Mwanne Mussa, Mkazi wa kijiji cha Kiwere akiwa katika shamba lake la Alizeti.
Esau Mwendele mfanyabiashara wa mafuta ya Alizeti katika Soko la Mashinetatu mjini Iringa.
WAKULIMA wa zao la Alizeti wameilalamikia
serikali, kwa kuingiza mafuta mbalimbali ya kula kutoka nje ya nchi, ambayo
yamekuwa yakiuzwa kwa bei ndogo na hivyo soko la zao la Alizeti na mafuta yake
kukosa Soko la uhakika.
Wakizungumzia hali ya soko la
Alizeti wakulima wa kijiji cha Kiwere kilichopo katika Wilaya ya Iringa wamesema awali serikali iliwahimiza kulima zao
hilo, na sasa wanamavuno ambayo hayana soko baada ya wateja kukimbilia mafuta
ya kula ya nje ya nchi ambayo yanayouzwa kwa bei ndogo.
Petro Kikoti amesema kuna haja
serikali ikazuia uingizwaji kutoka nje ya nchi wa bidhaa zitokanazo na mazao ya
kilimo, ili kuwapa fulsa wakulima ya kupta wateja na kukuza soko la ndani ya
nchi.
Naye Esau Mwendele ambaye ni
mfanyabiashara wa mafuta ya Alizeti katika Soko la Mashinetatu mjini Iringa, amesema
biashara ya mafuta hayo imekuwa ngumu, kutokana na tatizo hilo la uingizwaji wa
mafuta ya kula kutoka nje ya nchi.
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Kiwere Yustine Lipita amesema wakulima wengi wamepata mavuno ya kutosha lakini tatizo linalowasumbua ni kukosekana kwa soko, huku badhi ya wafanyabiashara wakitumia mwanya kwa kununua Alizeti kwa bei ndogo.
"Mimi mwenyewe nilikuwa na Alizeti nyingi sana, ambazo nilitegemea kama soko lingekuwa zuri ningeuzwa vizuri, lakini nimelazimika kuuza baada ya kuona nina matatizo na fedha sina, kwa kweli tunaomba serikali jambo hili waliangalie kwa kina ili wasitukatishe tamaa sisi wakulima," Alisema Lipita.
MWISHO
No comments:
Post a Comment