Sunday, May 5, 2013

TUKIO LA KULIPULIWA KWA KANISA WATU SITA WASHIKILIWA


Eneo lenye utepe ndipo kinachohisiwa kuwa bomu ndipo kilipotua na kulipuka katika Kanisa la Mt Joseph Olasiti Arusha ambapo Balozi wa Papa alikuwa akihudhuria ibada ya Kuzindua Parokia kanisani hapo....

 Hili ndilo kanisa lililolipuliwa jijini Arusha.
Baadhi ya majeruhi wa mlipuko uliotokea kanisani Arusha.



WAZIRI wa mambo ya ndani Dr. Emanuel Nchimbi ametangaza kukamatwa kwa watu 6 wanaoshikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano,  kutokana na tukio la kulipuliwa kwa kanisa kathoriki jijini rusha, ambapo mwanakwaya mmoja amepoteza maisha, huku watu 60 wakijeruhiwa.

 Tukio hilo ambalo limetokea majira ya saa tano asubuhi ya tarehe 5 mwezi huu Mei  wakati  Parokia  Mpya ya Mt. Joseph Mfanyakazi iliyokuwa inazinduliw rasmi na kabla ya tukio la uzinduzi kutokea mlipuko uliojeruhi watu 60, huku mmoja akipoteza maisha.

Parokia hiyo teule ya orasiti- ya mtakatifu Joseph mfanyakazi – Arusha ilikuwa ikifanya uzinduzi mpya, ambapo Kwa mujibu wa taarifa zinazosikika moja kwa moja kupitia Radio Maria, Tanzania, mlipuko huo umetokana na kitu kinasadikika kuwa ni bomu. 

Hata na hivyo haijafahamika ikiwa mlipuko huo ulikuwa niwa  bomu la kutegwa ama la kurushwa kwa mkono kutokana na jeshi la polisi kuendelea na uchunguzi wake juu ya mlipuko huo.

Inaripotiwa kuwa wengi wamejeruhiwa miguuni na kulazimika kuwahishwa hospitalini kwa matibabu zaidi. Hakuna taarifa zozote za kifo zilizoripotiwa katika tukio hilo.

Aidha viongozi mbalimbali wa Kanisa akiwemo mwakilishi wa Papa aliyekuwa anatabaruku Kigango hicho kilichozaliwa mwaka 2008 kuwa Parokia, Padre Francisco Padilla na viongozi wa jeshi la polisi na usalama, wanaendelea na kikao ili kuamua hatima ya misa iliyokatizwa.

Hata hivyo kutokana na usalama wa waumini waliokuwemo katika kanisa hilo, wametakiwa kuondoka na hivyo kukatishwa kwa misa na matukio hayo ya uzinduzi.

Viongozi mbalimbali wa mkoa wa Arusha, akiwemo mkuu wa mkoa, Mbunge wamefika katika eneo hilo, huku jeshi la polisi likiendelea na uchunguzi zaidi kuhusiana na mlipuko huo.







No comments:

Post a Comment