Tuesday, August 20, 2013

SAO HILL YAKABILIANA NA CHANGAMOTO YA MADAWATI


Viongozi wa shamba la Taifa Sao hill, Viongozi wa Kata ya Mtwango na Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi wakipena mikono kama shukrani ya msaada huo wa madawati 100.


SHAMBA la Taifa la miti la Sao hill lililopo katika Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa limejitoa katika aibu ya shule za wilaya hiyo kukosa madawati na hivyo wanafunzi wake kulazimika kuka sakafuni, huku baadhi yao wakitumia madawati mbadala yakutengenezwa kwa udongo na nyasi.
Hatua hiyo imetokana na shule mbalimbali wilayani huo ikiwemo Lugodalutali ambayo wanafunzi wake wanakalia madawati ya udongo almaarufu "Maadobe".

Akikabidhi msaada huo wa madawati 100 kwa shule za Kata ya Mtwango meneja msaidizi wa shamba la Sao hill Shadrack Bijuro alisema shamba limekuwa likitoa vibali vya bure ukataji wa miti kwa vijiji 58 vinavyolizunguka shamba hilo la Sao hill.

Bijuro alisema hatua ya mgao huo imelenga kupunguza ukubwa wa tatizo katika shule husika, ikiwa pamoja na kusaidia ujenzi wa nyumba za walimu, madaktari pamoja na ujenzi wa zahanati.
Aidha alisema kwa miaka minne mfululizo Sao hill imekuwa ikitoa shilingi Milioni 25 kwa vijiji husika ili wakazi wa vijiji hivyo kumaliza matatizo yao wanayoyapa kipaumbele.

Mandalo Abeid Salum afisa misitu idara ya mipango na matumizi ya rasilimali za miti alisema kuna utaratibu wa kutoa migao ya miti kwenye vijiji 58 vinavyozunguka shamba, huku asilimia kubwa ya shule wilayani humo zikikabiliwa na tatizo la madawati.

Alisema rasilimali ya shamba hilo ni kubwa na kuwa kuna umuhimu kwa wananchi husika kutoa taarifa za vipaumbele katika vijiji vyao ili kumaliza changamoto zinazowakabiri kupitia migao ya meta za vibari vya bure vinavyotolewa na shamba hilo.

Afisa elimu ufundi Faustine Mhapa alisema kupitia vibali vya bure kutoka Shamba hilo la Saohilo, wamefanikiwa kupata jumla ya madawati 2469 ambayo yamechongwa na kupunguza tatizo la uhaba wa madawati kwa shule za msingi 32.

Mhapa alisema wilaya ina jumla ya shule za msingi za serikali 173 zenye jumla ya wanafunzi 67, 089 huku madawati yakiwa 11,341 kati ya madawati 17, 403 yaliyopo na hivyo shule 141 zikiwa na upungufu wa madawati.

 
"Mufindi tuna jumla ya shule za msingi 173 za serikali ambazo zina jumla ya wanafunzi 67, 089 na madawati tuliyonayo ni 11,341, kati ya 17, 403 kwa hiyo shule 141 zina upungufu wa madawati," Alisema Mhapa.

Na kuwa katika kipindi cha mwaka 2012/ 2013 jumla ya madawati 2469 yalitengenezwa kupitia utaratibu wa vibali vya kupasua mbao huku jumla ya shule 32 zilizopo katika kijiji cha Kiyowela, Lugema, Lugolofu, Kilolo, Rungemba, Itulavanu, Igowole, Mkalala na Ikwega vikinufaika na mgao huo.

Vijiji vingine ni Itona, Kibao, Ifupira, Ifwagi, Igomtwa, Udumuka, Ibatu, Ihanu, Kilosa, Bumilayinga, Mapnada na Kisada,  kijiji cha Ihomasa, Mkonge, Igoda, Ludilo, Igeleke, Kibengu, Iyegeya, Ugesa na Chogo.

Mhpa alisema licha ya misaada ya mgao huo bado wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa madawati, na kuwaomba wadau wote kuendelea kushirikiana katika kulikabili tatizo hilo kwa lengo la kuboresha mazingira katika sekta ya elimu.

Lidia Lukuvi mkazi wa Mtwango alisema hawaoni sababu ya Wilaya hiyo yenye utajiri mkubwa wa mashamba ya miti kuwa na uhaba wa madawati katika shule zake, huku baadhi ya shule wanafunzi wakikaa sakafuni na wengine kualia madawati ya udongo.

"Hivi miti yote hii unayoiona ni mali yetu, mimi ninashangazwa sana na hali hii, kwani hata hilo shamba la Sao hill ni mali yetu kwakuwa tulitoa sisi ardhi yetu kwa serikali ili ipandwe miti ya Taifa, sasa huwa sielewi nikwa nini shule zetu wilayani hapa nazo zinakumbwa na uhaba wa madawati, hii ni aibu kubwa, Alisema Lukuvi.

 Hata hivyo kuna tetesi ya kuwa baadhi ya vibali vya uvunaji wa miti ambavyo vimekuwa vikitolewa bure na shamba la Sao hill kwa lengo la kuvinufaisha vijiji vinavyolizunguka shamba hilo, kwa kuchonga madawati na kutatuya baadhi ya changamoto zinazowakabiri wananchi, miti hiyo imekuwa ikiingizwa katika matumizi ya watu binafsi.
MWISHO
 
 
 

No comments:

Post a Comment