Saturday, May 4, 2013

AJALI YAUA 7 YAJERUHI 44 IRINGA


Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Iringa ASP Michael Kamuhanda, akitoa taarifa ya tukio la ajali Nyololo mkoani Iringa.

 Bus aina ya Taqwa ambalo limepata ajali eneo la Nyololo mkoani Iringa.
Wananchi wakiangalia mabaki yatokanayo na ajali hiyo mbaya.

ABIRIA saba wamekufa papo hapo baada ya basi la TAQWA waliokuwa wakisafiria kutoka jijini Dar es salaam kwenda Mbeya kugongana uso kwa uso wakati gari aina ya Scania likitaka kulipita basi hilo.

Ajali hiyo ambayo imetokea jana (juzi) majira ya saa kumi na moja jioni katika kijiji cha Nyololo Mufindi katika Mkoa wa Iringa, imepoteza maisha ya watu hao saba akiwemo dereva na utingo wake.

Akizungumzia ajali hiyo Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda alisema tukio hilo lilitokea katika barabara kuu ya Iringa na Mbeya ambapo gari namba TI04BZZ..T309 BTS Scania mali ya Sogea Sotom mkazi Dar es salaam na lilikuwa likiendeshwa na Johanis Udingo kabila Muhaya (32).

Kamuhanda alisema Gari hiyo ilikuwa ikitaka kulipita basi la Taqwa lenye namba T 273 CBR Nissan lililokuwa likiendeshwa na Abrahaman Abdul  (32) Mwarabu wa Ilala jijini Dar es salaam, na kusababisha kugongana uso kwa uso na gari lenye namba  T 597 AMZ   / T227 AVKSC Scania mali ya Nyato Transipot Ltd DSM iliyokuwa ikiendeshwa na dereva ambaye hakuweza kufahamika jin lake.

Akitaja majina ya watu waliokufa katika ajali hiyo Kamuhanda alisema ni Abdalahman Abdul (32) Mwarabu ambaye ni dereva wa basi, Nassoro Rashid Said (27) kabila mzigua wa Tanga ambaye alikuwa ni Kondakta wa basi hilo.

Wengine ni Shasin Ramadhan Shaban (32) fundi magari kabila Msambaa anayeishi Dar es salaam,  Ally Suleiman (26) Mwarabu na mfanyabiashara wa Dar es salaam, pamoja na abiria watatu ambao hawajafahamika majina yao.

Aidha Kamuhanda alisema pia ajali hiyo imesababisha kujeruhiwa kwa abiria 25, wanaume wakiwa 16 na wanawake 9 ambao wote wamelazwa katika Hospitali ya Mafinga Wilayani Mufindi Iringa, na kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi.

Hata hivyo mganga mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Mufindi  Dr. Erick Bakuza alisema walipokea majeruhi 44, wanaume wakiwa 27  na wanawake 17,  huku akipokea maiti 7, kati yake Wanaume wakiwa 6  na mwanamke mmoja.

Dr. Bakuza alisema kati ya majeruhi hao 44 tayari majeruhi 3 wameruhusiwa na hivyo Hospitali kubaki na majeuhi  41, huku 3 wakiwa na hali mbaya na kufanyiwa utaratibu wa kuwasafirisha katika Hospitali kubwa jijini Dar es salaam pamoja na Hospitali ya Rufaa Iringa.
MWISHO.

No comments:

Post a Comment