Mh. Tundu Lisu (Chadema) akiwahutubia wananchi wa mji wa Iringa, katika uwanja wa Mwembetogwa.
Mchungaji Peter Msigwa ambaye ni mbunge wa jimbo la Iringa mjini (wa kwanza kiushoto) akiwa na Mh. Tundu Lisu katika viwanja wa Mwembetogwa mjini Iringa.
Mh. Tundu Lisu akisalimiana na baadhi ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza katika mkutano wake.
Bw. Zuberi Mwachula, aliyekuwa mgombea kiti cha ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye kinyang'anyiro cha kura za maoni mwaka 2010, akiteremka katika jukwaa baada ya kukabidhi kati yake ya CCM kwa Mh. Tundu Lisu.
Wafuasi wa Chadema wakisindikiza msafara huo, ambapo gari hilo lilisukumwa mpaka maeneo ya MR. umbali wa km 2 kutoka eneo la mkutano.
Wananchi wakiusindikiza msafara.
Bw. Baraka Kimata, Kada wa Chadema akiwa amesimama na Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa wakisikiliza jambo kutoka kwa Mh. Tundu Lisu.
Maelfu ya wananchi wa Iringa mjini Wakijibu salamu ya CHADEMA "People Power!!" kutoka kwa mh. Tundu Lisu katika mkutano wa hadhara.
MNADHIMU mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, Tundu Lissu, ameilalamikia Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa mikakati ya kupanga kuchakachua rasimu ya mabadiliko ya katiba mpya, kwa madai kuwa rais Jakaya Kikwete amevunja sheria kwa kuingilia majukumu ya tume ya Jaji Joseph Warioba.
Akiwahutubia wananchi wa mji wa Iringa, katika mkutano wa wazi uliofanyika katika uwanja wa Mwembetogwa,Lissu alisema iwapo Rais Kikwete atashindwa kutoa majibu ya ufafanuzi wa hotuba yake aliyoitoa Desemba 31 mwaka huu.
Kutokana na mkanganyiko huo wa kisheria, Tundu Lissu amemtaka Rais Kikwete, atoe maelezo yenye majibu kwa watanzania kabla ya Januari 14 mwaka huu ya kuwa amepata wapi mamlaka ya kuzungumzia kazi za tume hiyo kabla haijakamilisha wajibu wake kumkabidhi kwa mujibu wa sheria.
Aidha Lisu alisema kambi ya upinzani itapeleka hoja binafsi bungeni wakitaka mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba aeleze ni nani kati ya wajumbe wake anayempelekea Rais maneno ya mchakato ambao bado haujakamilika na kukabidhiwa kwake.
“Tunataka Rais atoe ufafanuzi wa mambo matatu makuu kama ambavyo amezungumza katika hotuba yake ya mwisho wa mwaka (Desemba 31). Awe ametoa majibu hayo hadi kufikia Januari 14 lasivyo pale bungeni patawaka moto tutakapoanza vikao mwezi huu,”Alisema Lissu.
Alisema jambo la kwanza wanalotaka Rais Kikwete alitolee ufafanuzi na majibu sahihi kuhusu mamlaka hiyo ameipata wapi ya kuisemea tume ya mabadiliko ya katiba wakati yeye si msemaji wa tume hiyo.
Alitaja jambo la pili linalohitaji majibu ni Rais Kikwete kueleza sheria ipi iliyopitishwa na bunge inampa mamlaka ya kuzungumzia jambo lolote la tume hiyo kabla ya kazi hiyo kukamilika na kukabidhiwa kwake.
Alisema iwapo majibu hayo hayatapatikana hadi kufikia Januari 14, Jaji Warioba ambaye ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba atalazimika kutoa ufafanuzi pale bunge litakapoombwa kufanya hivyo.
Katika mkutano huo, Lissu alimpokea makada wawili wa CCM akiwemo aliyekuwa mshindi wa nafasi ya tatu ya kiti cha ubunge katika jimbo la Mbeya mjini Frank Mwaisumbe (44) na aliyekuwa mgombea kiti cha ubunge kwa tiketi ya chama hicho kwenye kinyang'anyiro cha kura za maoni mwaka 2010, Zuberi Mwachula.
Hata hivyo naye Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) alisema CCM hawana haki ya kuzungumzia juu ya kulikomboa jimbo hilo, kwa kuwa wananchi walipiga kura zao halali, licha yakuwa CCm walitumia fedha nyingi.
"Ndugu zangu nimewasikia hawa viongozi wa CCM wanasema eti wanajipanga kulikomboa jimbo hili, kwani mlinikopesha?? Si mlinipa wenyewe kwa ridhaa yenu, mimi niwahakikishie hawa CCM wanaojinadi kulikomboa jimbo hili wanapoteza muda wao bure, walitumia mamilioni ya fedha na nguvu binafsi lakini nyinyi kwa maamuzi yenu mlinipa mimi, kwa hiyo waache kabisa maneno neno yao ya kuwa eti watalikomboa jimbo hili," Alisema Msigwa.
Naye Mbunge wa viti maalum (Chadema) Chiku Abwao aliitumia fulsa hiyo kutangaza nia yake ya mwaka 2015 kugombea ubunge katika jimbo la Isimani, ambalo sasa linaongozwa na Waziri wa nchi, ofisi ya waziri mkuu, Sera na uratibu wa bunge Willium Lukuvi.
MWISHO
No comments:
Post a Comment