Falesy Kibassa akizungumza na wanahabari pamoja na wasomi wa vyuo vikuu, katika ukumbi wa chuo cha afya mjini Iringa.
Baadhi ya wanachuo na wanahabari wakifutilia jambo kwa umakini.
Wanahabari akiwemo mmiliki wa mtandao huu na mwandishi wa Star Tv/ Rfa (Oliver Motto) anayeandika, akiwa na wanahabari wenzake wakichukua hbari katika ukumbi wa Chuo cha afya Iringa, (wa kwanza kulia) ni Clement Sanga wa Chanel Ten. (wakwanza kushoto) Godfrey Mushi mwandishi wa gazeti la Nipashe , anayemfuata ni Irene Mwakalinga wa TBC.
Wanachuo wakifuatilia mazungumzo ya Falesy Kibassa, Mhadhiri wa chuo kikuu cha Mzumbe, alipokuwa akifanya mazungumzo.
Mwandishi CHANEL TEN Clement Sanga akiwajibika katika ukumbi wa chuo cha afya, wakati mhadhiri Kibassa akizungumizia mustakabari mzima wa hali ya Uchumi na Siasa mkoani Iringa.
VIJANA wametakiwa kuacha kutumiwa na wanasiasa na wanaharakati za kisiasa na badala
yake wafanye arakati zao bila kujiingiza
katika vyama vya siasa ili kuleta maendeleo katika taifa., huku wahadhiri nao
wakionywa kurukaruka katika vyuo.
Akizungumza
na baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani Iringa Mhadhiri wa chuo kikuu
mzumbe kilichopo mkoani Morogoro Falesy
Kibassa amesema vijana wanatakiwa kuwaacha wanasia na wanarakati wafanye
harakati zao.
Kibassa
amesema vijana wanapaswa kuwa makini na wanasiasa kwani wamekuwa wakiwatumia
vijana katika masuala yao yenye maslahi binafsi na hivyo kundi hilo kuliingiza
katika majanga ambayo ni hatari.
Amesema
vijana wanapaswa kutumia muda wao kupigana na adui Umasikini, Maradhi, huduma duni, miundombinu
mibovu, ukosefu wa mitaji, ukosefu wa maeneo salama, magonjwa.
Aidha
amewataka wasomi waache ushabiki wa kisiasa ambao hauna maana, na kuwaasa
wahadhiri kutumia elimu na utaalamu walionao kuwashauri wanasiasa masuala yenye
maslahi kwa uchumi wa taifa.
Amesema
kwa kuwa nchi inaendeshwa kwa falsafa ya UCHUMI na SIASA, na kuwataka wasomi
watumie taaluma yao kwa manufaa ya watanzania.
“Vijana
wasomi mlioko vyuoni achaneni na ushabiki wa kisiasa kwasababu hauna tija
katika taifa letu, tumieni muda na fikra
zenu katika kuwashauri wanasiasa masauala yenye maana, ili taaluma zenu ziwe na
manufaa,” Alisema.
“Na
nyinyi wanasiasa, kwa kuwa mmetambua nguvu yengu bila vijana ni ndogo, basi
endesheni saiasa zenu kwa Staha, Weledi na utu,” alisema.
Pia Kibassa
amesema wahadhiri waache kurukaruka kama Njiwa kwa kufundisha vyuo vingi kwa
tama ya fedha, na kuwa kazi yao ni kufanya utafiti wa masuala mbalimbali na
kuwapa wanafunzi.
Amesema
kazi hiyo wawaachie Maprofesa ambao huitwa ili kutoa utaalamu wao kuhusiana na
jambo Fulani.
“Wahadhili
wengi wapo kwa ajili ya kupata manufaa ya kupata fedha, na ndiyo maana unakuta
anafundisha chuo hiki, kile na kile, lakini hiyo si kazi yao, na kuna baadhi
yao wamejiingiza katika kamati za siasa za vyama, wameacha kazi zao za utalaamu
wamegeuka wanaitumikia Siasa,” alisema Kibasaa.
Kibassa
amesema mtaalamu yoyote anapoingia kwenye masuala ya siasa anatakiwa kuachana
na utalaa ili aitumikie siasa.
MWISHO
No comments:
Post a Comment