Mwezeshaji wa mafunzo ya "afya ya uzazi kwa vijana" Meshack Mollel Kutoka shirika la utafiti wa dawa na tiba (AMREF) akitoa somo kwa kundi la wanahabari waliohudhuria mafunzo hayo ambayo yamefanyika Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine SUA mkoani Morogoro.
Mchambuzi wa Sera kutoka shirika la utafiti wa dawa na tiba (AMREF) Bw. Meshack Mollel akitoa mada juu ya uandishi wa habari za afya ya uzazi kwa vijana kwa Waandishi wa habari na Wahariri kutoka mikoa ya Iringa,Njombe,Mbeya,Morogoro na Dar es Salaam katika chuo cha Kilimo SUA Morogoro.
Imeelezwa kuwa hakuna mfumo maalum wa upatikanaji wa taarifa za afya ya uzazi kwa
vijana na kuwasababishia kupata
changamoto mbali mbali ikiwa ni pamoja na maambukizi ya virusi vya Ukimwi,mimba
za utotoni na magonjwa ya zinaa.
Hayo
yameelezwa na mchambuzi wa sera katika shirika la utafiti wa dawa na tiba (AMREF) Bw. Meshack Mollel alipokuwa akizungumza katika semina ya siku
tatu ilitolewa na shirika hilo kwa waandishi wa habari kuhusu haki za afya ya uzazi kwa vijana inayofanyika
katika chuo cha kilimo SUA Mkoani Morogoro.
Aidha amesema vijana wamekuwa hawana elimu sahihi ya afya ya uzazi, kutokana na kukosekana kwa vituo vya utoaji wa taarifa hizo, na hivyo baadhi ya o kujikuta wakipotoshwa kutoka katika vyanzo visivyo rasmi.
Amesema hata tatizo la mimba kwa vijana walio na umri mdogo, linatokana na baadhi yao kuikosa elimu hiyo muhimu, na baadhi yao wakipata maambukizi ya Virus vya Ukimwi, na hivyo nguvukazi kubwa ya Taifa kupotea.
Mollel amesema ipo haja kwa wadau vikiwemo vyombo vya habari kujikita katika kutoa elimu hiyo ya afya ya uzazi kwa vijana ili iweze kuwakia vijana walio wengi, kwa madai kuwa kundi hilo ni robo tatu ya Watanzania.
Na kuwa mpango wa mradi huo ni kuwafikia vijana Laki moja, huku vijana 100 wasio sikia nao wakifikiwa na mrdi huo kwa muda wa kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2011 hadi 2014.
Hata hivyo waandishi hao wamelitaka shirika la AMREF kupitia mradi huo wa "Afya ya uzazi kwa vijana" kuona wakati umefika sasa mradi kuvitumia vyombo vya habari katika kutoa elimu hiyo, ikiwa pamoja na kuwawezesha waandishi kufika maeneo ya nje ya miji ambako ndiko kwenye tatizo hilo la kukosekana na elimu ya afya ya uzazi kwa Vijana.
MWISHO
No comments:
Post a Comment