Watu weweeee!!, Baba kapata mama, mama kapata baba!!
Bw. Abdulfatah akimremba mkewe Bi. Mriam. Jaamaniii!!
Maharusi wakiwa na wapambe wao, Bw. Mussa Kawambwa, ambaye pia ni mtangazaji wa kituo hicho.
Bw. Mussa Kwambwa akiteta jambo na Bw. Harus Abdulfatah Murtadha, wakiwa katika sherehe ya kuwapongeza maharusi hao, sherehe iliyofanyika ukumbi wa VETA mjini Iringa.
Bw. Abdulfatah akimvisha pete mke wake Bi. Mariam.
"Mwenzangu pokea pete hii......" Bi. Mriam akimvika Pete mumewe Abdulfatah Murtadha, hiyo ikiwa ni ishara ya kukubaliana kuingia katika mkataba huo wa maisha.

Msimamizi wa maharusi hao akiwapan neno maharusi.
Msimamizi wa maharusi hao akiwapan neno maharusi.
Keki ya harusi ina raha yake usiombe, hasa ukilishwa na umpendae.
Mtu chake bwana!! Manjonjo na vibweka, madoido ya kufurahisha yanaruhusiwa kwa wapendanao, keki hiyo mpaka kumfikia bi harusi Mariam- Bw. harusi alitufanyiwa mazingaombo ya aina yake, alijifanya kama anamtafuta mlaji mwingine wa keki akazunguka ukumbi na kumrudia Bi. harusi wake na kisha kumpa keki. Watu weweeeeeee!!
Ofisa uhusiano wa Ruaha Nationa park, Bi. Risala Meing'ataki akitoa ahadi kwa maharusi, ya kupumzika katika Hifadhi ya Ruaha kwa muda wa siku mbili, huku Maharusi hao wakipewa tunu ya kuwa MABAROZI wa kuitangaza hifadhi yiyo iliyo kubwa na yenye wanyama wengi barani Afrika.
Mmiliki wa mtandao huu, Bi. Oliver Motto, naye akibadilishana mawili matatu na ofisa wa Hifadhi ya Ruaha Nationa Park, Bi. Risala Meing'ataki,
Bi. Neema Msafiri mtangazaji wa kituo cha Ebony fm (Morning Tock) akiwa na mmiliki wa mtandao huu Bi. Oliver Motto, nje ya ukumbi wa Veta.
HAYAWI hayawi mara aaaah YAMEKUWA!! Hatimaye Mhariri wa kituo cha radio Ebony fm cha Mjini Iringa
Bw. Abdulfatah Murtadha amejinyakulia jiko la Gesi (Mke)
Nderemo, Hoi hoi na vifijo vilitawala mjini Iringa baada ya kidume huyo
kuachana rasmi na kambi ya Ukapera kwa kumchagua mwenzi wa maisha yake Bi. Mariam kuwa ndiye chague rasmi la moyo wake.
Harusi hiyo iliyofanyika tarehe 15, huku tarehe 16 wafanyakazi wa Ebony fm wakiandaa sherehe ya kuwapongeza maharusi hao, sherehe iliyofanyika katika ukumbi wa VETA mjini Iringa.
No comments:
Post a Comment