaji wa Kata ya Nyalumbu Jailos Kikoti amesema kuna
haja ya akuandaa machapisho ya kuzuia unyanyapaa ili wananchi wafahamu madhara
ya tabia hiyo, ikiwa pamoja na kubandika makaratasi yenye machapisho ya sheria
za kuwabana watu wanaoeneza ugonjwa wa Ukimwi Makusudi.
“Mimi kwa kuanza na elimu hii ya kudhibiti Unyanyapaa Kata yangu
itaandaa machapisho yanayoelezea athari za unyanyapaa, pamoja na madhara ya
uvunjaji wa sheria ya matumizi ya dawa za kulevya,” Alisema Kikoti.
Pia amesema wanampango wa kuthibiti uvaaji wa mavazi yasiyo ya
heshima kwa wahudumu wa Baa na wauzaji wa vileo hilo likiwa ni zoezi la
kupambana na maambukizi ya VVU.
Aidha meneja wa mradi wa FHI 360 Isihaka Banzi amesema kuna
haja elimu ya madhara ya unyanyapaa ikafundishwa shuleni ikiwa pamoja na sheria
zifanye kazi yake kwa wanaowanyanyapaa wagonjwa wa Ukimwi.
Kaimu mratibu wa mradi wa sheria ya kudhibiti Ukimwi
ya mwaka 2008 Nathan Magova ameitaka jamii kuacha tabia hiyo ya
unyanyapaa, na kuwa wananchi wenye kuendekeza destuli hizo watachukulia hatua
za kisheria.
Magova amesema tayari mradi umeanza kutekeleza sheria ya
Unyanyapaa kwa kutoa mafunzo katika Kata
ya tatu za Nyalumbu, Bomalang’ombe na kata ya Mtitu katika Wilaya ya Kilolo.
“Sheria hii inaruhusu anayeishi na Virus vya Ukimwi kumshitaki mtu yoyote anayemnyanyapaa, na kuna makosa na adhabu
amabzo zimeainishwa kwa mtu anayeeneza Ukimwi kwa makusudi, na tumeanza kutoa
mafunzo kwa Kata zilizopo Wilaya ya Kilolo, kwa maana ya Kata ya Nyalumbu,
Bomalang’ombe pamoja na Kata ya Mtitu, zote za Kilolo,” Alisema Magova.
Hata hivyo Venance Mwaikambo kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Kilolo ambaye alikuwa mgeni rasmi wa kufunga mafunzo hayo ya siku
mbili amewataka wananchi hao kuacha tabia hiyo ya unyanyapaa na kueneza Ukimwi
kwa makusudi, huku akiiasa jamii ibadili mienendo na tabia zinazopelekea kupata
maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi.
MWISHO
No comments:
Post a Comment