Sunday, May 5, 2013

TARWOC DROP- IN, ULEVI CHANZO CHA UKATILI


Mbarozi wa Kata 20 wakisubiri kukabidhiwa usafiri wa Baiskeri, nje ya kituo cha shirika la TARWOC DROP IN.    
 Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa Gervas Ndaki, akikabidhi Baiskeri kwa mabarozi wa Kata, kutoka Manispaa ya Iringa na Iringa Vijijini.
Baadhi ya mabarozi wakiwa na Baiskeri zao, baada ya kukabidhiwa rasmi na naibu Meya wa Manispaa ya Iringa

 Pendo Luoga (kushoto) Meneja wa kituo cha TARWOC DROP IN- Mkimbizi na Benedict Kibiki (mwenye suti) Ofisa mkuu wa shirika la TARWOC DROP IN- Wakishangilia baada ya makabidhiano hayo.
 Mabarozi wa Kata, wakifurahia msaada huo.
 Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa Gervas Ndaki- akitoa neno baada ya kukabidhi Baiskeri hizo kwa mabarozi.

Pendo Luoga na Benedict Kibiki wakimsikiliza kwa umakini Naibu Meya wa manispaa ya Iringa Gervas Ndaki.
Nasri Mwampeta mmoja wa mabarozi akitoa neno la shukrani kwa naibu meya Gervas Ndaki.
Viongozi wa shirika la TARWOC DROP IN- wakimuaga Meya baada ya makabidhiano hayao ya usafiri wa Baiskeri kwa Mabarozi 20 wa Kata za Iringa Manispaa na Iringa Vijijini. 
Johari Ngeng'enga (wakwanza kushoto) akiwa na Doreen Mgongolwa pamoja na barozi mwingine ndani ya kituo cha TARWOC DROP IN.
Amina Tenywa barozi wa Kata aya Mseke akiwa na akiwa na Grace Sanga barozi w Kata ya Kihesa wakisikiliza neno ndani ya kituo cha TARWOC DROP IN- Mkimbizi Manispaa ya Iringa.
Benedict Kibiki- ofisa mkuu wa shirika la TARWOC DROP IN, na Pendo Luoga, wakiwasikiliza mabarozi changamoto zinazowakabiri katika utoaji wa huduma katika jamii.
Farida Mpogole, diwani wa Viti malumu Kanda ya Kihesa akizungumza na Mabarozi wa Kata, juu ya utunzaji wa usafiri huo. 
Zawadi Kilovele- Mshauri wa kituo cha TARWOC DROP IN, akitoa maelezo ya kazi zake kwa mabarozi wa Kata.

UNYWAJI wa pombe kupindukia, umasikini pamoja na kukosekana kwa elimu ya madhara ya ukatili wa kijinsia miongoni mwa jamii hususan waishio vijijini, ni moja ya sababu inayochangia tatizo la unyanyasaji kuendelea.

Hayo yamezungumzwa na Pendo Luoga meneja wa kituo cha shirika la TARWOC DROP- IN, kilichopo Mkimbizi, kituo kinachojihusisha na huduma kwa wanyanyasaji na wanyanyaswaji wa ukatili nchini.

Naye Benedict Kibiki, ofisa mkuu wa shirika la TARWOC DROP- IN amesema kituo chake kimehudumia zaidi ya waathirika 1500 wa unyanyasaji na ukatili wa kijisia, na tatizo kuu likiwa ni uwepo wa mila na destuli potofu, uchumi mdogo pamoja na unywaji wa pombe.

"Tatizo hili linatokana na baadhi ya mila na destuli zetu zilizopitwa na wakati, hasa kwa hili la kujiona sisi wanaume kama ndiyo kila kitu, lakini suala la uchumi nalo linachangia ukatili na unyanyasaji, mtu mwanaume au mwanamke mwenye kipato duni anafanyiwa unyanyasaji kutokana na hali yake duni, la tatu ni kukosekana kwa elimu miongoni mwa jamii, kwani baadhi ya wananchi hawana elimu ya namna ya unyanyasaji," Alisema Kibiki.

Aidha aliongeza kuwa changamoto inayokikabili kituo hicho cha TARWOC DROP- IN cha Mkimbizi ni kukosekana kwa ausafiri wa gari, na hivyo kushindwa kuwafikia wananchi waishio maeneo ya mbali na kituo.

Kibiki alisema Kata 16 zilizopata baiskeri hizo ni kutoka ndani ya Manispaa ya Iringa huku Kata 4 za Iringa vvijijini ambazo ni Kata ya Mseke, Ifunda, Kihologota na Kata ya Kising'a.

Naye Doreen Mgongolwa katibu wa mabarozi wa kupingana na ukatili Manispaa ya Iringa na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, amesema ulevi wa  pombe za jadi na za kisasa ni chanzo kikuu cha migogolo katika familia na matukio ya ukatili.

"Ulevi ni tatizo kubwa sana linalochangia unyanyasaji na ukatili wa kijinsia, hapa ninazungumzia unywaji wa pombe zote, iwe za kienyeji au hizi pombe za viwandani bia, mtu akilewa anafanya mambo ambayo hata siku ya pili ukimueleza anaomba msamaha tu, kwa hiyo ulevi ni vchanzo kikuu cha unyanyasaji na ukatili wa kijinsia," Alisema Doreen

Hata hivyo kituo hicho cha TARWOC DROP - IN kimewakabidhi Baiskeri 20 zenye thamani ya shilingi Milioni 3.5 mabarozi wa Kata zilizopo katika  Manispaa ya Iringa na Halmashauri ya Iringa Vijijini, lengo likiwa ni kuboresha utoaji wa huduma za unyanyasaji na ukatili wa kijinsia kwa jamii iishio maeneo ya mbali.

Baiskeri hizo ambazo zimekabidhiwa na naibu Meya wa Manispaa ya Iringa Gervas Ndaki, huku akiwataka mabarozi hao kuvitunza vitendea kazi hivyo ambavyo ni chachu katika ufanisi wa kazi zao za kuwafikia kwa urahisi wananchi.

Benedict Kibiki ofisa mkuu wa shirika la TARWOC DROP- IN amesema Baiskeri hizo wamepatiwa mabarozi wa Kata 16 za Manispaa ya Iringa, na Kata 4 za Iringa Vijijini, huku akisema changamoto kubwa inayokikabili kituo ni kukosekana kwa usafiri wa gari la uhakika, katika kuwafikia wananchi wa maeneo ya vijiji vya mbali.

Kibiki amesema kwa sasa wameanza na usafiri kwa ngazi ya Kata kuhudumia mitaa, kwani awali walitembea kwa zaidi ya km 10 na hivyo utoaji wa huduma ya Unyanyasaji na Ukatili kukwamishwa.

"Awali mabarozi wetu wa Kata walilazimika kutembea umbali wa zaidi ya km 10 kuwafikia wananchi wa vijiji vya mbali, lakini Baiskeri hizi zitawarahisishia sana kazi, kwa kupunguza mwendo ule wa kutembea kwa miguu," Alisema Kibiki. 

Naye Amina Tenywa barozi wa Kata ya Mseke amesema vitendea kazi hivyo ni msaada mkubwa kwa jamii, katika kufikisha elimu na huduma kwa waathirika wa ukatili na unyanyasaji wa kijinsia.

MWISHO





No comments:

Post a Comment