Mmoja wa watoto wachanga waliozaliwa katika siku ya mkesha wa Sikukuu ya Krismas mkoani Iringa.
Baadhi ya akinamama waliojifungua watoto siku ya mkesha wa kuamkia sikukuu ya X-Maswakisikiliza ushauri kutoka kwa ofisa muuguzi kitengo cha chanjo.
Baadhi ya akinamama waliojifungua watoto siku ya mkesha wa kuamkia sikukuu ya X-Mas wakisubiri kwa hamu kuruhusiwa kurudi nyumbani.
JUMLA
ya watoto wachanga 20 wamezaliwa katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Iringa,
katika mkesha wa sikukuu ya Krismas,
ambapo jamii imewataka wazazi kuwalea watoto hao ili wawe mtaji na mbegu
bora ya Taifa.
Mmoja
wa akinamama waliojifungua mkesha wa siku ya Krismas Bi. Paulina Mgwilanga
amesema anayofuraha kupata mtoto katika siku yenye historia kubwa ya dunia, na
kuwa furaha hiyo ataionyesha pia katika malezi ya mtoto wake huyo.
Naye
Happy Fredy, mzazi aliyejifungua mtoto wa kiume amesema tayari ametoa jina kwa
mtoto huyo ambaye amependekeza aitwe Immanuel, kutokana na jina hilo kuwa na
maana ya “Mungu Pamoja nasi,” na kuwa hilo jina kwake linawakirisha kuzaliwa
kwa Mwokozi Yesu Kristo.
Mariam
Sabula- Afisa muuguzi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa amesema kati ya
watoto 20 waliozaliwa katika siku ya mkesha wa Sikukuu ya Krismas 16 niwakiume
na wane niwa kike.
“Katika
Hospitali hii ya mkoa wa Iringa wanawake 20 wamejifungua watoto usiku wa mkesha
wa sikukuu ya Krismas, ambapo watoto 16 niwakiume na wane niwakike, na
tunachoshukuru nikuwa wazazi na watoto wote hali zao ni nzuri, hakuna aliya na
hali mbaya,” Alisema Sabula.
Lakini
katika kusherehekea siku hii ya X-Mas jamii
imetakiwa kuacha desturi ya kutoa zawadi
na misaada ya vyakula na vinywaji pekee, na badala yake wajikite katika kusaidia masuala
yenye tija hususani sekta ya elimu.
Rai
hiyo imetolewa na mdau wa elimu Mathew Glory Nganyagwa mkazi wa Manispaa
ya Iringa, wakati akikabidhi vifaa vya shule vyenye thamani ya shilingi
Milioni nne kwa wanafunzi zaidi ya elfu tatu wa Kata ya Mseke iliyopo Wilaya ya
Iringa, hiyo ikiwa ni sehemu yake ya kusherekea sikukuu ya X- Mas.
Nganyagwa
amesema ipo haja kwa jamii kubadili mfumo uliozoeleka wa kutoa zawadi na
misaada hasa katika msimu wa sikukuu, na hivyo kujikita katika utoaji wa zawadi
na misaada inayolenga sekta ya elimu.
Akizungumzia
lengo la msaada huo Mathew alisema dhamira ya msaada huo ni kuwapa msukumo
wanafunzi kuipenda zaidi elimu, kwa
kutoa misaada ya vifaa vinavyounga mkono sekta hiyo muhimu, ikiwa pamoja na
kuwakumbusha wananchi juu ya kuzikumbuka shule zenye uhitaji wa vipaumbele
vyenye tija.
Aidha
Mathew aliitaka jamii kuwekeza zaidi katika sekta hiyo ya elimu ili kutatua
changamoto zinazowakabili walimu na wanafunzi shuleni, kwa madai baadhi ya
changamoto hukwamisha jitihada ya upatikanaji wa elimu, ambapo pia ameitaka
jamii kuacha mfumo wa kuchangia masuala yasiyo ya lazima.
“Nimeona
wakati msimu huu wa sikukuu mahitaji ya watoto siyo vyakula na vinywaji pekee, nikakumbuka kuwa kuna zawadi na msaada
muhimu unaosahaulika kama zawadi ya mtoto, na
mimi kama mdau wa elimu nikaona nije kutoa vifaa hivi kwa watoto
wanaotaraji kuanza darasa la kwanza na wale wa sekondari,” Alisema Mathew.
Mdau
huyo wa elimu amekabidhi kwa kila mwanafunzi Madaftari matano, karamu mbili,
mkebe kwa kila mwanafunzi, ikiwa pamoja na Chaki za kuandikia kwa shule zote
zenye uhitaji wa vifaa hivyo.
Mwalimu
mkuu wa shule ya msingi Kaning’ombe Mohamed Mchamba alisema anayo idadi kubwa
ya wanafunzi yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi, ambao wengi wao
wamekuwa wakikosa mahitaji muhimu ya shule.
“Ninao
wanafunzi wengi Yatima na wanaoishi katika mazingira magumu, ambao baadhi yao
hushindwa hata kuandika kutokana na kukosa vifaa kama madaftari na karamu, lakini
msaada huu utawasaidia sana,” Alisema Mchamba.
Sakina
Mwenda mwalimu wa shule ya msingi Makota alisema shule yake inakabiliwa na
changamoto ya uhaba wa Chaki, tatizo ambalo linasababisha walimu kushindwa
kuandika kazi nyingi ubaoni baada ya kubaki na vipande tu vya Chaki.
Naye
mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Kaning’ombe Pascal Mnyifuna alisema msaada
huo umekuja wakati muafaka, kwani wanafunzi wengi wamekuwa wakikosa vifaa vya
shule baada ya wazazi na walezi wao kumaliza fedha katika shughuli za Kilimo na
sikukuu za Krismas na mwaka mpya.
Mnyifuna
alisema kijiji chake kina idadi kubwa ya watoto yatima na waishio katika
mazingira hatarishi na magumu, kutokana na asilimia kubwa ya watoto kulelewa na
bibi au babu zao, baada ya wazazi wao kukimbilia mjini kufanyakazi, huku walezi
hao wakiwa hawana uwezo wa kumudu mahitaji ya wajukuu zao.
“Watoto
wengi hapa unaowaona wanalelewa na bibi au babu zao, siyo kama mama zao
walifariki, hapana, wapo mjini wanafanyakazi, kwa hiyo wazee walio wengi hawana uwezo
wa kuwahudumia wajukuu wao, nah ii ni kutokana na maisha duni
waliyonayo, msaada huu ni mkubwa sana na utasaidia sana kukabilia na changamoto
wanayoipata wanafunzoi kwani baadhoi yao huwa wanakosa hata Karamu na madaftari
ya kuandikia,” alisema Mnyifuna.
Hata
hivyo mratibu wa elimu Kata ya Mseke Eleonora Mwakalundwa alisema shule zake
zinachangamoto ya Chaki, licha ya kuwa serikali imekuwa ikijitahidi katika
kutatua tatizo hilo kwa kuwashirikisha na wananchi.
Mwakalundwa
aaliitaka jamii pia kuiga mfano huo wa uchangiaji wa masuala ya elimu, ikiwa
pamoja na wananchi kuacha imani potofu ya kuwaona wanaochangia kuwa ni watu
wenye kipato kikubwa, huku baadhi yao wakidiliki kuwaita Freemason.
“Ninajua
hapa kumekuwa na tabia ya zamani sana, mtu anapochangia mmekuwa mkimpa majina
mengi na mabaya mara Freemason, na wengine hata wakiwakataza ndugu na jamaa zao
wasijitolee kwa imani ya kulogwa, hayo ni mambo ambayo yamepitwa sana na
wakati, tubadilike na kuona jukumu la uchangiaji wa masuala ya elimu ni yetu
sote,” Alisema Mwakalundwa.
MWISHO
No comments:
Post a Comment