Sunday, May 19, 2013

MBUNGE MSIGWA AKAMATWA












MBUNGE wa jimbo la Iringa mjini kupitia tiketi ya chama cha demokrasia ana maendeleo CHADEMA amekamatwa na jeshi la polisi mkoani Iringa kufutia vurugu za wafanyabiashara wa soko la Mashinetatu.

Vurugu hizo ambazo zimeanza majira ya saa moja asubuhi, zimesababisha pia watu 50 kukmatwa kwa tuhuma za kuhusika na vurugu hizo.

Aidha Mchungaji Msigwa amekamatwa majira ya saa nane mchana baada ya kudaiwa kuungana na wafanyabiashara hao kuanzisha vurugu hizo ambazo ni madai ya wafanyabiashara kutaka kuendesha shughuli zao katika eneo hilo la Mashinetatu.

Madai ya wafanyabiashara hao yametokana na kuhamishwa eneo hilo na  kupelekwa katika uwanja wa Mlandege ambako wanalalamikia kuwa ni nje ya mji , hakuna huduma muhimu  na hivyo kukosa wateja.


Mabomu pamoja na magari yenye maji ya kuwasha vimetumika katika kuwadhibiti wafanyabiashara hao, ambao baadaye waliungana na wananchi mbalimbali, wakipinga kuondolewa kwa soko hilo maalufu la Mashine tatu, huku baadhi ya barabara zikifungwa na matairi yakichomwa moto katika kukabiliana na nguvu ya jeshi la Polisi.

Mtafaruku huo umezua balaa, huku baadhi ya wananchi wakipoteza watoto na mali mbalimbali kuharibiwa, na kusababisha maduka yote ya mji wa Iringa kufungwa na  mji kuzizima, kufuatia vuta nikuvute hiyo ya uwepo wa biashara katika soko la Mashinetatu, biashara inayofanyika mara moja kwa wiki, ambayo ni siku ya jumapili pekee.

Vuta nikuvute hiyo inatokana na kukinzana kwa pande mbili, baina ya mbunge wa jimbo la Iringa mjini (CHADEMA) mchungaji Peter Msigwa ambaye anawataka wafanyabiashara hao waendelee kufanya shughuli zao za utafutaji wa ridhiki eneo la Mashinetatu, huku Manispa ya Iringa ikiwawataka waondoke.

Akizungumzia sakata hilo, kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Iringa SACP Michael kamuhanda amesema  tayari watu 50 wanashikiliwa na jeshi hilo la polisi kwa tuhuma za kuhusika katika vurugu hizo.


No comments:

Post a Comment