Mh. Ritta Kabati-Mbunge wa viti malumu CCM mkoa wa Iringa, akitoa nasaha kwa vijana walioshiriki tamasha hilo la Kabati Katiba Star Search.
Mh. Ritta Kabati-Mbunge wa viti malumu CCM mkoa wa Iringa, (wa pili kushoto) akishiriki uimbaji.
Kulia- Ni mkurugenzi wa Mnispaa ya Iringa Bi. Teresia Mahongo, akitazama awasanii wakiwajibika jukwaani(hawapo pichani).
Msanii Alfred Mdembwe akitimiza wajibu wake.
Mbunge Ritta Kabati akisubiri ugeni kutoka ofisi mbalimbali mkoani Iringa, ambao walifika katika tamasha hilo kumuunga mkono juu ya kile alichokifanya kwa vijana.
Kamisaa Temmy Mahondo (mwenye Tshirt Nyeusi) akiwa na mratibu wa tamasha hilo la "Kabati katiba star search" Bw. Eddo Bashir.
Wadau wa tamasha hilo wakisubiri kumpata kinara wa mashindano hayo yaliyowashirikisha wasanii 400 wa muziki wa kizazi kipya mjini Iringa.
Msanii Naomi Mgima, akijiandaa kuingia katika ukumbi wa Twisters kushuhudia mpambano huo.
Mh. Ritta Kabati, akitoa taarifa ya mpango huo na malengo yake.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma ambaye alikuwa mgeni rasmi, akisoma hotum juu ya sanaa na wasanii kuwa mfano bora wa kuigwa katika jamaii.
Mbunge Ritta Kabati, akisikiliza jambo kwa makini.
MC-(Master of Sermon) wa shughuli hiyo Bw. Denis Mlowe, akiwajibika vilivyo Stegin.
Mratibu wa shindano hilo, Bw. Eddo Bashir akiwatangaza washindi wa Kabti Katiba Star Search.
Msanii Emanuel Mgata (wa kwanza kulia) aliyeshika cheti ndiye aliyeibuka mshindi wa nafasi ya kwanza wa shindano la Kabati Katiba Star Search, akiwa amesimama na mkurugenzi wa mashindano hayo Mbunge Ritta Kabati.
WASANII wa tasnia mbalimbali nchini wametakiwa kuacha mara
moja kuiga mitindo ya kimagharibi ambayo haiendani na maadili ya kitanzania
ambapo hujikuta wakitengwa na jamii.
Wito huo umetolewa na wasanii wa muziki wa kizazi kipya
(Bongo Flavor) wa mjini Iringa, wakati wa kumsaka mshindi wa shindano la Kabati
Katiba Star Search, lililoandaliwa na mbunge wa viti malumu mkoa wa Iringa
Ritta Kabati, lililofanyika katika ukumbi wa Twisters mjini Iringa.
Wakizungumzia
tabia za baadhi ya wasanii Nickson Sanga na Naomi Mgima walisema kufanya mambo ya kuiga
tabia za nchi nyingine, kunawafanya baadhi yao kutengwa na jamii na hivyo
kushindwa kupokelewa kwa kazi zao na kupoteza fulsa hiyo ya ajira.
Nickson (DJ Nass) alisema endapo kundi la vijana wataitumia vema
fulsa hiyo ya muziki na sanaa ya uigizaji pasipo kufanya masuala yasiyoipendeza
jamii, sanaa hiyo inaweza kutoa ajira kubwa kwa kundi la vijana ambalo
linakabiriwa na changamoto hiyo.
“Mimi ninawasihi vijana wenzangu, kwani ninaona muziki wa kizazi
kipya unatusaidia kwa kutoa ajira kwa vijana nchini, lakini utumiaji wa dawa za
kulevya ni katika mambo yanayoudumaza muziki huu, na kufanya maadali yazidi
kumomonyoka,” Alisema Nickson.
Naomi alisema muziki huo na sanaa ya uigizaji
ni moja tasnia ambazo zimeinua vijana wengi nchini lakini baadhi yao wamekuwa
wakiitumia ndivyo sivyo, kwa kuiga mambo yasiyofaa, na hivyo kuonekana sanaa
hiyo kama ni uhuni.
Aidha alisema changamoto kubwa inayowakabiri
wasanii wa kike, ni pamoja na kukithiri kwa rushwa ya ngono katika hatua
wanazopitia za kufanikisha muziki wao uweze kusikika.
“Sioni kama kuna sababu ya kuwa msanii mpaka
ufanye mambo ya kuishangaza jamii, unajua sisi ni kioo cha jamii, sasa
inatupasa tufanye yale yanayoifunza jamii, na watu waige mambo mazuri kutoka
kwetu, kuvaa nusu uchi siyo ndiyo usanii, huo ni ulimbukeni tu, tena kibaya
zaidi baadhi yetu tunajikuta tukiingia hadi katika matumizi ya dawa za kulevya,
kuna haja ya kuachana na masuala hayo yasiyofaa ili tuwe walimu wazuri katika
jamii yetu ya kitanzania, Alisema Naomi.
Mkurugenzi wa tamasha hilo mbunge Ritta
Kabati, alisema lengo kuu la mashindano ayo, ilikuwa ni kuwakusanya vijana na
kuwapa elimu ya umuhimu wa kutoa maoni ya katiba, kwani asilimia kubwa walikuwa
hawana auelewa huo.
Kabati alisema ili kuwapata vijana wengi
alianza kwa kufanya mashindano hayo, kwani alitambua vijana wengi wanapenda
muziki huo wa kizazi kipya na hivyo baada ya kufanikisha lengo huu, aliendelea
na mashindano ya uimbaji.
Katika tamasha hilo la kumpata mshindi wa
mashindano ya Kabati Katiba Star Search mjini Iringa , mgeni rasmi alikuwa mkuu
wa mkoa wa Iringa Dokta Christine Ishengoma ambaye aliwataka vija kuachana na
desturi zisizofaa ambao zinachangia kuwapoteza.
Akizungumzia matatizo ya wasanii na mpango
mzima wa shindano hilo, mkurugenzi wa Kabati Katiba Star Search, ambaye pia ni
mbunge wa Viti maalumu CCM Ritta Kabati amesema lengo lilikuwa ni kutoa elimu
ya umuhimu wa Katiba, na kutafuta vipaji vya vijana na kuviendeleza.
Dr. Ishengoma aliwasihi vijana kuachana na matumizi ya dawa
za kulevya, ili waendane na jamii ya kitanzania ikiwa ni pamoja na kuinua
vipaji vyao kwani muziki huo umekuwa ukisaidia kutoa ajira kubwa kwa vijana na
hivyo kuachana na utegemezi kwa kukuza uchumi wa vijana.
Shindano hilo ni mara ya kwanza kufanyika, ambapo
jumla ya vijana 400 walijitokeza katika mchakato wa awali ulichukua zaidi ya miezi
miwili kuwachuja ili kupta vipaji vya muziki wa kizazi kipya, kwa lengo la
kusaidia udhamini wa kurekodi nyimbo na
video.
Kwa mujibu wa mratibu wa mashindano hayo,
kamisaa Temmy Mahondo na Muba msanii Emanuel Mgata aliweza kutangazwa kuwa
ndiye mshindi wa kwanza kati ya wasanii 10 walioingia katika awamu ya tatu ya
kumpata mshindi, na hivyo kupata fulsa ya kurekodiwa nyimbo zake bure, audio na
video.
Kuna umuhimu viongozi wengine wakalikumbuka kundi hili la vijana, ambalo ndilo nguzo na nguvukazi ya Taifa, kwa kuwapa mafunzo mbalimbali, kulingana na uhitaji wao, ili kuwawezesha waweze kujitegemea na kupunguza mzigo mkubwa unaowakabiri wa ukosefu wa ajira.
MWISHO
No comments:
Post a Comment